Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.

Wakishaongea na wizara husika ifanye nini?? Ili iweje???? Serikali ya Rwanda inaweweseka tu. Wanakomoa wanajisahau kama na wao pia watu wao wengi wanafanya biashara huku na sisi tukianza kufanya kama wao ni wananchi wa pande zote wataumia.
 

mkuu mizigo inayopitia bandari ya Dar kwenda Rwanda ni asilimia ndogo sana. Bandari yetu haitegemei kabisa mizigo ya Rwanda
Ni gharama kubwa sana kupitishia mizigo ya Rwanda kwa bandari ya Mombasa hasa ukiangalia distance. Sisi tukomae waache wajiongezee gharama kubwa za maisha maana wezi hao walikua wanaiba madini ya Kongo kupitia M 23 sasa M23 tunawapa adabu ya maana na tuone sasa wapi watakapotoa madini.
Cha muhimu hapo serikali ni kuimarisha bandari zetu pamoja na miundo mbinu ya barabara na reli bado tuna client wengi sana hasa Kongo, Burundi, zambia na Malawi
Ikiwezekana na sisi kuanzia sasa tutangaze marufuku kwa mizigo ya Rwanda kukanyaga ardhi ya Tanzania
 
Kwakweli we kichuguu ni kiboko ninakubaliana na wewe naomba umtumie mwakyembe ujumbe huo tumalize tofauti na ubabe wa huyo pk
 
Rwanda ushuru juu, Uganda umeme miezi kumi, tehe tehe tunatafunana wenyewe kwa wenyewe sasa kwasababu ya bifu la JK na PK, ndege mjanja?
 
Burundi itanufaika sana hapa!!Tu trade na burundi kwa rate ndogo sana ili wafuate bidhaa burundi!
 
Bila shaka serikali ya Rwanda imepania kudhoofisha uhusiano wake na Tanzania kwani sasa imeamua kuendeleza rafu zake dhidi ya serikali ya Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la Habarileo la siku ya leo tarehe 02/09/2013,serikali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania pekee kwa kupandisha ushuru wa barabara kutoka dola 152 mpaka dola 500.Hii maana yake ni kuhujumu bandari ya Dar-es-salaam.Tozo hiyo inaanzia Rusoma kuelekea Kigali.

Kwa mazingira haya kuna haja gani ya kuwa na uhusiano na nchi kama hii?!!.Mpaka sasa Rwanda imeshafanya hujuma nyingi tu na sisi kuwa wavumilivu tafsiri yake sasa ni unyonge na kujipendekeza!Dhamira ya utawala wa Kagame no kuvunja uhusiano na Tanzania na anacho kifanya sasa ni kutafuta sababu tu.Hivyo basi ni bora kuvunja uhusiano kuliko huu unyonge.
 
nahisi kagame asamehewe! maana nnaona hajui ni kitu gani anafanya! kujiamini sana kunamponza hata kufanya maamuzi yasiyokuwa na msimgi!
 

Ingawa ni lugha ya kigeni kwa kweli nimekuelewa sana
 
landlocked country inawawekea kikwazo nchi yenye access na bahari. siku kenya kukinuka, rwanda watakula nnya.watakosa pa kupitishia mizigo yao.
 
atacompansate na mapato ya madin kutoka drc anaakili ya hesabu kuliko yako, unadhani kwanini hakuna nyumba za nyasi kule tafuta majibu.

ndio maana tumeingia goma na sie tukachote madini wakati yeye tall na m23 wake tumewatimua rwanda...pia hata dar haina nyumba ya nyasi..rwanda ni ndogo kuliko dar na mkoa wa pwani....majibu umeyapata. Eneo la tanzania ni ni zaidi ya mara 25 ya eneo la hiyo wilaya yako ya rwanda...think big

jwtz is a game changer in goma and rwanda economy in general..ahahaaaaaaaa..pole tutsi and r.i.p tall

kama ulishawahi kucheza draft..sie tuna king mbili rwanda and kete nne...waulize wataalamu watakuambia...game limekwisha. Nyodo zooote zitakwisha tukiikamata goma na kuingia kigali....

Hapo bado hatujaonyesha ni kikundi gani cha waasi tukipe support kimwanzishie mbungi ajiulize atapigana na waasi au atasupport m23 au ataendelea kuichokonoa tanzania au tumwongezee wakimbizi aangaike wapi pa kuwalaza na nini cha kuwalisha..coz tunao hapa kwetu kama laki 8-1m.

Balali acha woga..tutamchapa nje ndani na bado hata kitandani tunamgalagaza mbayaaaaa.
 
Hii taarifa kama ya kweli ebu tuingalieni kwa makini maana neno ningeua huja baada ya safari
 
Hii taarifa kama ni ya kweli ebu tuiangalieni kwa makini sana, maana "Neno ningejua huja baada ya safari"
 
kagame bwana...in simple economic theory..nchi ndogo inapofanya protectionism dhidi ya nchi kubwa(kwa eneo na uchumi) inayoumia ni nchi ndogo na raia wake na ile nchi kubwa haitodhurika.....ni sawa tanzania iongeze import duty kutoka USA..hasara ni kwa tanzania..kagame umeumia..uchumi wako unakua kwa kasi lakini bado ni mdogo kulinganisha na wa tanzania
 
watakaomia ni wanyaruwanda wenyewe,mimi nilijua anaakili huyu Kagame kumbe Bure kabisa, na huu ni mwisho wake, M23 wameondolewa na jw hivyo na anakurupuka na kutoa maamuzi ya kijinga yanayowacost raia wake,
 
Mkuu,

Mambo ya usalama wa taifa mimi sina ujuzi nayo kabisa. Hayo ni mambo yanayofanyika kwa siri kubwa, wanaoyafahamu vizuri ni wale ambao shughuli zao zina uhusiano na idara hiyo.

Safi sana kwa kuwa honest,yana wenyewe hayo!
 
sasa hapo wewe unaona kamaomoa nani?,mizigo inatoka Dar Port kwenda Rwanda,charges zilizoongezeka zinaongeza bei ya bidhaa husika,saa nanai mlaji wa hizo bidhaa?

Hujaelewa!Ni kwamba kama amepandisha charges kwa magari kutoka TZ,na yale yanayotoka nchi nyinginezo charges ziko palepale bac hii inamaanisha bidhaa kutoka TZ zitakuwa hazinunuliki na hivyo biashara Kati ya hizi nchi mbili itapungua kama sio kufa kabisa!Sidhani kama PK angefikia maamuzi hayo kama angejua wananchi wake watadhurika!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…