Siasa za SUGU na VINEGA

Siasa za SUGU na VINEGA

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Mwanasiasa, mwanamuziki, mwandishi na mwanaharakati SUGU ametangaza rasmi kuwa asilimia 33 ya mapato yote ya tamasha litakalofanywa jijini Mbeya na VINEGA zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko hukohuko Mbeya.

Mimi, wewe na wengine wote wanajua kuwa Mbeya ni strategic area kwa shughuli za kisiasa za SUGU. Vilevile sote tulijulishwa kuwa lengo la ANTI VIRUS movement na VINEGA ni kuwakomboa wasanii toka kwenye unyonyaji wa "matajiri". Hii ni kumaanisha kuwa wasanii wawekeze kwa kutumia vipaji vyao ili wajikomboe kiuchumi.

Iwapo mgawanyo wa pesa utakuwa kama ulivyotajwa, basi VINEGA (zaidi ya 20) itabidi wagawane pesa zitakazobaki yaani asilimia 67 toa gharama za investment. Sasa tujiuliye, je huu uwekezaji wa kutoa msaada asilimia 33 ya gross income una tija kwa VINEGA? Jibu lake ni rahisi, kiuchumi/investment hakuna tija. Kwa vile kiuchumi mgawanyo huo hauna tija, je ni kwanini SUGU amesimamia kuhakikisha mgawanyo unakuwa hivyo?

Hapa ndipo tunapokuta kwamba SUGU anawatumia VINEGA kujijengea umaarufu kisiasa. Mkombozi wa kweli wa wasanii wa Bongo (iwapo wanadhurumiwa) bado hajapatikana. SUGU is just another mnyonyaji.

Ninawapa ushauri wasanii wote wanaohusika katika VINEGA kuwa makini na terms za ushirikiano wenu. Msikubali kuyumbishwayumbishwa. Kama kuna haja ya kuchangia maafa basi kila msanii apate pato lake na yeye mwenyewe kwa hiari yake akachangie maafa. Priority yenu number one inapaswa kuwa "KUTOKA KIUCHUMI".

Merry Christmass...
 
nilishawahi kusema na narudia....hii vita ya ruge na sugu ni kwa manufaa yao wenyewew!
 
Sasa hapo cha ajabu ni kipi?ulitaka akupe wewe na familia yako?
 
SUGU NI MAARUFU ZAIDI YA CLOUDS TEAM + REDIO + kiTV. nazani wamekubaliana kusaidia waathirika coz kipato watakao toa ni watu wa mbeya pia sio lazima msanii apate faida wakati wa matatizo ya kijamiii
 
nilishawahi kusema na narudia....hii vita ya ruge na sugu ni kwa manufaa yao wenyewew!

Upeo wa vijana wa leo umejaa ushabiki kiasi kwamba macho yao yametandwa na giza. Wao hawaoni tatizo, mpaka siku wanashtukia washatumiwa sana.
 
SUGU NI MAARUFU ZAIDI YA CLOUDS TEAM + REDIO + kiTV. nazani wamekubaliana kusaidia waathirika coz kipato watakao toa ni watu wa mbeya pia sio lazima msanii apate faida wakati wa matatizo ya kijamiii

Kilichoongelewa hapa siyo umaarufu. Jaribu kusoma vizuri utaelewa kilichoandikwa.
 
unaakili nyepesi sana mchumba mbona unaonekana kuingilia makubaliano yao yakuchangia jamiiiiii, umetumwa na ruge nini au huwa unawananihiii
 
Nilishazungumza hao vinega wanatumiwa tu na sugu kulipiza kisasi kwa ruge,hao vinega ni kenge waliokwenye msafara wa mamba wawili wenye ugomvi yoo
 
Nafikiri ujumbe umefika mkombozi wa wasanii hawezi hata siku moja akawa politicians, kwa lugha rahisi sugu anawatumia tu kwa maslahi yake ya kuwawini wanambeya.
 
Kwani haiwezekani kuwa hao vinega wakawa wameamua kujitolea kuwasaidia wahanga?
Show imeenda Mbeya wakati wa maafa so wanawasaidia wenzao, am sure ingekuwa inapigwa Dar now pia wangejitolea kuwachangia wahanga wa mafuriko.

Je Vinega walipotoa wimbo kwa ajili ya wahanga wa Meli ilozama Nungwi pia ilikuwa ni Sugu Na Siasa?

Je wewe kesho utaogopa kumsaidia ndugu yako kidogo kisa unahisi ni umaarufu unatafuta?

Hii inaitwa "giving back to community" rafiki yangu. Utajiri wa hao wasanii unatokana na michango inayopatikana kwenye mauzo ya albums na shows zao, na wateja ni hao wananchi ambao ndio wahanga wenyewe nw kuna ubaya wakirudishiwa japo kidogo wajikwamue na janga kuna ubaya?

Na hiyo ni kama wananchi wa Mbeya wamepata platform ya kuwasaidia wenzao kupitia wawakilishi waaminifu.

Muziki na Maisha ndio hii sasa.
Songa Mbele Sugu, Songa Mbele Vinega.
 
mwanasiasa, mwanamuziki, mwandishi na mwanaharakati sugu ametangaza rasmi kuwa asilimia 33 ya mapato yote ya tamasha litakalofanywa jijini mbeya na vinega zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko hukohuko mbeya.

Mimi, wewe na wengine wote wanajua kuwa mbeya ni strategic area kwa shughuli za kisiasa za sugu. Vilevile sote tulijulishwa kuwa lengo la anti virus movement na vinega ni kuwakomboa wasanii toka kwenye unyonyaji wa "matajiri". Hii ni kumaanisha kuwa wasanii wawekeze kwa kutumia vipaji vyao ili wajikomboe kiuchumi.

Iwapo mgawanyo wa pesa utakuwa kama ulivyotajwa, basi vinega (zaidi ya 20) itabidi wagawane pesa zitakazobaki yaani asilimia 67 toa gharama za investment. Sasa tujiuliye, je huu uwekezaji wa kutoa msaada asilimia 33 ya gross income una tija kwa vinega? Jibu lake ni rahisi, kiuchumi/investment hakuna tija. Kwa vile kiuchumi mgawanyo huo hauna tija, je ni kwanini sugu amesimamia kuhakikisha mgawanyo unakuwa hivyo?

Hapa ndipo tunapokuta kwamba sugu anawatumia vinega kujijengea umaarufu kisiasa. Mkombozi wa kweli wa wasanii wa bongo (iwapo wanadhurumiwa) bado hajapatikana. Sugu is just another mnyonyaji.

Ninawapa ushauri wasanii wote wanaohusika katika vinega kuwa makini na terms za ushirikiano wenu. Msikubali kuyumbishwayumbishwa. Kama kuna haja ya kuchangia maafa basi kila msanii apate pato lake na yeye mwenyewe kwa hiari yake akachangie maafa. Priority yenu number one inapaswa kuwa "kutoka kiuchumi".

Merry christmass...

huna hoja
 
Kwani haiwezekani kuwa hao vinega wakawa wameamua kujitolea kuwasaidia wahanga?
Show imeenda Mbeya wakati wa maafa so wanawasaidia wenzao, am sure ingekuwa inapigwa Dar now pia wangejitolea kuwachangia wahanga wa mafuriko.

Je Vinega walipotoa wimbo kwa ajili ya wahanga wa Meli ilozama Nungwi pia ilikuwa ni Sugu Na Siasa?

Je wewe kesho utaogopa kumsaidia ndugu yako kidogo kisa unahisi ni umaarufu unatafuta?

Hii inaitwa "giving back to community" rafiki yangu. Utajiri wa hao wasanii unatokana na michango inayopatikana kwenye mauzo ya albums na shows zao, na wateja ni hao wananchi ambao ndio wahanga wenyewe nw kuna ubaya wakirudishiwa japo kidogo wajikwamue na janga kuna ubaya?

Na hiyo ni kama wananchi wa Mbeya wamepata platform ya kuwasaidia wenzao kupitia wawakilishi waaminifu.

Muziki na Maisha ndio hii sasa.
Songa Mbele Sugu, Songa Mbele Vinega.

Puppy,
Are you convinced kwamba hao VINEGA hawana matatizo ya kutatua makwao? If yes, kwanini waamuliwe na kamati ya maandalizi kuwa theluthi (33%) inabaki kwenye shughuli za siasa za SUGU. Hii asilimia ni kubwa mno, hata Bill Gates hawezi kufanya hivi. This is not giving back to the community, this is buying the community politically kwa kutumia vipaji vya VINEGA.
Jaribu kufikiria asilimia 33 ya kipato chako, then jiulize kama unaweza kwenda kukitoa charity, then kumbuka kuwa hiyo inayobaki wanagawana VINEGA wote.
 
Nilishazungumza hao vinega wanatumiwa tu na sugu kulipiza kisasi kwa ruge,hao vinega ni kenge waliokwenye msafara wa mamba wawili wenye ugomvi yoo

Watu wamejitolea kuchangia jamii mnalaumu nini ninyi? We umejitolea nini? ***** kabisa :angry:
 
Back
Top Bottom