ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Mwanasiasa, mwanamuziki, mwandishi na mwanaharakati SUGU ametangaza rasmi kuwa asilimia 33 ya mapato yote ya tamasha litakalofanywa jijini Mbeya na VINEGA zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko hukohuko Mbeya.
Mimi, wewe na wengine wote wanajua kuwa Mbeya ni strategic area kwa shughuli za kisiasa za SUGU. Vilevile sote tulijulishwa kuwa lengo la ANTI VIRUS movement na VINEGA ni kuwakomboa wasanii toka kwenye unyonyaji wa "matajiri". Hii ni kumaanisha kuwa wasanii wawekeze kwa kutumia vipaji vyao ili wajikomboe kiuchumi.
Iwapo mgawanyo wa pesa utakuwa kama ulivyotajwa, basi VINEGA (zaidi ya 20) itabidi wagawane pesa zitakazobaki yaani asilimia 67 toa gharama za investment. Sasa tujiuliye, je huu uwekezaji wa kutoa msaada asilimia 33 ya gross income una tija kwa VINEGA? Jibu lake ni rahisi, kiuchumi/investment hakuna tija. Kwa vile kiuchumi mgawanyo huo hauna tija, je ni kwanini SUGU amesimamia kuhakikisha mgawanyo unakuwa hivyo?
Hapa ndipo tunapokuta kwamba SUGU anawatumia VINEGA kujijengea umaarufu kisiasa. Mkombozi wa kweli wa wasanii wa Bongo (iwapo wanadhurumiwa) bado hajapatikana. SUGU is just another mnyonyaji.
Ninawapa ushauri wasanii wote wanaohusika katika VINEGA kuwa makini na terms za ushirikiano wenu. Msikubali kuyumbishwayumbishwa. Kama kuna haja ya kuchangia maafa basi kila msanii apate pato lake na yeye mwenyewe kwa hiari yake akachangie maafa. Priority yenu number one inapaswa kuwa "KUTOKA KIUCHUMI".
Merry Christmass...