Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?

Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?

Kuna mambo meeengi hauyaelewi, hata najisikia uvivu kuandika na kukuelezea hapa. Nenda ofisini kwa Kalemani watakwambia kwanini wameingia hayo makubaliano.
 
Kuna mambo meeengi hauyaelewi, hata najisikia uvivu kuandika na kukuelezea hapa. Nenda ofisini kwa Kalemani watakwambia kwanini wameingia hayo makubaliano.
Tupo 55M, sasa kila mmoja akisema aende kwa Ofisini kwa Kalemani akaambiwe hayo, HIVI HUYO WA MILIONI 55 ATASUBIRI SIKU NGAPI HADI APATE NAFASI YA KUWAONA?
 
Je, mahitaji ya sasa ya umeme yanajitosheleza kabla ya hiyo SG kukamilika hiyo 2023?

Hiyo mikataba mipya iliyoingiwa ni ya kuuziana kwa muda wa miezi/miaka mingapi?
 
Matumizi ya umeme wa gas ile tuliyokuwa tunaimbishwa uchumi wa gas kama wendawazimu yameishia wapi?
Kuhusu umeme wa Gas ,Serkali iliachana na suala hilo kutokana na gharama kubwa sana katika mradi huo (hadi mradi kukamilika unahitaji kama nusu bajeti ya Tanzania nzima) hivyo mradi umesimama kuepuka kuendesha mradi kwa hasara.
Wadhamini wa mradi huu wapo,lakini wanataka cha juu zaidi jambo ambalo mh jiwe hawezi kuona linatendeka.
Kuhusu haya makampuni 6 ,acha tusubiri litajibiwa vipi. Huenda wanamaana kubwa ambayo sisi wananchi hatuielewi.
#jr
 
Nafikiri miradi hiyo ni ya hydro na ni economic haina gharama kama matumizi makubwa ya mafuta masharti ya kinyonyaji kama standing charges na gharama za kifisadi.

Pamoja na bwawa la mwalimu nyerere wawekezaji wadogowadogo inazidisha tija maana mahitaji ya umeme yataongezeka kufuatana na uchumi unavyokua.

Pia tanesco kwa utaratibu wetu inahodhi usambazaji na uuzaji wa umeme kwa hivyo ni sahihi kila mzalishaji wa umeme wa kuuza aweze kua na maelewano ya kuuza umeme wake tanesco kusudi uweze kusambazwa.

Muhimu ni kuona mikataba ya tanesco na wazalishaji binafsi ina tija na hakuna ufisadi unatendeka
 
Haw oka watu wakiwauzia Tanesco Ni Bora zaidi kuliko kuwauzia wananchi direct mana wanachi wanawezapigwa 3 times,

Mbali na kutakiwa kuonyesha mikataba ilitakiwa waonyeshe mitambo inayozalisha umeme mfano uko njombe, na kigoma ,nadhani hii mitambo inatumia maji , mara nyingi hii mitambo , huwa haipo katika site husika. Mfano Ni wananchi Ilungu walivyopigwa ela zao na watu wanaozalisha umeme hewa.
 
Kuna wananchi wa Ilungu wamepigwa mpaka Basi, Tena miundo Mbinu ambayo haiko standard , na mradi wa kuzalisha umeme usifanikiwe zaid ya kuamua kuunganishwa naumeme wa Tanesco.
 
Huku Zanzibar umeme usije nunua mwisho wa mwezi au mwanzo wa mwezi, katikati ya mwezi 10,000 unapata unit 32 , ukinunua mwisho wa mwezi au mwanzo unapata units 22 ,

Wizi balaa ZeCo
 
Umeme unaosemwa tunazalisha ni kiwango kidogo mnoo kwa viwanda 12ambavyo lazima vijengwe na vingine ni kwa muda mfupi ujao.

1) LNG Industrial complex in Lindi 490 mw .
2) Mchuchuma/ Liganga Iron Ore Complex 540mw - Liganga.
3) Kigoma Cement plant 240mw - Kigoma.
4) Fertilizer / Urea industria complex - Kilwa. Expert port facilities 158mw.
5) Hellium Gas Processing Complex 80mw.
6) Post harvest industries for Cashewnuts, Cotton, Textiles, and allied industries 540mw.
7) Nickel-Cobalt complex in Ngara - Kagera 350 Mw.

8) SGR - Rail network and supporting repair/ Services centers 70mw.

9) Matumizi ya umeme shuguli za kijamii, viwanda vya kati na vodago (medium and small industries )utafiki a 3500 Mw 2020-2035.

10) Uranium refining processes.
11) Coal mining services and Coal dressing for export- 30 Mw.
12) Fish Industrial processes and Cold chain network 35 Mw.
13) Bagamoyo Port facility / Export Manufacturing Complexes 350 Mw.

Tunahitaji umeme wa MW 15000 kuweza kuendesha uchumi wa 9000 Billion Dollars. Kwa 2020- 2035.

Na hii miradi itatekelezwa karibu yote kwa miaka 7 mpaka 12 kuanzia 2020 to 2032.
 
Kwako mleta mada na wote wanaopitia uzi huu.

Tanzania imeridhia utekelezaji wa Sustainable Development Goals (SDGs). Mmoja wapo ya SDGs ni goal namba saba inayohimiza upatikanaji wa nishati/umeme wa bei nafuu, msafi, na endelevu tena kwa ufanisi. Nishati hii ni nishati jadidifu( renewable energy). Kwenye miradi yote uliyotaja ambayo Tanesco ameingia mikataba sita, hakuna hata mmoja unaozalisha umeme kwa njia ya kuchakata mafuta ya ukaa/ fossil fuel. Miradi yote ni ya nishati jadidifu ( labda kama kizungu ulichowasilisha kiwe kimenipiga chenga).

Pia Tanzania kupitia sera yake ya Nishati ya mwaka 2015, inahimiza ongezeko la matumizi ya nashati jadidifu katika ujumla wa matumizi ya nishati hapa nchini.

Kwa sasa nadhani bado Tanzania tuna kiasi cha umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta ya ukaa. Na madhara ya matumizi ya mafuta ya ukaa ni pamoja kuzidisha athari hasi za mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo juhudi za kumaliza kabisa uzalishaji wa umeme kutokana na mafuta hatuna budi kuziunga mkono.

Kwa maelezo hayo hapo juu, Mimi, TUJITEGEMEE na raia ambaye nimewahi kupitia makabrasha Ya sera na maridhiano ya nchi juu ya masuala ya nishati, ninadhubutu kuunga mkono hatua Ya Tanesco kuingia mikataba hiyo sita.

Na karibisha ukosoaji.
 
Kitu kikubwa unachotakiwa kukijua ni miradi ipi hufanywa na Tanesco na miradi ipi hufanywa na hao independent power producer.
Kwa mfano vyanzo vya hydro power vyenywe kuweza kuzalisha me 10 au chini ya hapo haifanywi na Tanesco kwani ni mradi mdogo , lakini haizui mtu binafsi kufanya miradi hiyo na kuiuzia Tanesco au majirani zako.
Sasa ktk mada hii , umeme uliozungumzia ni mw 19 hivi.
We renewable energy, sasa cha angalia hapa was it economic reasonable kwa Tanesco to do it independently from the scratch au kumuacha P afanye then awauzie Tanesco
 
Jamaa anataka kuonekana

Kumbe wenzake washakaa na kujadili


Anadhani labda MD wa tanesco au bodi inekurupuka.

Wakati Wana baraka toka huko juu

Unless iwe ile ya" tengeneza tatizo halafu litatue ,Kisha wewe Ni shujaa"

Huyo atamaliza hii Miaka 5 hapati teuzi

Ye anadhani mkuu kasahau lile swali lake pale ikulu[emoji1787]

Analikumbuka ndio Hana habari wewe coz we Ni mnafiki wa wazi wazi at least wengine
 
Kwani imekuwa nongwa kwa Pascal kuwa kada wa CCM ? Tuzungumzie umeme na dio mada husika hapa. Mkuu tujenge na kulinda heshima ya hili Jukwaa kwa wivu mkubwa.
 
Mbona gas inatumika ww tatizo lako nn nenda Kinyerezi pale ukajionee..!

Tuliambiwa huo umeme wa gas utatoa 5,000mg, kuna megawati ngapi mpaka sasa? Kwanini tuachane na kuzalisha hizo 5,000mg turukie 2,115mg, ambapo wanaoimba umeme wa maji leo hii utetezi wao kwenye umeme wa gas ilikuwa ni mabadiliko ya tabia nchi. Toka nje ya box mzee baba unaingizwa mjini. Usishangae akaja rais mwingine na deal lake la umeme wa makaa ya mawe au upepo, kisha ww ukatumika tena kutetea milo ya watu.
 
Back
Top Bottom