Ifike mahala tuwe tunajadili mada kwa hoja kwa kina bila kutia ushabiki!!!
madai ya rwanda dhidi ya kukuthiri urasimu rushwa bandarini na barabarani ,idadi nyingi ya mizani kwa magari ya mizigo, si ya leo, na kwa kiasi kikubwa yana ukweli na yalitakiwa kutatuliwa na viongozi wetu, leo rwanda anaonekana mbaya kwa kupandisha kodi ,yes japokuwa kweli kunaonekana kuna element za visasi ,truth is we have been doing exactly the same to our neighbours.
Binafsi nimesafri kwa barabara karibu nchi zote kusini mwa Africa , ukweli ni kuwa Tanzania tunaongoza kwa sheria zisizotekelezeka , ngumu na zinazoleta usumbufu mkubwa sana hasa kwa wageni. chukulia mfano mizani ya barabarani ambayo kila nchi ni mandatory kupitia kwa malori. Dar mpaka Tunduma , distance ya kilometa 930, kuna mizani minane(8) achilia mbali mizani ya mkeka ambayo inaweza zuka mahali popote, Nakonde(Zambia) to Livingstone almost 1600 km kuna mizani minne(4), Police check point ziko sehemu Rasmi, kuanzia Nakonde hadi livingstone si zaidi ya kumi na Trafiki police ni miongoni mwa askari unaotegemea kuwakuta kwenye checkpoint hizo, huku kwetu kipande kifupi tu cha Mbeya Tunduma kina vituo vya trafiki zaidi ya ishirini , achilia mbali TRA na majembe, fire officers , wenzetu watu wa revenue ni nadra sana kuwakuta barabarani.
Truck operators wengi kutoka nchi za sadc Namibia botswana South Africa hawaitumii Bandari ya dar wakisight matatizo kama hayo waliyoainisha Rwanda, sina uhakika kama na wao waliwahi kuilalamikia, ila chances are waliamua kutuacha na sheria zetu ,wao wakatafuta route mbadala nchi jirani, hasa mozambique, Ukifika Tunduma utaona malori ya south afirica botswana yana offload mizigo yao na kupakia kwenye malori ya Tanzania .
Tujiulize kama Rwanda wameamua kutoza dola 500 kutoka 152 kwa lori la kitanzania, je sisi TRA inachaji kiasi gani kwa lori la Rwanda ? chances are that pengine ni kubwa kuliko hizo ndo maana haiwekwi hadharani , leo Rwanda anajitoa kesho atakuwa na nani kama si Zambia na Malawi, na je kama Bandari ya Mombasa ikifanikiwa kuteka wateja wetu wakubwa hatuoni kuwa Bandari ya Beira Mozambique ikikamilika nayo inaweza kuteka wateja wetu waliobakia Hasa wazambia, ikizingatiwa kuwa Tazama pipeline iliyokuwa ina waatach kuitumia Dar port inaingia matengenezo makubwa yatakayodumu kwa miaka kadhaa , hivyo hakutakuwa na ulazima wa wao kushushia mafuta Dar .
Itakuwa ni busara kwa mawaziiri husika Fedha, ujenzi, mambo ya ndani kukaa chini na wasome alama za nyakati ikiwezekana watembee kwa barabara wajifunze wataona mapungufu makubwa kitendaji baina ya majirani zetu, ili baadaye tuweze kuweka international fair standards.vinginevyo huko mbele ya safari watanzania tunawezajikuta hakuna biashara tunaweza kufanya na nchi jirani zetu