Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
uono wa kisigino..............kinaona
kilipotoka na si kinapoenda..................siyo kosa lako mkuu
50 yrs ya uhuru, maendeleo mpaka tuambiwe, lakini kwa macho hayaonekani. Hilo ni kosa lako kuamini na kushabikia CCM
 
Hatimaye serikali ya RWANDA yapandisha ushulu wa kulipia mpakani kwa magari ya kutoka TANZANIA pekee, Magari yote yaliyosajiliwa TANZANIA yamepandishiwa bei kutoka Dolla 153 hadi dolla 500. Hii inaonesha picha kamili kwa kutaka wafanyabiashara kutoka Rwanda wahamie Mombasa . kwa upande wa Kenya na Uganda ushulu kwa magari yanayoingia Rwanda imebaki dolla 153. HUYU JAMAA ANAITAJI KUFUNDISHWA.​
 

yani tunaumiza kichwa kisa ka nchi kama Rwanda ambayo idadi ya mizigo yake yote inayoshafirishwa uko ni kidogo kuliko mizigo inapelekwa kwenye mkoa wa arusha.
 
Watakaoumia ni wanyarwanda wenyewe,kwani ninachojua hakuna mfanyabiashara anayepata hasara hata siku moja! hivyo kama bidhaa kama zinapelekwa Rwanda bei ya bidhaa zitapanda tu!

kuna mtu mmoja aliwahi kupost akisema kagame ni mad man.
Kwa move hii atawachinja wafanyabiashara wa Rwanda wote maana hawatakubali kusafirisha mizigo kutoka mombasa mpaka rwanda wakati shortcut ipo.

hajui hata hesabu ya kujumlisha. Anadhani anawakomoa watanzania kumbe anamkomoa mlaji ambaye ni mnyarwanda atakayelipia gharama ya kulipia hiyo dola 500.
 
Nauli ikiongezeka atakeumia ni Mwananchi wa kawaida wa Rwanda, hiyo gharama inachanganywa kwenye bidhaa anapelekewa mlaji.!!
 

Malipo ya ubaguzi, ukijiona wewe mbabe, wenzako nao watakuonesha jeuri yao, tulipofanya unyanyapaa kwa wanyarwanda mlidhani wao watatulia tu kama kondoo!

Majuto ni mjukuu.
 
Hii ni vita baridi ambayo mwisho wake cjui utakuwa je?
 
Katika hali ya kushangaza Serikali ya Rwanda imeongeza bei/gharama kwa mabasi yanayotoka Tanzania kwenda Rwanda. Kutoka USD 152 mpaka USD 500! Kweli Kagame yuko serious..

SOURCE: EATV News

Mkuu una uhakika ni Ma basi ???
 
yani tunaumiza kichwa kisa ka nchi kama Rwanda ambayo idadi ya mizigo yake yote inayoshafirishwa uko ni kidogo kuliko mizigo inapelekwa kwenye mkoa wa arusha.

Wapo watanzania wanaoishi kwa kufanya biashara na hako karwanda utawatafutia biashara mpya na masoko mapya.

hata kama ni wachache bado athali zake tutazipata tu.

Kama fedha ipo ya kutosha kwanini wanalazimisha kodi ya kadi za sim? sisi Tz ni masikini tu.
 
Kwani Rwanda wanaenda Watanzania au Warwanda? Huyu kagame mgonjwa kweli!!!
Katika hali ya kushangaza Serikali ya Rwanda imeongeza bei/gharama kwa mabasi yanayotoka Tanzania kwenda Rwanda. Kutoka USD 152 mpaka USD 500! Kweli Kagame yuko serious..

SOURCE: EATV News
 
Wakuu sio Ma Basi , ni Ma roli, Hebu leteni Habari za kueleweka jamani
 

Atacompansate na mapato ya madin kutoka drc anaakili ya hesabu kuliko yako, unadhani kwanini hakuna nyumba za nyasi kule tafuta majibu.
 
Tumia akili, hapo maana yake ni kuwalazimisha wafanyabiashara wa Rwanda wapite Mombasa.

Au kwa namna nyingine kuwafanya wafanya biashara wa Rwanda wasitumie Bandari ya Tanzania
 
ni sawa na kodi ya bia inapopanda anayelipa ni mnywaji.
 
Ngoja nikujibu, kwa miaka zaidi ya 20 tulikua tunakaa na warwanda bila ya Jk kulalamika toka akiwa w. Mambo ya nje mpaka hi leo, iweje wahamiaji haramu watafutwe Kagera ,Geita, Kigoma? Je hawapo Namanga? Mbeya je Dar je? Mwaga ugali nimwage mboga
 
Last edited by a moderator:
Nimesema sana nimebezwa.

Lazima tuwe na viongozi wenye hekima, busara na wenyekujali utu. Mwl Julius Nyerere pamoja na udogo wake hakuipuuza wala kuidharau Zanzibar, aliipa heshima kamili. hakuwapuuza wala kuwabaguwa majirani zake, tumepata watawala wasionaaibu wala hawaoni mbele, kwao lazima visasi na uwongo ndiyo sera.

Tutawapuuza wanyarwanda lakini kuna baadhi ya watanzania watapoteza mali na hata kufilisika kwa sababu za kijinga kabisa wala hazina mashiko kwa mtu yoyote mwenyekufikiri vema.

Lazima tuzingatie mahusiano bora na majirani zetu kwa matokeo bora ya tanzania ya kesho
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…