Siasa za Tanzania huwa zinanifanya nikumbuke Wakenya tumetoka mbali

Siasa za Tanzania huwa zinanifanya nikumbuke Wakenya tumetoka mbali

Nilishahisi tu story zenu bila kutaja Tanzania haiwi story

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app

Hili jukwaa japo limetengewa mambo ya Wakenya, lakini Watanzania ndio wengi huja kutoa maoni, hivyo inabidi kuwataja. Sijaona Mkongoman au Mganda humu.

Hivyo jadili hoja wacha kulia lia.
 
Hongera sana kwa kuwa mfuasi mzuri wa siasa za Tanzania. Ni vyema ungeangalia kwa M7 na Rwanda nako kunafurahisha sana.
Huyo anayetaka kufukuza watu ni Msukuma anayetokea Usumani-Mwanza, hivi anaweza kwenda Maneromango na kumfukuza Mzaramo? La hasha kijana Makonda alikuwa anastarehesha barza. Anajua fika kumtoa Mzaramo wa Maneromango, ubavu huo hana!!
 
Huwa napata shida sana nikiona Wakenya wanzangu humu wakiponda nchi yetu huku wakidai kwamba tupo nyuma sana kidemokrasia na kwenye mambo mengi. Lakini kwa baadhi yetu ambao tumepata fursa ya kuzitembelea nchi zote majirani kama vile Sudan Kusini, Uganda, Ethiopia, Tanzania, Burundi, Rwanda na Kongo huwa tunawashangaa sana hawa Wakenya wasiokua na shukrani hata kidogo.

Nimeona sehemu kauli za mkuu wa mkoa Dar es Salaam, kwamba kasema ".., Ninao uwezo wa kumfukuza mtu yoyote ndani ya mkoa wangu kwa masaa ninayotaka mimi na asiondoke na chochote zaidi Ya ndala alizovaa." - Paul Makonda, RC, Dar-es-salaam

Tundu Lissu: Makonda hana mamlaka anayojidai nayo ya kuhamisha watu

Sasa nawaza hapa gavana wa Nairobi leo hii akatumia maneno kama hayo, aisei sidhani kama hata anaweza kuvumilia moto unaoweza kumkuta maana atapondwa hadi hata na wafuasi wa chama chake. Kule Bongo hata kuna mbunge yule wa Arusha yupo jela siku nyingi kisa kasema ameota ndoto kumhusu rais, wakati hapa kwetu rais mnampa majina ya kila aina ila yote anaona sawa na kuwachekea tu.

Wakenya ambao hujifanya kichaa na kuponda nchi yetu mfikirie sana, hama nenda uishi hata miezi michache ndani ya hizi nchi majirani uone ukirudi utakua umetia akili. Ilitugharimu sana kufikia hapo tulipo, baadhi yetu nikiwemo tilipgwa mabomu ya machozi na kuumizwa sana kipindi tunapambana kupigania hii demokrasia ambayo tunajivunia leo. Kila Mkenya alihusika kwa namna moja au nyingine.

I think you are making some sense out of your writing. I can agree with you on some of the issues. To be honest, you are somehow far ahead of us katika suala la uhuru wa kujieleza na ni kweli Kenyans wanajitambua zaidi kuliko Tanzanians. Mengine yanajadilika though
 
Kwani lazima kujilinganisha na sisi? Fanyeni yenu, kila kitu ni mtazamo tu.
 
Hata hapa Tanzania tayari RC kasema anauwezo wa kumfukuza mtu Dsm. Mimi nimejihami nahamisha vilivyo vyangu narudi Kulima vinyungu Mufindi

Kusema yanasemwa mengi isitoshe unachanganya mambo, RC siyo mwenyeji wa Dar lkn Kenya ni kwamba wenyeji ndiyo wanaofukuza wasio wenyeji, kama RC akifukuza watu hiyo ni Serikali ndiyo inafanya hivyo siyo ubaguzi bali utakuwa ni mfumo wa nchi lkn Kenya ni Ubaguzi perse!
 
Siasa za Kenya na Tanzania ni tofauti na hazifanani hata kidogo.

- Siasa za Kenya zimejaa ukabila, Raila Odinga hata akisema wajaluo wenzake waandamane uchi watafanya - amewafanya misukule wa kutisha. Yaani wako tayari hata kuuawa wakimtetea mjaluo
mwenzao
Wakati Tanzania hakuna ujinga wa kiwango hicho - Hakuna mmasai anayeweza kushawishiwa na mchagga andamana kiasi cha kupigwa hata risasi akakubali

- Kenya ni watu wa kukopi na kupesti, wamekopi katiba ya Marekani kiasi kwamba wabunge wanakataa hata kula chakula cha kantini la bunge na kufanya ziara ya kwenda kula ulaya

- Wanasiasa wa kenya ndio matajiri wa kutisha na wenye nguvu ( WEALTH & POWER ) Wakenya wengine ni nyumbu, watumwa na masikini wa kutisha ndio maana wamekuwa wezi wakubwa duniani kote, wakati hapa kwetu hakuna mtu mwenye hizo nguvu za kutisha

- In Tanzania there's neither strong families nor strong politicians, mtu yeyote anaweza kuisoma namba at any time t

N.B Usifananishe Tanzania na mambo ya kijinga
 
Tuongee tu ukweli. Wale madaktari wakenya ingekuwa bongo wangeshatimuliwa kazi, kinachopendeza Kenya ni swala la ugatuzi hapo kwakweli wametuzidi.Japo yapo mapungufu ya ukabila.Tanzania siasa imeathiri kila idara. Tuwe tunakubali kukosolewa ili tujirekebishe jamani.
 
Kwa hiyo ni bora watu wasio na hatia kufa ili kulinda mfumo? Hivi mpaka sasa unajuwa ni watoto wangapi wamekufa kwajilu ya mama zao kukosa huduma salama ya kujifungua. Mifumo mingine inakandamiza masikini na kulinda walio juu.
 
Ingekuwa Tanzania huo mgomo ungekuwa ushakwisha, Kenya madaktari wameona wanakaribia uchaguzi - kwahiyo wanatumia nafasi hiyo kushnikiza mambo makuubwa ambayo hata nchi labda haiwezi kuwapa kwa sasa kwa lengo la kuwaharibia JUBILEE Kisiasa , yaani hapo Madaktari wanavyoendelea na mgomo CORD wanachekelea.
 
Tanzania ya sasa ni kama Kenya ya Moi.....
mmetuacha mbali kiukweli

Sisi watu wanafungwa kwa ku comment kitu watsaap na Facebook...
 
Huwa napata shida sana nikiona Wakenya wanzangu humu wakiponda nchi yetu huku wakidai kwamba tupo nyuma sana kidemokrasia na kwenye mambo mengi. Lakini kwa baadhi yetu ambao tumepata fursa ya kuzitembelea nchi zote majirani kama vile Sudan Kusini, Uganda, Ethiopia, Tanzania, Burundi, Rwanda na Kongo huwa tunawashangaa sana hawa Wakenya wasiokua na shukrani hata kidogo.

umeongea kweli tupu...wanaokupinga ukweli wanaujua ila ndo hivyo tena wanalipwa kwa kupinga ukweli.
 
Hongera sana kwa kuwa mfuasi mzuri wa siasa za Tanzania. Ni vyema ungeangalia kwa M7 na Rwanda nako kunafurahisha sana.
Huyo anayetaka kufukuza watu ni Msukuma anayetokea Usumani-Mwanza, hivi anaweza kwenda Maneromango na kumfukuza Mzaramo? La hasha kijana Makonda alikuwa anastarehesha barza. Anajua fika kumtoa Mzaramo wa Maneromango, ubavu huo hana!!

Dah kule kwa M7 hata usitaje maana kuna jamaa moja anaitwa Besigye ambaye imekua desturi lazima achezee kibano kwenye kila uchaguzi, M7 inabidi kuhakikisha huyo jamaa asije kuwa rais maana lazima atalipiza kisasi.

Nimecheka sana hilo la kusema Msukuma ametokea Mwanza na kwenda kung'anga'nia kumfukuza Mzaramo kwao, Barbosa haamini linawezekana.
Lakini twende mbele na kurudi nyuma hatua chache, Makonda naona kwa hili la kupigana na biashara ya madawa ya kulevya anaonekana kushinda vita. Nampongeza sana kwa hilo, mambo mengine inabidi kujifanya kichwa cha mwenda wazimu ili kuyafanikisha. Naomba mtuazime huyo jamaa aje Mombasa maana huko imekua kama kiwanda cha haya mambo, vijana wetu wa kule wanaisha...twafa.
 
nilishawahi kusema na Leo narudia tena,tatizo la wakenya wengi waliofungua account JF,wanaingia JF kwa misukumo miwili tu,nayo ni kuisifia kenya kwa nguvu zote na kushambulia nchi majirani hususani Tanzania.

matokeo yake ni kwamba anapotokea Mkenya wa kupost topic/post zinazo eleza ukweli kuhusu hali halisi ya maisha ya kenya kisiasa na kiuchimi,anaonekana kama anavunja masharti ya tambiko la ukoo.basi wakenya wote wataanza kumshambulia.

kuna Mkenya mmoja hapa anaitwa Juakali1980 .huyu yeye kaamua kuisimamia kweli maana waungwana kusema kweli itakuweka huru.

yeye yupo tofauti na kundi la kina MK254 ,topic/post zake siku zote zinajaribu kutoa picha halisi ya maisha ya wakenya(kiuchumi na kisiasa).

Nina hakika,hata hii mada aliyoianzisha M254,imelenga kum-counter attack juakali1980.maana inaonekana anaenda kinyume na tambiko la ukoo kwa kutoa siri za ukoo hadharani.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwa hiyo ni bora watu wasio na hatia kufa ili kulinda mfumo? Hivi mpaka sasa unajuwa ni watoto wangapi wamekufa kwajilu ya mama zao kukosa huduma salama ya kujifungua. Mifumo mingine inakandamiza masikini na kulinda walio juu.
Unajua akili za watu sijui huwa zinawaza nini ndugu yangu - Mfano hao madaktari wakipewa wanachotaka ( ingawa wanashnikiza Kwa influence ya kisiasa ) watarudisha uhai wa waliopotea ? Siasa zinapoingizwa kwenye masuala muhimu ndo hivi - Mtu kama unajiona daktari mzuri ( global doctor ) na malipo unayopewa hayakutoshi, acha kazi katafute wanakolipa vizuri - siyo kulazimisha nchi ikulipe kila kitu wakati haina uwezo huo kwa wakati huo !
 
Dah kule kwa M7 hata usitaje maana kuna jamaa moja anaitwa Besigye ambaye imekua desturi lazima achezee kibano kwenye kila uchaguzi, M7 inabidi kuhakikisha huyo jamaa asije kuwa rais maana lazima atalipiza kisasi.

Nimecheka sana hilo la kusema Msukuma ametokea Mwanza na kwenda kung'anga'nia kumfukuza Mzaramo kwao, Barbosa haamini linawezekana.
Lakini twende mbele na kurudi nyuma hatua chache, Makonda naona kwa hili la kupigana na biashara ya madawa ya kulevya anaonekana kushinda vita. Nampongeza sana kwa hilo, mambo mengine inabidi kujifanya kichwa cha mwenda wazimu ili kuyafanikisha. Naomba mtuazime huyo jamaa aje Mombasa maana huko imekua kama kiwanda cha haya mambo, vijana wetu wa kule wanaisha...twafa.
Ni kweli kwa Mombassa ambapo mimi nina unasaba nako kwa kweli hali sio nzuri. Mji jirani nao uko kwenye harijojo. Yaani kama ukifika Tanga tembelea Chumbageni uone vijana walivyokwisha. Yaani Chumbageni Stars kwishne, mpira woooote tulokuwa tunaringia margoooro. Ule umwamba wa Tanga kwenye mpira umepotea kabisa, sasa sifa imehamia kwenye uwezo wa tumbo kubeba kete nyingi!! Inasikitisha sana.
 
Yaani majanga kwa kweli, halafu vigogo wa nchi ndio wananufaika.
 
Tz ?..tusilinganishe vitu vya kipuuzi na kenya...sisi ni "ma....f..la"...tuliambiwa pale jangwani..na its the reality...hate it or like it...mbuzi tu!...bravoo kenya!
 
Back
Top Bottom