Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
Mbona zipo option nyingi. Malori yanaweza kushushia mzigo hapo mpakani wakachukua kwa lori za Rwanda bila kulipia extra road toll.

All in all gharama za biashara zinaongezeka kwa wanyarwanda zaidi kuliko kwa watanzania.

Mzigo ukishukia Tanzania maana yake sio "on transit" tena na inabidi TRA wachukue chao! ndio sheria inavyotaka
 
au ndio keshawajua huku wengi tukiwa tumelala bado?

Mkuu kuna kipindi habari zilivuma sana hata kabla ya hili sakata la JK/PK kuwa kuwa mheshimiwa kaingiza vichwa vya Scania 50 hajalipa hata senti tano ya ushuru. Sasa hapo kuna reli tena?
 
Mkuu, mkiona Kagame anapiga kelele ni amejaribu sana kuwa accomodating ila kuna mahali inafika mtu unashindwa kuvumilia. Tanzania inabidi mjirekebishe katika karne hii ya utandawazi na ushindani.

Tutamrekebisha Kagame instead kwani muda mfupi ujao tutakuwa Kigali kuwapatieni rais mwenye akili nzuri. Huyo militant ni matatizo tu hata kwa raia wake mwenyewe.
 
huyu anajichongea tu kwa watu anaowaongoza haoni kwamba maisha yatapanda na mwisho wa siku ataonekana chizi yeye tu!siku zote mtu anayekosana na Tanzania ujue yeye ndo ana chokochoko!tutaona mengi lakini no war.
 
Kwani wenye magari watakuwa wapumbavu kiasi hiko na wao ongezeko la gharama si wanawatupia wenye mizigo, hawataki mizigo inadoda bandarini na gharama za kuifadhi juu; mpaka inabaki kuwa mali ya serikali ya Tanzania.

Hapa serikali irudishe compliments tu na magari yatakayo toka Rwanda yapate same treatment for now at least we should gain whilst they are still reinforcing their strategy of diverting their cargo to Mombasa.

Mkuu, ukimputupia mwenye mzigo naye atatafuta sehemu yenye nafuu kwenye usafirishaji ili bidhaa yake iwe na ushindani sokoni. Maana yake ni kwamba bidhaa hiyo hiyo ikipita Mombasa itakuwa bei nafuu kuliko Dar kwa ajili ya usafirishaji tu. Mwisho wa siku kila mwenye mzigo atapitisha Mombasa - na hilo ndio lengo.
 
I agree ni mkakati wa kuimarisha Mombasa Port. Nafikiri Tanzania inalazimishwa kujipanga,labda akili na uzalendo vitaturudia!!
 
Hii vita itatughalimu tu baadaye, mizigo ya Rwanda itapungua saana au haitapita tena muda si mrefu , halafu kazi zitafutwa kule C&FAs , GVT revenue itapungua vilevile, baada ya hapo Burundi inaweza kujiunga na Rwanda , kesho Eastern Congo safari imekolea hiyo, uchumi wetu bado unahitaji fedha za jirani zetu jamani tusidanganyane.
 
Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

Mimi nnadhani madhara ya kiuchumi yatatokea kwa upande wanTanzania,japo kwa kiwango fulani.Nnapata ukakasi kidogo kuchangia kwa ukamilifu kwa sababu hatujui gharama sahihi za kushusha/kupitishia mizigo ktk bandari ya Mombasa nchini Kenya vile vile kwa hapa kwetu Tanzania .

Ila kwa juu juu ni kuwa mfanyabiashara siku zote anahitaji unafuu katika biashara zake ili kupata faida na pia kuuza mali zake kwa wepesi hasa kutokana na bei.Kwa mfano wapo wanaosema wananchi wa Rwanda ndio watatishwa mzigo huu ulioongezwa na hilo nnakubaliana nalo ila tuchukulie mimi ni mfanyabiashara wa Rwanda nimeshusha mifuko ya saruji kupitia Tanzania na mfanyabiashara mwenzangu nae ameshusha hiyo hiyo mifuko ya saruji na yeye akatumia bandari ya Mombasa nchini Kenya.Swali la kujiuliza hapa ni hivi kama gharama za kushusha mzigo kupitia Mombasa zitakuwa ni za chini zaidi ya za Tanzania ni mfanyabiashara yupi atakubali kupitishia mzigo ktk bandari ya Tanzania.

Tukumbuke wafanyabiashara wanahitaji unafuu katika kazi zao ili waweze kwenda kushindana na soko huko wanapopeleka mizigo yao..

Nnawaomba wenzangu ktk jukwaa hili muache kuishambulia Rwanda na raisi wao,ile ni nchi na ina mamlaka zake tusiwaingilie ktk maamuzi yao hata kama watasema hakuna kuingiza magari yanayotoka Tanzania.Tujadili athari za kiuchumi kama mtoa mada alivyowasilisha,pia tungeomba wenye upeo zaidi katika taaluma ya uchumi waje huku watusaidie,lakini kuwashambulia kina Kagame na nchi yake haitotusaidia chochote.
 
this is an opportunity kwa wafanyabiashara kujizolea soko la wanyarwanda,this man should have consulted the nation's economists before doing all this shit...the consumers take the burden hasa kwa neccessity goods kama mafuta..yetu macho,ninao JKT nawategemea sana.:tongue:
 
Kwani kagame ana watu wengi kias gani cha kuutishia uchumi wa Tanzania kwamba tunakosa soko huko??

Au kusema kwamba tunakosa ushuru wa kupeleka bidhaa?
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

OK!
Nimekuelewa!
So ngoma droo!
 
Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

Ni hiv: Kuna tetesi kwamba wafanya biashara wote wa Rwanda, wameambiwa wasipitishe mizigo katika Bandari ya Dar. Hii ni njia mojawapo ya kuwafanya wasipitishe mizigo hapa. Kuongeza ushuru wa barabara kutawafanya Wafanyabiashara wengi kuacha kutumia bandari yetu. Na hii ina madhara ya kiuchumi kwa serikali na watu binafsi pia. Wharfage na handling ambayo walikuwa wanalipa bandarini kwetu haitakuwepo tena na pia wasafirishaji watakosa mizigo....ajira hakuna.
 
Watakaoumia ni wanyarwanda wenyewe,kwani ninachojua hakuna mfanyabiashara anayepata hasara hata siku moja! hivyo kama bidhaa kama zinapelekwa Rwanda bei ya bidhaa zitapanda tu!

Hoja yako tamu kweli aisee maana hapa anachofanya ni kuchukia plate number za Tz wakati wanaoumia ni Wanyarwanda, ingekuwa kwa magari yanayotoka hapo ndio ingekuwa mkomoeni
 
Mimi nnadhani madhara ya kiuchumi yatatokea kwa upande wanTanzania,japo kwa kiwango fulani.Nnapata ukakasi kidogo kuchangia kwa ukamilifu kwa sababu hatujui gharama sahihi za kushusha/kupitishia mizigo ktk bandari ya Mombasa nchini Kenya vile vile kwa hapa kwetu Tanzania .

Ila kwa juu juu ni kuwa mfanyabiashara siku zote anahitaji unafuu katika biashara zake ili kupata faida na pia kuuza mali zake kwa wepesi hasa kutokana na bei.Kwa mfano wapo wanaosema wananchi wa Rwanda ndio watatishwa mzigo huu ulioongezwa na hilo nnakubaliana nalo ila tuchukulie mimi ni mfanyabiashara wa Rwanda nimeshusha mifuko ya saruji kupitia Tanzania na mfanyabiashara mwenzangu nae ameshusha hiyo hiyo mifuko ya saruji na yeye akatumia bandari ya Mombasa nchini Kenya.Swali la kujiuliza hapa ni hivi kama gharama za kushusha mzigo kupitia Mombasa zitakuwa ni za chini zaidi ya za Tanzania ni mfanyabiashara yupi atakubali kupitishia mzigo ktk bandari ya Tanzania.

Tukumbuke wafanyabiashara wanahitaji unafuu katika kazi zao ili waweze kwenda kushindana na soko huko wanapopeleka mizigo yao..

Nnawaomba wenzangu ktk jukwaa hili muache kuishambulia Rwanda na raisi wao,ile ni nchi na ina mamlaka zake tusiwaingilie ktk maamuzi yao hata kama watasema hakuna kuingiza magari yanayotoka Tanzania.Tujadili athari za kiuchumi kama mtoa mada alivyowasilisha,pia tungeomba wenye upeo zaidi katika taaluma ya uchumi waje huku watusaidie,lakini kuwashambulia kina Kagame na nchi yake haitotusaidia chochote.

Ka nchi kadogo sana kale,

Ingekuwa Rwanda ni nchi nawiri kama zanzibar kweli,ila sasa wale wana nin??njaa kali tuh maskin land locked wale,hawatunyimi usingiz sisi hata kidogo,hata kama athari tutapata kweli lakin sio kiivo kama wanavodhani wao,

Sisi maskin jeuri kweli kweli,sema tuh tumekosa usimamiz na tuna serikali lege lege na wakumbatia rushwa na ufisadi,ila RWANDA WASITUTISHE KWA LOLOTE
 
Afadhali wambie Kamanda, unajua Watanzania ni kama tumelogwa. Tunashabikia mambo bila kufikiria, watakao umia ni haohao wanaomiliki biashara za malori. Na hii maana ya haraka haraka ni kuanza ku discourage mizigokushushiwa Dar sasa watalazimika kwenda Bandari ya Mombasa.

Mambo mengine adghabu zake ni hapa hapa tu hakuna kungojea,

TAFAKARI

Hasira za mkizi! Anawaumiza watu wake mwenyewe! So wewe unataka JK aseme nini hasa pale unapoona kabisa usalama wa nchi yako unahatarishwa! Amekuwa mkali kisa JK amegusa M23 Anajua anachokifanya na hao waasi anafaidika nini na vita huko Goma Halafu anapewa ushauri anakuwa mkali utafikiri ametiwa pilipli machoni. He is a war criminal!
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

Sina hakika kwanini EAC hawajafanya harmonization katika hili, hata hivyo bado kuna mambo ya msingi nawe pia uyabainishe. 1. Je ushuru wa Barabara unakadiriwa kwa kutumia kigezo gani? kwasababu kama usemavyo ndivyo, kuna haja ya kujiuliza ukubwa wa athari kwa Barabara baina ya safari mbili (yaani kutoka Rusumo hadi Dar na kutoka Rusumo hadi Kigali). Nionavyo mimi magari ya Rwanda "yanaathiri" barabara kutoka Rusumo hadi Dar wakati yale ya Tanzania "yataathiri" barabara kutoka Rusumo hadi Kigali ambapo ni distance fupi (if am right). Hivyo ndiyo yaweza kuwa sababu ya kuweka tozo tofauti. Aidha sababu nyingine ni idadi ya magari yanayovuka kila upande (basing on revenue collection); kwa kuwa magari mengi ni kutoka Tanzania, kiwango kidogo cha tozo kinaweza kuleta makusanyo makubwa tofauti na magari yatokayo Rwanda kuingia Tanzania hayana budi kulipa kiwango kikubwa ili kuwa na significant revenue (kama siyo mengi).

Mkuu weka tofauti kando kaka, Hii ni business usifanye mchezo. Mwanzoni walikuwa wakitoza 150 USD per truck sasa wameongeza mpaka 500USD kwa magari ya TZ pekee, Ya nchi zingine wanachaji hiyohiyo 150usd. Sasa inaonekana hujui hali ipoje kaka.

Ikiwa kweli hali ndio iko hivyo, ni vema tujue charge kwa upande wa Rwanda/Kenya; Rwanda/Uganda na Rwanda/Burundi (ceteris paribus). Tukijua hivyo tutaweza kuona nini Tanzania inaweza kufanya. Na nmna mojawapo ni kutumia "US style"; kiburi cha Rwanda kinatoka Kenya, Mombasa Port na Trilateral cooperation lakini Kenya inauza Tanzania zaidi ya 50% ya mauzo yake yote EAC; hivyo namna rahisi ni ku-deal na Kenya kwa kumuanzishia masharti magumu ya kuingiza bidhaa zake Tanzania (based on cost-benefit analysis). Hii itamlazimisha Kenya apeleke hoja EAC kwanini Tanzania imeweka masharti mapya na hapo ndipo Tanzania ita-lobby kupata maamuzi yatakayotengua tozo mpya ya Rwanda (Reverts all new rates imposed by any EAC country on specific dates before negotiating) .

This is "news" to me! Kumbe haya malalamiko yetu hayana msingi wowote kata hali ni hii unayoisema!
Usiwe mwepesi mkuu, ngoja kwanza atupe info zaidi huyu murutongore kama yuko sahihi. Sioni kwanini Rwanda ilikuwa inataka kuwa na rate moja na Tanzania bilateral badala ya Regional? Na je vigezo gani havina budi kutumika kama tutafikia kuwa na equal rates wakati (huenda) magari kutoka kila upande yanatumia barabara umbali tofauti?

Mkuu, mkiona Kagame anapiga kelele ni amejaribu sana kuwa accomodating ila kuna mahali inafika mtu unashindwa kuvumilia. Tanzania inabidi mjirekebishe katika karne hii ya utandawazi na ushindani.
Toa maelezo zaidi acha unazi, Rusumo/Kigali-Rusumo/Dar how? Na je kwanini accomodating ya Kigali iwe bilateral badala ya Regional approach kama hiyo ndiyo hoja?
 
Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

Kama hayo yametokea its a pitty, inaitwa knee jack reaction on the part of Rwanda strongman Kagame! Ndio Tz tutapoteza revenue bandarini na jobs but Rwandese wataumia zaidi kwa kutumia Mombasa, it is 900 kms or more na hiyo gharama msafirishaji anairudisha kwa mlaji bila shaka! Poor Rwandans sasa ni wakati wa kuchukua maamuzi magumu.
 
Ni hiv: Kuna tetesi kwamba wafanya biashara wote wa Rwanda, wameambiwa wasipitishe mizigo katika Bandari ya Dar. Hii ni njia mojawapo ya kuwafanya wasipitishe mizigo hapa. Kuongeza ushuru wa barabara kutawafanya Wafanyabiashara wengi kuacha kutumia bandari yetu. Na hii ina madhara ya kiuchumi kwa serikali na watu binafsi pia. Wharfage na handling ambayo walikuwa wanalipa bandarini kwetu haitakuwepo tena na pia wasafirishaji watakosa mizigo....ajira hakuna.

Mnanishangaza sana watanzania, Rwanda ukubwa wake ni kama wilaya ya karagwe, kiasi kwamba mizigo yao ilikuwa ni tone kwenye uchumu wetu. Hatuna time nao waende kulima magimbi hatuna issue nao. Hapa mjue kuwa Rwanda haina biashara, au Zao ambalo linauzwa kwenye soko lolote duniani. waliingia kongo kwa mgongo wa m23 ili wachimbe madini angalu nao wapate pesa za kigeni.

Walipo ona Tanzania wamepeleka jeshi la kulinda amani nchini kongo wakaona tunakata mizizi ya biashara hiyo haramu ndo wakaanzisha bifu na Tz, wala tusipoteze muda na hao, make damu walizo mwaga kwa binadamu wasio na hatia zinawaru. So msipoteze muda na hiyo wilaya.
 
Kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya Mombasa badala ya Dar es Salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia Mombasa mambo yatatulia.

Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.

Mkuu wenye magar ya kusafirisha wao wataendelea kupga faida kama kawa wakipandsha kodi ya kuvuka pale na wao wanawabana wenye mzigo,wenye mzigo wanawabana watumiaji wanaoenda kuwauzia ss we unadhani Nan anaumizwa hapo kama sio wanyarwanda?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom