Mimi nnadhani madhara ya kiuchumi yatatokea kwa upande wanTanzania,japo kwa kiwango fulani.Nnapata ukakasi kidogo kuchangia kwa ukamilifu kwa sababu hatujui gharama sahihi za kushusha/kupitishia mizigo ktk bandari ya Mombasa nchini Kenya vile vile kwa hapa kwetu Tanzania .
Ila kwa juu juu ni kuwa mfanyabiashara siku zote anahitaji unafuu katika biashara zake ili kupata faida na pia kuuza mali zake kwa wepesi hasa kutokana na bei.Kwa mfano wapo wanaosema wananchi wa Rwanda ndio watatishwa mzigo huu ulioongezwa na hilo nnakubaliana nalo ila tuchukulie mimi ni mfanyabiashara wa Rwanda nimeshusha mifuko ya saruji kupitia Tanzania na mfanyabiashara mwenzangu nae ameshusha hiyo hiyo mifuko ya saruji na yeye akatumia bandari ya Mombasa nchini Kenya.Swali la kujiuliza hapa ni hivi kama gharama za kushusha mzigo kupitia Mombasa zitakuwa ni za chini zaidi ya za Tanzania ni mfanyabiashara yupi atakubali kupitishia mzigo ktk bandari ya Tanzania.
Tukumbuke wafanyabiashara wanahitaji unafuu katika kazi zao ili waweze kwenda kushindana na soko huko wanapopeleka mizigo yao..
Nnawaomba wenzangu ktk jukwaa hili muache kuishambulia Rwanda na raisi wao,ile ni nchi na ina mamlaka zake tusiwaingilie ktk maamuzi yao hata kama watasema hakuna kuingiza magari yanayotoka Tanzania.Tujadili athari za kiuchumi kama mtoa mada alivyowasilisha,pia tungeomba wenye upeo zaidi katika taaluma ya uchumi waje huku watusaidie,lakini kuwashambulia kina Kagame na nchi yake haitotusaidia chochote.