Kwako mleta mada na wote wanaopitia uzi huu.
Tanzania imeridhia utekelezaji wa Sustainable Development Goals (SDGs). Mmoja wapo ya SDGs ni goal namba saba inayohimiza upatikanaji wa nishati/umeme wa bei nafuu, msafi, na endelevu tena kwa ufanisi. Nishati hii ni nishati jadidifu( renewable energy). Kwenye miradi yote uliyotaja ambayo Tanesco ameingia mikataba sita, hakuna hata mmoja unaozalisha umeme kwa njia ya kuchakata mafuta ya ukaa/ fossil fuel. Miradi yote ni ya nishati jadidifu ( labda kama kizungu ulichowasilisha kiwe kimenipiga chenga).
Pia Tanzania kupitia sera yake ya Nishati ya mwaka 2015, inahimiza ongezeko la matumizi ya nashati jadidifu katika ujumla wa matumizi ya nishati hapa nchini.
Kwa sasa nadhani bado Tanzania tuna kiasi cha umeme unaozalishwa kwa kutumia mafuta ya ukaa. Na madhara ya matumizi ya mafuta ya ukaa ni pamoja kuzidisha athari hasi za mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo juhudi za kumaliza kabisa uzalishaji wa umeme kutokana na mafuta hatuna budi kuziunga mkono.
Kwa maelezo hayo hapo juu, Mimi, TUJITEGEMEE na raia ambaye nimewahi kupitia makabrasha Ya sera na maridhiano ya nchi juu ya masuala ya nishati, ninadhubutu kuunga mkono hatua Ya Tanesco kuingia mikataba hiyo sita.
Na karibisha ukosoaji.