Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
Afadhali wambie Kamanda, unajua Watanzania ni kama tumelogwa. Tunashabikia mambo bila kufikiria, watakao umia ni haohao wanaomiliki biashara za malori. Na hii maana ya haraka haraka ni kuanza ku discourage mizigokushushiwa Dar sasa watalazimika kwenda Bandari ya Mombasa.

Mambo mengine adghabu zake ni hapa hapa tu hakuna kungojea,

TAFAKARI

Hakuna mtanzania ataumia hapo wewe, Tanzania inasafirisha mizigo Kongo, Zambia, Burundi, Malawi n.k. hawategemei Rwanda peke yake. Utakuta hiyo USD 500 ni ndogo kuliko gharama za kusafirisha mzigo kutokea Mombasa kutokana na Jeografia ilivyo. Kwa maana hiyo, bidhaa ikitokea Mombasa bado itapanda bei na ile itakayotozwa USD 500 itapanda bei pia, ataumia mlaji wa Rwanda.
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

du....kama ni ivo,sawa tu
 
Kila nchi sasa ni majanga tupu hasa sisi wa Afrika
ali ya uchumi ni ngumu mno palipobaki ni kutafunana wenyewe kwa wenyewe.mimi sina mchango wowote kwani maneno hayataifanya serkali ya Rwanda kupunguza kodi
 
Sina hakika kwanini EAC hawajafanya harmonization katika hili, hata hivyo bado kuna mambo ya msingi nawe pia uyabainishe. 1. Je ushuru wa Barabara unakadiriwa kwa kutumia kigezo gani? kwasababu kama usemavyo ndivyo, kuna haja ya kujiuliza ukubwa wa athari kwa Barabara baina ya safari mbili (yaani kutoka Rusumo hadi Dar na kutoka Rusumo hadi Kigali). Nionavyo mimi magari ya Rwanda "yanaathiri" barabara kutoka Rusumo hadi Dar wakati yale ya Tanzania "yataathiri" barabara kutoka Rusumo hadi Kigali ambapo ni distance fupi (if am right). Hivyo ndiyo yaweza kuwa sababu ya kuweka tozo tofauti. Aidha sababu nyingine ni idadi ya magari yanayovuka kila upande (basing on revenue collection); kwa kuwa magari mengi ni kutoka Tanzania, kiwango kidogo cha tozo kinaweza kuleta makusanyo makubwa tofauti na magari yatokayo Rwanda kuingia Tanzania hayana budi kulipa kiwango kikubwa ili kuwa na significant revenue (kama siyo mengi).



Mkuu salute nimependa uchambuzi wako. Tatizo sasa ni hao watendaji inakuwaje,
chama@ZeMarcopolo@Ritz hivi TISS haina kitengo cha ECONOMIC INTELIGENCY UNIT ambacho kinadeal na mambo ya business both domestic na international?

hao tiss wanaosifiwa na WAR-SIRA????
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usiwe na shaka, hizo ni hasira za mkizi tuu. PK anawatwisha mzigo wananchi wake, huo ni uamzi wa kisiasa zaidi sio technical. Nimesikiliza Times FM, Kwamba magari ya nchi zingine ushuru haujapanda ila ya TZ umepanda 3 times.

Rule of the game lazima itaaply tuu na hapo ndoo PK atakubali.(kama wewe ni mfanya biashara hope unaelewa ninaposema RULE OF THE GAME). Hilo ongezeko effect zake ataziona mda si mrefu sana.


cc ZeMarcopolo

Litakuwa ni kosa kubwa ikiwa Rwanda imefanya hivi (sitaki kuamini) kwa sababu ni kinyume cha Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Soko la Pamoja. Hairuhusiwi kuweka viwango vya tozo au ushuru unaobagua watoa huduma. Ngoja tusubiri maelezo yao na ya Wizara yetu ya Afrika Mashariki.
 
Ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. Haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
sasa kama hataki msalimiane wewe utamlazimisha......................
 
From the content ni kwamba ushuru umepanda kwa magari ya Tanzania pekee kutoka Dola 150 hadi Dola 500 huku magari kutoka nchi nyingine yakilipa ushuru za zamani,kwa maana nyingine ni "Magari ya Tanzania yanazuiliwa kuingia Rwanda"


Akufukuzaye hakwambii toka.

Kama haya ni ya kweli, basi wa kuumia hapa ni mwananchi wa rwanda ambaye general supplies nyingi anazipata kutoka ama kupitia tz, raia wa rwanda atakayeshabikia hili atakuwa hajui atendalo
 
Last edited by a moderator:
jamaa yatu sasa anakoendea sipo .nadhani mda wake kutawala rwanda unakaribia ukingoni.ana chokochoko sana na tanzania ,ajifunze kwa iddi amnini na mobuttu shauriyake .watanzania tumezoeha kufunga mikanda.hii yote ni hasira za kundi lake la m23 kulifukuza congo.
 
Last edited by a moderator:
ccm haihusiki hapo bali ni jeuri na kiburi cha mhuni kagame
It takes two to tango, kama unadhani CCM haihusiki, subiri joto la jiwe. Unakumbuka after vita vya Mtukula, tulivaa matairi ya gari, mbunju na maduka ya kaya.
 
ifike mahali hii cold war iishe. Tena tuache kabisa kushabikia haya mambo. haipendezi kuwa na jirani ambaye hamsalimiani hata kama wewe ni tajiri na una kila kitu.

Sent from my blackberry 9860 using jamiiforums

hapo penye red hata mie nashindwa kuelewa inakuwaje jirani yetu pk hata kama anasifiwa na ulaya yote kuwa uchumi wake umekuwa inakuwaje anakataa ushauri wa jirani wa kumtaka aongee na ndugu zake wa damu wakae kwa amani..kisha anatutukana na kutishia kutuadabisha na hasa rais wetu.

Huyu hafai kuwa jirani yetu..amepotea njia kuja kukaa karibu na sie wastaarabu...asubirie majibu coz hata amini dada alikosea njia tukamtoa na kuwaweka kina m7.

Na tall atatoka tuu aendelee kutapatapa aone kama hatujamwambia kenya achague rwanda au tanzania yupi awe marafiki zake.
 
Amwulize mfalme Nebkadreza alivyofamywa na nguvu ya Mungu ,na atayaona ya Filaini
 
Kama kuna mwana JF ambaye ana data za kiasi cha mizigo ambayo inapitishwa hapa Tanzania kwenda Rwanda atupatie ili tujue ni hasara kiasi gani ambayo labda tunaweza au tumeanza kuipata,maana tusishabikie upuuzi anaoufanya PK kwa kigezo cha kupata hela,lazima tulinde na heshima yetu wana JF.
 
ha ha haa, siku tukiyumba kiuchumi kutoka na vikwazo vya rwanda mimi nakunywa sumu live..! Yaani ni sawa na singida iiwekee vikwazo dar

mkuu leo nimecheka mbavu zinaniuma..tutakutana tunywe laivu na tv iwaonyeshe watanzania...hiyo ni kupinga mende rwanda kuangusha kabati tanzania...ahahahahaaaaaaaaaaaaaa. Hawa wenye pua ndefu kumbe akili ni fupi kiasi hiki....mungu wasamehe hawajui wanajitia kitanzi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom