Ukitaka nchi yenye makabila mengi na dini tofauti kama Tanzania iendelee ni lazima uwe na Demokrasia na Uhuru na Haki za binadamu na utawala bora.
Vinginevyo utumie Kabila moja au mawili makubwa au dini moja kubwa kugandamiza wengine kwa kiwango cha kuwatia hofu mpaka wenywee na kuufyata mkia.
Tanzania Kwenye soka bado hatujawekeza vya kutosha kwa sababu watu hawapo huru kutumia vipaji vyao kujitafutia maslahi makubwa ndani na nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa uraia pacha.
Marathoni hatujawaandaa watu wa Ukanda wa Kati na Kaskazini kutokana na kujaribu kuwazibiti badala ya kutumia vipaji vyao kuendeleza Taifa.
Ni wazi kuwa Kwenye Mbia za Marathoni Wa Makabila ya Wameru, Wairaq ,Warangi,Wanyaturu ,Wasonjo, Wabarbeig na Wamasai ndio wanaotisha kwa Kukimbia.
Hawa walipaswa watumiwe vizuri sana na uwekezaji wenye tija kwa vijana wenye vipaji. Leo tungewapita Kenya kwa Mabali sana na Ethiopia mana Sisi Tuna Makabila Mengi zaidi.
Lakini kutokana na Katiba inayotoa Mwanya wa Upendeleo, Ukabila na Udini basi Kila anayeingia madarakani anawaza kupendelea watu wa Kabila au dini yake na kupuuza maeneo mengine kwa kusema wale wasubiri mana sasa ni zamu Yetu.
Tutachelewa sana kwa Katiba hii ya Wakoloni weusi inayolinda Genge la watu wachache na familia zao chini ya Mwavuli wa Chama cha CCM badala ya kulinda maslahi ya Taifa na Mama Tanzania.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app