Siasa za uwekezaji na uwezeshaji, tofauti na uhalisia wake

Siasa za uwekezaji na uwezeshaji, tofauti na uhalisia wake

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2017
Posts
610
Reaction score
749
Baada ya kuwa msomaji na mfuatailiaji na mchangiaji mzuri sana wa Jamii Forums kwa muda mrefu, ingawa uchangiaji wangu hapa JF umejikita katika mambo ya biashara, ujasiriamali na mengineyo machache, leo nimeona nitoe dukuduku langu kwa uchache kwenye siasa. Lakini mada yangu hii ya siasa itajikita katika siasa za uwekezaji, uwezeshaji na uhalisia wake kama kichwa cha mada kiashiriavyo.

Siasa ya uwekezaji imekuwa ikitumika sana kwa muda mrefu kwa aina mbali mbali tofauti kutokana na uwekezaji wanyewe umelenga nini na au unadhaniwa ulete tija ipi. Kuna uwekezaji wa kibiashara, kisiasa, kielimu na kadhalika lakini lengo kuu la uwekezaji ni mavuno yatayotokana na uwekezaji huo.

Hakuna uwekezaji usiolenga mwisho wa siku kuleta faida, au ya muda mfupi au ya muda mrefu. Lengo kuu la uwekezaji ni kuleta faida. Cha kutazamwa kwa umakini ni pale wanasiasa wanapotumia dhanna ya uwekezaji, huwa wamelenga kupata faida ipi katika uwekezaji huo wanouhubiri kwa wakati huo? Faida ya jamii au faida binafsi ya mwana siasa kisiasa?

Kuna uwekezaji wa kitaifa na kimataifa, wote lengo lake ni faida, faida ipi? Kwa manufaa ya nani au nini?

Upande mwengine tuna siasa ya uwezeshaji ambayo nayo inashika kasi kw muda mrefu kwa aina tofauti tofautiau misamiati tofauti tofati, cha kutazama na kufikiri, ni nini lengo la uwezeshaji? Hakuna kazi, iwe siasa, biashara, ajira isiyotakiwa kuwa na faida, cha kujiuliza ni hii dhana ya uwezeshaji, nayo inalenga kuwezesha au kumwezesha nani kwa faida ipi?

Wapenzi wa siasa tujadili hii mada kwa mtazamo chanya na pale tusipoelewa oni au maoni ya mchangijai mwenzetu tuulizane ili inoge.

Nakaribisha mjadala na pia na declare interest, mimi binafsi naitumia sana dhana ya uwekezaji na uwezeshaji lakini si kiasiasa bali kijasiriamali, biashara na kijamii kwa uchache. Lengo kuu ni faida. Faida zipi? Tuzichambue tuone kama faida za uwekezaji/uwezeshaji kibiashara Zinatofautiana na faida za dhana ya uwekezaji na uwezeshaji inayotumiwa na wanasiasa?

Karibuni.
 
Uwekezaji na uwezeshaji kwa CCM ni kwa watu jamii ya Polepole, Bashiru, Gwajima, Mwigulu na kadhalika ambao ni wabinafsi waongo na wanafiki wanaoona suala la umasikini na ujinga ni sifa ya kuwa mzalendo.

Uwekezaji na uwezeshaji kwa kutengeneza kikundi cha watu wachache wanaofaidika na rasilimali za nchi huku jamii kubwa ikizidi kuogelea kwenye lindi la ufukara na umasikini. Tanzania sasa hivi ili uweze kufurahia maisha kwenye nyanja zote inabidi uwe mwanaccm
 
Dhanna yako kwa hao uliowataja wa CCM ni kwa muono wako wa kisiasa au huo ni uhalisia wa wana siasa wengi wa Tanzania? Bila kujali chama?
 
Back
Top Bottom