Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Rwanda iiwekee vikwazo Tanzania??? Ni sawa na syria kuiwekea vikwazo marekani.
Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums[Tuache kujidharau.. Rwanda si size yetu... Ifike sehemu tuache kuchekacheka.. Tuwe wakali na wenye kiburi.. Mwl JKN asingecheka na kagame... Tusipigane ila tumwonyeshe yeye na washirika wake kuwa tunaweza... Na akiendelea kunyosha shingo vijana wetu walioko Goma tutawambia waje kwa mguu magari watayakuta Rusumo yakuwarudishe makambini kwao...
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.
Umenena vyema! Watakaoumia na Wanyarwanda!
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Mkuu hayakualikwa kwa sababu ya ukabila wao na mauaji sanjari na kukosekana kwa haki za binadamu.Hivi ule mkutano wa Smart Partnership Rwanda haikualikwa nini? Can't see even bogus partnership.
Kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya Mombasa badala ya Dar es Salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia Mombasa mambo yatatulia.
Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.
Ifike mahala tuwe tunajadili mada kwa hoja kwa kina bila kutia ushabiki!!!
madai ya rwanda dhidi ya kukuthiri urasimu rushwa bandarini na barabarani ,idadi nyingi ya mizani kwa magari ya mizigo, si ya leo, na kwa kiasi kikubwa yana ukweli na yalitakiwa kutatuliwa na viongozi wetu, leo rwanda anaonekana mbaya kwa kupandisha kodi ,yes japokuwa kweli kunaonekana kuna element za visasi ,truth is we have been doing exactly the same to our neighbours.
Binafsi nimesafri kwa barabara karibu nchi zote kusini mwa Africa , ukweli ni kuwa Tanzania tunaongoza kwa sheria zisizotekelezeka , ngumu na zinazoleta usumbufu mkubwa sana hasa kwa wageni. chukulia mfano mizani ya barabarani ambayo kila nchi ni mandatory kupitia kwa malori. Dar mpaka Tunduma , distance ya kilometa 930, kuna mizani minane(8) achilia mbali mizani ya mkeka ambayo inaweza zuka mahali popote, Nakonde(Zambia) to Livingstone almost 1600 km kuna mizani minne(4), Police check point ziko sehemu Rasmi, kuanzia Nakonde hadi livingstone si zaidi ya kumi na Trafiki police ni miongoni mwa askari unaotegemea kuwakuta kwenye checkpoint hizo, huku kwetu kipande kifupi tu cha Mbeya Tunduma kina vituo vya trafiki zaidi ya ishirini , achilia mbali TRA na majembe, fire officers , wenzetu watu wa revenue ni nadra sana kuwakuta barabarani.
Truck operators wengi kutoka nchi za sadc Namibia botswana South Africa hawaitumii Bandari ya dar wakisight matatizo kama hayo waliyoainisha Rwanda, sina uhakika kama na wao waliwahi kuilalamikia, ila chances are waliamua kutuacha na sheria zetu ,wao wakatafuta route mbadala nchi jirani, hasa mozambique, Ukifika Tunduma utaona malori ya south afirica botswana yana offload mizigo yao na kupakia kwenye malori ya Tanzania .
Tujiulize kama Rwanda wameamua kutoza dola 500 kutoka 152 kwa lori la kitanzania, je sisi TRA inachaji kiasi gani kwa lori la Rwanda ? chances are that pengine ni kubwa kuliko hizo ndo maana haiwekwi hadharani , leo Rwanda anajitoa kesho atakuwa na nani kama si Zambia na Malawi, na je kama Bandari ya Mombasa ikifanikiwa kuteka wateja wetu wakubwa hatuoni kuwa Bandari ya Beira Mozambique ikikamilika nayo inaweza kuteka wateja wetu waliobakia Hasa wazambia, ikizingatiwa kuwa Tazama pipeline iliyokuwa ina waatach kuitumia Dar port inaingia matengenezo makubwa yatakayodumu kwa miaka kadhaa , hivyo hakutakuwa na ulazima wa wao kushushia mafuta Dar .
Itakuwa ni busara kwa mawaziiri husika Fedha, ujenzi, mambo ya ndani kukaa chini na wasome alama za nyakati ikiwezekana watembee kwa barabara wajifunze wataona mapungufu makubwa kitendaji baina ya majirani zetu, ili baadaye tuweze kuweka international fair standards.vinginevyo huko mbele ya safari watanzania tunawezajikuta hakuna biashara tunaweza kufanya na nchi jirani zetu
Wakati mwingine ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti,sisi kama Tanzania tuna haki ya kutoa maoni yeyote na pia tuna haki ya kusimamia kauli zetu kwa gharama yeyote la sivyo tutaendeshwa na next time watatuchukulia kuwa sisi ni big 4 nothing ,hii ni cold war na hakuna vita without casualties na hizo wafanyavyo rwanda ni casualties na wanyewe wanazipata kwa kuwatesa raia waoAfadhali wambie Kamanda, unajua Watanzania ni kama tumelogwa. Tunashabikia mambo bila kufikiria, watakao umia ni haohao wanaomiliki biashara za malori. Na hii maana ya haraka haraka ni kuanza ku discourage mizigokushushiwa Dar sasa watalazimika kwenda Bandari ya Mombasa.
Mambo mengine adghabu zake ni hapa hapa tu hakuna kungojea,
TAFAKARI
That is the whole idea but then i dont think they thought of it thoroughly on this reinforcement tactic. The facts still remain the same there is a big gap in distance from Mombasa to Kigali compared to Dar es salaam to the same destination.Mkuu, ukimputupia mwenye mzigo naye atatafuta sehemu yenye nafuu kwenye usafirishaji ili bidhaa yake iwe na ushindani sokoni. Maana yake ni kwamba bidhaa hiyo hiyo ikipita Mombasa itakuwa bei nafuu kuliko Dar kwa ajili ya usafirishaji tu. Mwisho wa siku kila mwenye mzigo atapitisha Mombasa - na hilo ndio lengo.