Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?

kwamba niwambie nitazikwa wapi😂😂😂😂..
Pamoja katika ujenzi wa taifa.goja nitafte fact 100% then nakuja hapa tena.

Kumbe hata hukuwa na facts? Si ulisema sijasikia ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika, kwa mantiki ya kuwa ww ulisikia? Haya boss, kasake facts uje uzimwage hapa jukwaani. Tena hizo facts uzifungulie uzi wake kabisa.
 
Kumbe hata hukuwa na facts? Si ulisema sijasikia ufafanuzi kutoka kwa mamlaka husika, kwa mantiki ya kuwa ww ulisikia? Haya boss, kasake facts uje uzimwage hapa jukwaani. Tena hizo facts uzifungulie uzi wake kabisa.
msssiuuu eti sikuwa na fact!! Sasa nimejuwaje yote hayo?? Unaanza kukwama wapi mkuu?? Au kusema nitafte ukweli zaidi unaona kama umeshinda hii battle??
Sipendi kubishana bila evidance,sipendi uongo napenda ukweli na nitasema ukweli daima. Tatzo unakurupuka kuja kutoa mapovu bila kufanya utafti kama wenzako.Tatfa ushahidi then uje hapa,usilete story za kwenye kahawa mkuu.Sijapenda...
Sifungulii uzi wala nini,nitakutafta nikupe ushahidi woooote,nadhani baada ya ukweli huo nitakuwa nimekuokoa na kazi ya kuabudu hapo ufipa.
#Lengo ni kujenga sio kubomoa!!
 
Ingekuwa vizuri ungeweka conclusion baada ya kuweka bei ya huo umeme. Vile vile inaonekana mradi huu wa wazalishaji wadogo haukuanza leo, information za ziada zinahitajika ili kuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka. Je walianza huo mpango lini? Kama unafahamu ingekuwa jambo la maana kulifahamu.

BTW mradi wa JNHPP utakuwa unategemea maji ndio sababu kama sikosei kutakuwa na mabwawa ya ziada endapo kutatokea ukame nk. Kama tutakuwa na umeme mwingi sio vibaya tukawauzia majirani ambao watakuwa wanahitaji. Solar energy in a long run ndio utakuwa nafuu zaidi lakini mwanzo ni ghali. Ni vizuri Tanzania kukumbatia kila aina ya nyezo ya kuwezesha kuwa na wigo kubwa wa upatikanaji wa umeme.
 

Nimecheka kwa nguvu haya maelezo yako. Nilijua lazima utapanick. Haya nasubiri hizo facts, ili niache kusujudia Ufipa.
 

Iwapo bwawa la JNHPP kutatokea ukame, sasa ikitokea ukame hayo mabwawa mengine huo ukame hautafika?
 
Matumizi ya umeme wa gas ile tuliyokuwa tunaimbishwa uchumi wa gas kama wendawazimu yameishia wapi?
Hivi kichwa chako kina kamasi? Mara ngapi umeambiwa JK alishaikula hiyo gas na umeme wake utakuwa wa bei juu sana. Hii iwe mara ya mwisho kukueleza jambo hili
 
Hivi kichwa chako kina kamasi? Mara ngapi umeambiwa JK alishaikula hiyo gas na umeme wake utakuwa wa bei juu sana. Hii iwe mara ya mwisho kukueleza jambo hili
Amechukuliwa hatua gani, kulikuwa na Mahakama ya mafisadi mbona hatukuona yoyote huko? Je kama JK Kala ya gas na ameachwa, tuna uhakika gani mradi huu wa SG hatuliwi?
 
Amechukuliwa hatua gani, kulikuwa na Mahakama ya mafisadi mbona hatukuona yoyote huko? Je kama JK Kala ya gas na ameachwa, tuna uhakika gani mradi huu wa SG hatuliwi?
JK sheria inamlinda bwashee. JPM kuona hilo akautia pembeni ili waliotoa hela wamdai waliomhonga. Hata hili huoni kuwa JPM alifanya la maana?
 
JK sheria inamlinda bwashee. JPM kuona hilo akautia pembeni ili waliotoa hela wamdai waliomhonga. Hata hili huoni kuwa JPM alifanya la maana?

Uko sahihi sana, kwahiyo sheria inalinda mwizi? Na jiwe akitupiga itakuwa sawa tu maana sheria inamlinda? JK katupiga, kisha mkewe akapewa ubunge, na sasa mtoto na mke wako bungeni! Katika mazingira hayo unaamini vipi kwa sasa hatupigwi? Na uko hapa unatetea hayo!?
 
JPM hana ubavu wa kutuchapa kama JK. Huelewi aliyeanza kutuchapa katika madini alikuwa JK akiwa waziri wa Nishati na Madini. Prof Mwandosya akiwa Katibu Mkuu wake. Mikataba mibovu ya umeme JK, we acha tu! Ila kwa mbali JPM kamkomesha. Tuyaache tumchunge JPM asije akakengeuka. Ila nina imani JPM hawezi kuwa fisadi kiasi cha JK
 
Wewe ambae unauhakika na imani kuwa tunapigwa tunaomba uthibitisho na ushahidi.
 
So long hakuna janja janja ya kulipana capacity charges au mashariti mabovu kama ilivyokuwa kwa Dowans, Iptl na Richmond, hili ni jambo jema.
 
Kila nikisoma post zako humu JF huwa naona kama huwa umejeza matope kichwani. Habari za familian JK zinaingia vipi hapa?
 
Pasco hizo hesabu za megawati zinaweza kuwa kama zile za kilimo cha tikiti, unaweka milioni 5 unavuna milioni 15.

Hesabu za karatasi huwa ni tamu sana ila kwa graundi inaweza kuwa tofauti. Cha msingi tulia kunywa mtori, nyama zipo chini !
 
Nanusa harufu ya ufisadi, naanza kupata mashaka, renewable energy ndio iwe sababu ya kutetea deal kama hizi? Hakuna 10%? Mbona hata usa Hydroelectric ndio mkombozi wao! China na Brazili wanaongoza kwa kuzalisha HEP kwa nini kuhangaika na kununua umeme wakati tunasubiri Mw 2115? Hizi Mw 19 za nini?
 
Mkuu nisamehe kwa kuchelewa kukujibu majukumu mengi. Tukirudi kwenye swali lako ni kwamba kipindi cha nyuma ishu nyingi zilikuwa zinaanzishwa ili watu wapige pesa, mfano mzuri benki ya Standard Chartered HongKong imetumiwa Sana kutukopesha ili watu wapige pesa bila kujali huko mbele itakuwaje, na waliweka mikataba tata sana ambayo kuivunja ni ngumu. Sababu ya pili umeme wa gesi una limit. Gesi inaisha ardhini na ina mwisho wake kabisa. Kadiri unavyoitumia ndo inavyopungua ardhini. Ni Kama mtungi wa Kg45 jikoni kwako inavyopungua kadri unavyoitumia,sema huko ardhini ni Kama mtungi mkubwa sana, so ukiwekeza $bil.6.5 huna uhakika Kama zitarudi gesi haijaisha ardhini. Gesi ni natural reserve ambayo composition yake inachukua muda mrefu sana. Lakini Stigler Gorge inategemea maji kwa 95% au zaidi na ukifatilia umeme wa maji bado ni wa uhakika Sana tofauti na gesi. JPM ni mwanasayansi mzuri sana na anayajua haya yote na wameshayajadili, tatizo wengi humu wamekaa mkao wa kupinga lolote atakalofanya. Sijui Kama nimeeleweka vizuri mkuu.
 

Mtu anayenajisi uchaguzi anatoa wapi uadilifu?
 
Hii sio fact, hayo ni maoni yako.
Sote tunajua duniani kote umeme wa maji sio jambo la kudumu, kadri muda unavyokwenda na mabadiliko ya tabia nchi basi na nguvu ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji inapungua.

Upande wa pili, kuzalisha umeme kwa kutumia maji kuna kwenda sambamba na uharibifu ya ikologia ya viumbe hai.

Jambo moja kuu kuhusu umeme wa maji ni cheaper but limited. Gharama iko kwenye kuwekeza zaidi kuliko uendeshaji wake lakini hawezi kuzalisha zaidi ya kiwango cha juu kilichotegemewa.
 

Sina tatizo na maelezo yako mazuri, ila wakati tunaambiwa umeme wa gas ndio sahihi maana hiyo gas tutaitumia zaidi ya miaka 50, huyu anayetekeleza umeme wa maji alikuwa waziri kwenye serikali hiyo hiyo, mbona hakupinga? Wakati ule Utetezi wa umeme wa maji dhidi ya gas, tuliambiwa matatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Je baada ya utawala kubadili hayo mabadiliko ya tabia nchi yameboreka? Kama mtu aliweza kukalia kimya upotoshaji ule, unaweza kumuamini vipi sasa kwenye hili?

JPM ni mwanasayansi mzuri sana, je uanasayansi wake ulianza baada ya mkataba wa umeme wa gas? Mbona hakuyajadili hayo huko nyuma kwenye vikao vya gas? Sisi hatupingi lolote, bali hatukubali lolote bila maelezo ya kina, tumeshaumwa na nyoka. Hatuna imani na Magu wala chochote cha kwake, angekuwa mtu muadilifu angejitenga na huo wizi wa kwenye gas. Toka amaeingia madaraka hakuna uchaguzi wowote umefanyika kwa uadilifu, kama mtu anaweza kuchezea uchaguzi wa nchi, uadilifu anautoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…