Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Hata tukishabikia kama mwenye akipuuzia kuna shida gani? au ndio hivyo mnavyo sema kwamba hana muda wa kujishauri kama sio kutafakari, eti?
 
Wakuu! Hebu tujuzeni na magari ya mizigo yatokayo Rwanda kuja TZ yanatozwa kiasi gani cha kodi?
 
Kuwa na akili tmam ww, huyo ndg yako alishauriwa, ha2mshambulii wala haogopeki km ww unavo dhani. Mm nngekushaur muulize , alizaliwa nyumbani au hospital. ndo 2tajua 2anzie wpi kum-psychotherapy,
 
Huu mgogoro naona kama vile ni ugomvi wa kitoto, nasema hivyo kwa sababu watoto wakikoseana hulipiza kwa stahili hii inayofanywa na Rwanda na Tanzania. Ushauri mwepesi tu, "suluhu itafutwe kwa fulani kuongea na anaeonekana ni chanzo cha mgogoro Congo" yakaanza maneno kibao ya kejeli, mwingne akarespond kwa timuatimua, leo hii mwingne kaibuka vikwazo vya kiuchumi kwa kupandisha kodi!!! Bila kuwaza kuwa nae anawatisha wananchi wake mzigo, this is nonsense, and type of these leaders are burden to their citizens. Simlaumu mkenya hata kidogo maana "vita vya panzi ni furaha ya kunguru" nyie piganeni yeye atafaidi na kusonga....mtapoteza muda na resources ktk malumbano na propaganda, huku mwenzenu anawekeza kwenye propaganda zenu.

I want to tell you leaders, madaraka mliyo nayo mmepewa kwa hisani ya wananchi, hata kama mliingia kwa mtutu wa bunduki hapo awali but uwepo wenu madarakani ni hisani ya wananchi. And whatever kind of hardship and suffering you made to any one will also be upon you right here on the earth.

Pia, kama mtu akikosea,au mpubavu akikurapia na nawe ukamkaripia utaonekana -------- zaidi!!! SASA NA TUJIHOJI -------- NI NANI? Yatupasa kama ndugu kukaa kwa umoja na kupatana vema.

NB: NONE OF THE RACE/TRIBE BORN TO BE LEADERS OVER OTHERS FOREVER!!!

Serikali ya Rwanda imeongeza ushuru wa
barabara (ROAD TOLL) kwa magari yote ya
Mizigo (Fuel and Dry Cargo) yenye plate
numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka
USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi, kwa siku magari
ya mizigo takribani 300 yanavuka Rusumo
ambapo ni mpakani mwa Tanzania na Rwanda
na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo yana
plate number za Tanzania.
Wamiliki wa Malori wameiomba serikali kuingilia
kati ili kunusuru hali hiyo.
 
Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums[Tuache kujidharau.. Rwanda si size yetu... Ifike sehemu tuache kuchekacheka.. Tuwe wakali na wenye kiburi.. Mwl JKN asingecheka na kagame... Tusipigane ila tumwonyeshe yeye na washirika wake kuwa tunaweza... Na akiendelea kunyosha shingo vijana wetu walioko Goma tutawambia waje kwa mguu magari watayakuta Rusumo yakuwarudishe makambini kwao...
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

ID yako na hiki ulichopost vinashabihiana
 
Umenena vyema! Watakaoumia na Wanyarwanda!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

kama tunavoumia sisi kwa kutoza toll kubwa magari ya Kenya yanayoingia Tanzania au siyo? Mkuki kwa nguruwe. Unafiki wetu hadharani.
 
Hivi ule mkutano wa Smart Partnership Rwanda haikualikwa nini? Can't see even bogus partnership.
 
Ifike mahala tuwe tunajadili mada kwa hoja kwa kina bila kutia ushabiki!!!

madai ya rwanda dhidi ya kukuthiri urasimu rushwa bandarini na barabarani ,idadi nyingi ya mizani kwa magari ya mizigo, si ya leo, na kwa kiasi kikubwa yana ukweli na yalitakiwa kutatuliwa na viongozi wetu, leo rwanda anaonekana mbaya kwa kupandisha kodi ,yes japokuwa kweli kunaonekana kuna element za visasi ,truth is we have been doing exactly the same to our neighbours.
Binafsi nimesafri kwa barabara karibu nchi zote kusini mwa Africa , ukweli ni kuwa Tanzania tunaongoza kwa sheria zisizotekelezeka , ngumu na zinazoleta usumbufu mkubwa sana hasa kwa wageni. chukulia mfano mizani ya barabarani ambayo kila nchi ni mandatory kupitia kwa malori. Dar mpaka Tunduma , distance ya kilometa 930, kuna mizani minane(8) achilia mbali mizani ya mkeka ambayo inaweza zuka mahali popote, Nakonde(Zambia) to Livingstone almost 1600 km kuna mizani minne(4), Police check point ziko sehemu Rasmi, kuanzia Nakonde hadi livingstone si zaidi ya kumi na Trafiki police ni miongoni mwa askari unaotegemea kuwakuta kwenye checkpoint hizo, huku kwetu kipande kifupi tu cha Mbeya Tunduma kina vituo vya trafiki zaidi ya ishirini , achilia mbali TRA na majembe, fire officers , wenzetu watu wa revenue ni nadra sana kuwakuta barabarani.

Truck operators wengi kutoka nchi za sadc Namibia botswana South Africa hawaitumii Bandari ya dar wakisight matatizo kama hayo waliyoainisha Rwanda, sina uhakika kama na wao waliwahi kuilalamikia, ila chances are waliamua kutuacha na sheria zetu ,wao wakatafuta route mbadala nchi jirani, hasa mozambique, Ukifika Tunduma utaona malori ya south afirica botswana yana offload mizigo yao na kupakia kwenye malori ya Tanzania .

Tujiulize kama Rwanda wameamua kutoza dola 500 kutoka 152 kwa lori la kitanzania, je sisi TRA inachaji kiasi gani kwa lori la Rwanda ? chances are that pengine ni kubwa kuliko hizo ndo maana haiwekwi hadharani , leo Rwanda anajitoa kesho atakuwa na nani kama si Zambia na Malawi, na je kama Bandari ya Mombasa ikifanikiwa kuteka wateja wetu wakubwa hatuoni kuwa Bandari ya Beira Mozambique ikikamilika nayo inaweza kuteka wateja wetu waliobakia Hasa wazambia, ikizingatiwa kuwa Tazama pipeline iliyokuwa ina waatach kuitumia Dar port inaingia matengenezo makubwa yatakayodumu kwa miaka kadhaa , hivyo hakutakuwa na ulazima wa wao kushushia mafuta Dar .

Itakuwa ni busara kwa mawaziiri husika Fedha, ujenzi, mambo ya ndani kukaa chini na wasome alama za nyakati ikiwezekana watembee kwa barabara wajifunze wataona mapungufu makubwa kitendaji baina ya majirani zetu, ili baadaye tuweze kuweka international fair standards.vinginevyo huko mbele ya safari watanzania tunawezajikuta hakuna biashara tunaweza kufanya na nchi jirani zetu
 
Mara nyingi kufanya jambo kwaajili ya kumkomoa mwingine huwa lina hasara zaidi kuliko faida. Mbinu za Rwanda kutaka wafanyabiashara na raia wa Rwanda wasitumie bandari za Tanzania badala yake watumie bandari ya Mombasa kwa kiwango Fulani itawaumiza wafanyabiashara wa Tanzania lakini itawaumiza zaidi Wanyarwanda.

Kumbuka kuna Wanyarwanda wanaingiza magari yao kupitia Dar, na wanayaendesha barabarani mpaka nchini kwako, sasa watalazimika kuendesha umbali mkubwa zaidi, wakitumia mafuta mengi zaidi, siku nyingi zaidi, na hatari za kusafiri umbali mrefu zaidi.

Serikali ya Tanzania ili kufidia pengo litakalotokana na upungufu wa mizigo ya Rwanda na Uganda inabidi iboreshe haraka huduma za bandari na reli, na kuweka vivutio zaidi kwa wasafirishaji mizigo ya Burundi, Congo, Malawi na Zambia. Kama gharama za usafirishaji mizigo kupeleka mizigo Congo zitakuwa ndogo sana, Wanyarwanda watagundua kosa walilofanya. mambo kama haya usiyatazame wakati wote kuwa ni matatizo bali uone ni opportunity, unakumbushwa kufanya kitu kwenye nchi yako, namaanisha serikali.

Kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya Mombasa badala ya Dar es Salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia Mombasa mambo yatatulia.

Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.
 
sipati picha ingekuwaje kama kagame angekuwa rais wa taifa kubwa kama tz.
Na sielewi kwa nini Tanzania tunamdekeza kiasi cha kuomba suluhu nae.inachefua sana.
 
Naunga mkono maelezo yako kwa 100%. Tanzania tuna sharia za kipuuzi, tuna mbinu za kipuuzi, tuna usimamizi wa kipuuzi. Karibu kila sharia, wasimamizi wake wanafanya kwa nia ya kumkomoa mtu. Wewe umeelezea kuhusu vituo vya mizani na vituo visivyo na hesabu vya ukaguzi wa polisi. Traffic polisi wetu, mkewe akimwambia hana mboga, anavaa uniform na kwenda kusimama barabarani, popote pale na kuanza kusimamisha magari ovyo, na kuuliza maswali yasiyo na vichwa wala miguu. Akiona hutaki kumpa chochote, anaweza kukuacha na kuanza kuwauliza madereva wengine. Na njia nzima wamejaa askari wa namna hiyo, fikiria muda unaoupoteza njiani.

Usumbufu huo wa polisi ni juu ya ule unaosababishwa na matuta yasiyo na hesabu yaliyopo barabarani kila kijiji. Uliwahi kuona wapi highway inakuwa na matuta? Ni Tanzania tu! Rais Kikwete aliwahi kusema kuwa aliwahi kulalamikiwa na marais wa SADC kuhusiana na matuta lakini kama kawaida yake aliongea huku anacheka, na sikuona kama alikuwa ametoa maelekezo yoyote kama mkuu wa nchi. Mlevi akigongwa, kesho linawekwa tuta alipogongewa, mototo akigongwa kwa sababu wazazi wamemwacha kama kuku wa kienyeji, kesho linawekwa tuta. Hivi tutaweza kumwekea tuta kila mtu ili asigongwe na gari? Wenzetu nchi nyingine, utaona madaraja mepesi yamewekwa (siyo kama la Manzese) kwenye vivuko vya waenda kwa miguu au taa maalum zenye sauti kwaajili ya kuvuka waenda kwa miguu, siyo huu upuuzi wa matuta wa Tanzania.

Ifike mahala tuwe tunajadili mada kwa hoja kwa kina bila kutia ushabiki!!!

madai ya rwanda dhidi ya kukuthiri urasimu rushwa bandarini na barabarani ,idadi nyingi ya mizani kwa magari ya mizigo, si ya leo, na kwa kiasi kikubwa yana ukweli na yalitakiwa kutatuliwa na viongozi wetu, leo rwanda anaonekana mbaya kwa kupandisha kodi ,yes japokuwa kweli kunaonekana kuna element za visasi ,truth is we have been doing exactly the same to our neighbours.
Binafsi nimesafri kwa barabara karibu nchi zote kusini mwa Africa , ukweli ni kuwa Tanzania tunaongoza kwa sheria zisizotekelezeka , ngumu na zinazoleta usumbufu mkubwa sana hasa kwa wageni. chukulia mfano mizani ya barabarani ambayo kila nchi ni mandatory kupitia kwa malori. Dar mpaka Tunduma , distance ya kilometa 930, kuna mizani minane(8) achilia mbali mizani ya mkeka ambayo inaweza zuka mahali popote, Nakonde(Zambia) to Livingstone almost 1600 km kuna mizani minne(4), Police check point ziko sehemu Rasmi, kuanzia Nakonde hadi livingstone si zaidi ya kumi na Trafiki police ni miongoni mwa askari unaotegemea kuwakuta kwenye checkpoint hizo, huku kwetu kipande kifupi tu cha Mbeya Tunduma kina vituo vya trafiki zaidi ya ishirini , achilia mbali TRA na majembe, fire officers , wenzetu watu wa revenue ni nadra sana kuwakuta barabarani.

Truck operators wengi kutoka nchi za sadc Namibia botswana South Africa hawaitumii Bandari ya dar wakisight matatizo kama hayo waliyoainisha Rwanda, sina uhakika kama na wao waliwahi kuilalamikia, ila chances are waliamua kutuacha na sheria zetu ,wao wakatafuta route mbadala nchi jirani, hasa mozambique, Ukifika Tunduma utaona malori ya south afirica botswana yana offload mizigo yao na kupakia kwenye malori ya Tanzania .

Tujiulize kama Rwanda wameamua kutoza dola 500 kutoka 152 kwa lori la kitanzania, je sisi TRA inachaji kiasi gani kwa lori la Rwanda ? chances are that pengine ni kubwa kuliko hizo ndo maana haiwekwi hadharani , leo Rwanda anajitoa kesho atakuwa na nani kama si Zambia na Malawi, na je kama Bandari ya Mombasa ikifanikiwa kuteka wateja wetu wakubwa hatuoni kuwa Bandari ya Beira Mozambique ikikamilika nayo inaweza kuteka wateja wetu waliobakia Hasa wazambia, ikizingatiwa kuwa Tazama pipeline iliyokuwa ina waatach kuitumia Dar port inaingia matengenezo makubwa yatakayodumu kwa miaka kadhaa , hivyo hakutakuwa na ulazima wa wao kushushia mafuta Dar .

Itakuwa ni busara kwa mawaziiri husika Fedha, ujenzi, mambo ya ndani kukaa chini na wasome alama za nyakati ikiwezekana watembee kwa barabara wajifunze wataona mapungufu makubwa kitendaji baina ya majirani zetu, ili baadaye tuweze kuweka international fair standards.vinginevyo huko mbele ya safari watanzania tunawezajikuta hakuna biashara tunaweza kufanya na nchi jirani zetu
 
Afadhali wambie Kamanda, unajua Watanzania ni kama tumelogwa. Tunashabikia mambo bila kufikiria, watakao umia ni haohao wanaomiliki biashara za malori. Na hii maana ya haraka haraka ni kuanza ku discourage mizigokushushiwa Dar sasa watalazimika kwenda Bandari ya Mombasa.

Mambo mengine adghabu zake ni hapa hapa tu hakuna kungojea,

TAFAKARI
Wakati mwingine ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti,sisi kama Tanzania tuna haki ya kutoa maoni yeyote na pia tuna haki ya kusimamia kauli zetu kwa gharama yeyote la sivyo tutaendeshwa na next time watatuchukulia kuwa sisi ni big 4 nothing ,hii ni cold war na hakuna vita without casualties na hizo wafanyavyo rwanda ni casualties na wanyewe wanazipata kwa kuwatesa raia wao
 
Mkuu, ukimputupia mwenye mzigo naye atatafuta sehemu yenye nafuu kwenye usafirishaji ili bidhaa yake iwe na ushindani sokoni. Maana yake ni kwamba bidhaa hiyo hiyo ikipita Mombasa itakuwa bei nafuu kuliko Dar kwa ajili ya usafirishaji tu. Mwisho wa siku kila mwenye mzigo atapitisha Mombasa - na hilo ndio lengo.
That is the whole idea but then i dont think they thought of it thoroughly on this reinforcement tactic. The facts still remain the same there is a big gap in distance from Mombasa to Kigali compared to Dar es salaam to the same destination.

Meaning the haulage has to consider fuel cost again which will be added to the customer and the business has to consider time, there have to be more participants in the transportation of their goods if they are to receive enough volume compared to dar due to distance differences.

In short this is bad tactic, until they finish the railway planned from Mombasa to Kigali that is when they will see the fruits of using the Mombasa port; even that will have negative effects for Kigali transporters since they produce nothing to export outside only the government will gain in transportation revenue not the people if not reducing the industry to almost none existence.

By that time prices will have shoot in the market and we don't know if businesses will be willing to lower them in short let the megalomaniac Kagame be responsible for his own demise.
 
Hili tatizo ni dogo sana; ningekuwa na madaraka ningelitolea uamuzi wakati nakunywa chai ya asubuhi kabla hata sijaingia ofisini kwa kuweka policy yenye step nne tu.
STEP1: Ningetoa tamko la kiserikali kuwa mzigo hiyo itarudishwa bandarini Dar kwa gharama za serikali ya Tanzania iwapo haitapokelewa na Rwanda kulingana na taratibu zilizopo katika muda wa siku mbili tangu roili kufika mpakani.
STEP2: Baada ya step 1 hapo juu, nitatoa amri kwa maroli yote yenye namba za Tanzania yarudishe mizigo yao bandarini Dar, serikali itawalipa gharama zao za halali ili kuhakikisha biashara zeo haziathiriki na upuuzi huu.
STEP3: Mizigo ikishafika Dar itarudishwa katika mamlaka ya bandari ambapo bandari iatarudisha malipo yote ya clearing serikalini.
STEP4: Gari litakolochukua mizigo hiyo liliilipe serikali fidia kwa gharama za step 2 na vile vile liilipe tena bandari gharama za step 3 halafu pia lilipe road toll ya $500; Marekani wanita kitu hii kuwa ni reciprocity policy: kwetu inaitwa jino kwa jino.

Mwisho wa yote atakayeumia ni mnyawaranda aliyekuwa akitegema mizigo hiyo; very simple. You can't just change rules in the middle of the game.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom