Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
wewe chunga mdomo wako! sisi huwezi kutulinganisha na kinchi kama mkoa wa singida! sisi tuna bandari,maziwa na visiwa, mapori,milima na takataka kibao mpka nchi matajiri wanatugombania hao wana nini zaidi ya damu ya ma elf ya watu katika nchi ndogo kama hiyo!

Yaani wewe ndio kabisaaa. Kwa hiyo unajivunia kugombaniwa na wazungu na wachina. Hiyo mentality ndio unazaa umaskini. Unajua hadithi ya mwanamke mtaani aliyekuwa anagombaniwa na vijana wote wa mtaani? Mwisho wake ni nini?
 
Watakaoumia ni wanyarwanda wenyewe,kwani ninachojua hakuna mfanyabiashara anayepata hasara hata siku moja! hivyo kama bidhaa kama zinapelekwa Rwanda bei ya bidhaa zitapanda tu!

jameni acheni ushabiki wa kijinga! hivi kama kweli ushuru umepanda kwa magari ya kitanzania tu, inamaana wafabiashara wataacha kukodi malori ya Tanzania na hivyo watatumia magari yasiyosajiriwa Tanzania pia itafanya wafanya biashara wa Rwanda kuteka soko la usafirishaji katika ukanda huo!
bidhaa haziwezi kupanda wakati sio wote waliopandishiwa huo ushuru, yaani haiwezekani wengine wapandishe bei na wengine wasipandishe halafu nyie mnaolipa ushuru mkubwa m-survive pamoja na hao wasiopandishiwa ushuru katika soko moja! never under the commercial world!
 
Nafikiri sasa inatakiwa tuendelea kuomba kuwe na amani maana hakuna haja yakuonyeshana nani zaid wakati Wanyarwanda hawa wamekulia ama kuzaliwa kigoma na sehemu nyingine lakini sasa wamesahau
 
Kumbe sisi ndio wenye makosa sasa kwanini tuwatoze road toll kubwa magari ya Rwanda na kuwaacha wengine na toll ile ile. Kwa hili wa kulaumiwa ni Serikali ya Tanzania kwa kutafuta unnecessary frictions na majirani zetu. Tangu wapo hatukubaliani kwenye Congo basi na hili tuwekane sawa.
 
Hali iliyopo kati ya Rw na Tz haifurahishi hata kidogo. Kijamii ni hasara kwa pande zote. Hivi ni jirani gani hulala usingizi mzito wakati uhusiano kati yake na jirani yake ni wa uadui/mashaka?
Kijamii binadamu yeyote huchagua rafiki. Nani anamchagua jirani yake? Tupende tusipende uhusiano wetu na Rwanda unatakiwa uwe mzuri kwa juhudi za Rw na Tz. Tusije tukafanya kosa la kudhani kuwa mmoja kati yetu ni wa muhimu kuliko mwingine! Tunahitajiana. Ni wakati mwafaka tunaowalipa kwa ajili ya shughuli za uhusiano wa kimataifa wakaonyesha ujuzi wao wa kazi.
 
Jamii Forums ni kisima cha habari zote, kwa hiyo Taarifa nyingi za vyombo vya Habari km magazeti TV nk huanzia hapa, siwezi kulaumu mleta Mada kwani ilikuwa post yake ya kwanza au hakujua chanzo cha huo mgogoro wa ushuru kuwa ni dola za Marekani 16 kwa kila kilometa 100, ushuru ambao ndio uliokuwa ukitozwa na Tanzania kwa malori yaliyokuwa yakipitisha mizigo kwenda nchi za nje.

Rwanda iliamua kupandisha ushuru huo, kutoka dola 16 kwa kilometa 100, hadi dola 152 bila kuzingatia kilometa.
Kabla ya kupandishwa kwa ushuru huo, Tanzania ilionekana kupata faida, kwa kuwa kutoka Dar es Salaam hadi Rusumo, ni kilometa 1,350 na hivyo kwa ushuru wa dola 16 kwa kilometa 100, Serikali ilipata dola 216 kwa gari.

Kwa Rwanda taarifa zinaeleza kuwa hali ilikuwa tofauti kutokana na udogo wa nchi, ambapo kutoka Rusumo hadi Kigali ni kilometa 139, ambao kwa ushuru huo wa dola 16 kwa kilometa 100, Serikali ya Rwanda ilijikuta ikiambulia dola 22.24 tu kwa gari.

Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, alikiri Wizara yake kupata taarifa za kupanda kwa ushuru huo kupitia wafanyabiashara, lakini hadi sasa wizara hiyo haijapewa taarifa rasmi na Rwanda.

Alisema juzi akiwa katika kikao hicho cha mawaziri wa Afrika Mashariki, Wanyarwanda walikuwa wakilalamikia kiasi cha ushuru kinachotozwa nchini katika barabara kuwa ni mkubwa ikilinganishwa na nchi za Afrika Mashariki.
Alisema kutokana na malalamiko hayo, alilazimika kuwajibu kuwa ushuru huo ni lazima utozwe kutokana na vigezo vilivyowekwa na lengo lake kubwa ni kulinda barabara.

1.png

Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

UPDATES - 03.09.2013

Bado nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda, kwa habari ambazo ni rasmi Serekali ya Rwanda imefuta ongezeko la ushuru wa barabara ( Road Toll) la USD 500 kwa kila gari lenye usajili wa Tanzania na kuanzia leo kila gari litavuka kwa ushuru wa zamani wa USD 152. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye plate numbers za Rwanda kutoka USD 500 mpaka USD 150. Hatua hii inaoenakana ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa umbali kutoka Dar mpaka Rusumo sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka Kigali....kwahiyo ushuru wa barabara hauwezi kuwa sawa kwa simple basics za economics.....

mkuu twambie je magari yote yanayotumia barabara ya tz yalichajiwa hiyo hela au ni yale ya rwanda tu?
 
Nimegundua kuwa Kagame si kitu wala si tishio kwetu. Ukweli ni kuwa msaliti wetu nambari moja ni Rais Kenyatta akiungwa mkono na Museveni. Huyu Kagame si kitu kabisa.

Kosa kubwa ambalo Serikali yetu ilifanya ni kukubali kuwaacha Kenyatta, Museveni, na Kagame wakindelea na vikao binafsi kwa jina la EAC integration vila ya sisi kushiriki wakati Tanzania nasi ni sehemu ya EAC!

Ukweli ni kuwa tulipuuzia mambo muhimu wakati tunaona maadui~Kagame na Museveni wakipatana wakati ambapo Kenyata kila siku anatafuta fursa ya kupanua biashara za familia yake.

Nadhani hii tabia yetu Watanzania kupuuzia mambo ndio inayotugharimu.
 
RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA

Tuesday, September 3, 2013 | 11:25 AM

1.png
RWANDA imeamua ‘kucheza rafu' kwa kuanza kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam, kwa kupandisha ushuru wa barabara kwa magari ya mizigo yanayotoka Tanzania pekee kuanzia Rusumo hadi Kigali, kutoka dola za Marekani 152 za awali, hadi 500.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichomalizika hivi karibuni Arusha, ushuru huo ulianza kutozwa rasmi kwa magari hayo juzi.

Hali hiyo imesababisha mtafaruku katika eneo la Rusumo, mpakani mwa Tanzania na Rwanda, ambako zaidi ya malori 200 yenye mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, yamekwama kwa kushindwa kulipa kiwango hicho kipya cha ushuru wa barabara.

Awali nchi hiyo ilikuwa ikitoza ushuru wa dola za Marekani 16 kwa kila kilometa 100, ushuru ambao ndio uliokuwa ukitozwa na Tanzania kwa malori yaliyokuwa yakipitisha mizigo kwenda nchi za nje.

Hata hivyo, katika kilichoonekana kuwa mazingira yasiyo sawa ya kupata faida kutokana na udogo wa eneo wa nchi hiyo, Rwanda iliamua kupandisha ushuru huo, kutoka dola 16 kwa kilometa 100, hadi dola 152 bila kuzingatia kilometa.

Kabla ya kupandishwa kwa ushuru huo, Tanzania ilionekana kupata faida, kwa kuwa kutoka Dar es Salaam hadi Rusumo, ni kilometa 1,350 na hivyo kwa ushuru wa dola 16 kwa kilometa 100, Serikali ilipata dola 216 kwa gari.

Kwa Rwanda taarifa zinaeleza kuwa hali ilikuwa tofauti kutokana na udogo wa nchi, ambapo kutoka Rusumo hadi Kigali ni kilometa 139, ambao kwa ushuru huo wa dola 16 kwa kilometa 100, Serikali ya Rwanda ilijikuta ikiambulia dola 22.24 tu kwa gari.

Kutokana na mazingira yaliyoonekana ya kutopata sawa na Tanzania, yaliyotokana na udogo wa nchi husika, Rwanda ilipandisha ushuru huo na kuwa dola 152 bila kujali umbali, kwa kuwa kijiografia haukuwa na msaada kwao.

Hata hivyo, taarifa zimeeleza kuwa Tanzania haikulalamika kwa ongezeko hilo la ushuru na iliendelea kufanya biashara na Rwanda kama inavyofanya na nchi zingine zinazopitisha mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hujuma kwa Tanzania
Katika mazingira yanayotafsiriwa kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam, nchi hiyo mwanachama mwenza wa Afrika Mashariki, imepandisha ushuru tena hadi dola 500, mara hii ushuru huo ukiwa kwa magari yanayopita Bandari ya Dar es Salaam tu.

Ushuru huo kwa mujibu wa taarifa hiyo, ulitangazwa ghafla muda mfupi baada ya Kenya kutangaza kuondoa vikwazo vya barabara kwa magari ya mizigo inayopita katika Bandari ya Mombasa kwenda Kigali.

Mfanyabiashara aliyeathirika na ushuru huo, alisema sasa ni wazi kuna jaribio la Rwanda kuonesha kuwa usafirishaji wa mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali, umbali wa kilometa 1,350, ni aghali kuliko kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mombasa hadi Kigali, umbali wa zaidi ya kilometa 2,700.

Taarifa rasmi
Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, alikiri Wizara yake kupata taarifa za kupanda kwa ushuru huo kupitia wafanyabiashara, lakini hadi sasa wizara hiyo haijapewa taarifa rasmi na Rwanda.

Alisema juzi akiwa katika kikao hicho cha mawaziri wa Afrika Mashariki, Wanyarwanda walikuwa wakilalamikia kiasi cha ushuru kinachotozwa nchini katika barabara kuwa ni mkubwa ikilinganishwa na nchi za Afrika Mashariki.

Alisema kutokana na malalamiko hayo, alilazimika kuwajibu kuwa ushuru huo ni lazima utozwe kutokana na vigezo vilivyowekwa na lengo lake kubwa ni kulinda barabara.

"Kama Wizara hatujapata taarifa rasmi, lakini tumepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu kutozwa ushuru huo mpya, tunachofanya sasa ni kuangalia namna suala hili litakavyoathiri usafirishaji na baada ya hapa, tutashauri wizara za fedha na ujenzi hatua za kuchukua," alisisitiza.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax ambaye sasa ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), alisema hatua hiyo ya Rwanda kupandisha ushuru ni ya kutengeneza ushindani usio sawa.

Kwa mujibu wa Dk Tax, kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam inafanya vizuri ikilinganishwa na ya Mombasa na ndiyo maana anaona ushuru huo ni wa kuweka mazingira yasiyo sawa ya ushindani kati ya Bandari ya Dar es Salaam na ya Mombasa.

"Tangu Rwanda ilipojiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilikuwa ikilalamikia vikwazo vya Tanzania vya barabara, lakini ukweli ni kwamba Tanzania na Kenya zimekuwa zikijenga barabara zake zenyewe, ndiyo maana ni vema zitengeneze mkakati wa kudhibiti matumizi ya barabara hizo ili zikiharibika kuwe na fedha za kuzikarabati," alisema.

Suluhisho
Hata hivyo, Dk Tax alisisitiza kuwa kabla ya kuondoka wizara hiyo ya Afrika Mashariki, tayari nchi za Jumuiya hiyo zilikuwa na mkakati wa kuanza kutumia kiwango kimoja cha uzito wa magari kisichozidi tani 55, ili kuhakikisha miundombinu ya nchi hizo hususani barabara haiharibiwi na uzito wa magari hayo.

"Hili ndilo suluhisho la pekee iwapo nchi zote za Afrika Mashariki zitakuwa na kiwango kimoja cha uzito, hata tozo za ushuru zitakuwa sawa na ushindani inaowaumiza wafanyabiashara hautakuwapo," alisisitiza.

Msemaji wa Chama cha Umoja wa Wasafirishaji wa Malori nchini (TATOA), Zacharia Hans-Pope, alikiri kuwa na taarifa za kupandishwa kwa ushuru huo na hadi jana jioni magari ya mizigo zaidi ya 200 yalikuwa yamekwama Rusumo kutokana na kushindwa kulipa tozo hiyo.

"Magari zaidi ya 200 yamekwama pale Rusumo kwa kuwa hayana uwezo wa kulipa tozo hiyo… ni kubwa mno, sisi chama tunasubiri tamko la Serikali ya Tanzania, kwanza hatukuwa na taarifa kabisa juu ya suala hili," alisisitiza.

Alisema ushuru huo utakuwa ‘mwiba' kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa utaifanya ionekane kuwa ya gharama kusafirisha mizigo kwenda Kigali jambo ambalo si la kweli.

Ni nchi za SADC pekee ndizo zenye ushuru mmoja wa barabara ambao ni dola 16 kwa kilometa 100 za barabara, lakini bado Jumuiya ya Afrika Mashariki haijaweka kiwango kimoja cha tozo hiyo.

Read more: RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA - GUMZO LA JIJI
 
mashambulizi yapo ya aina nyingi, hata kutoza ushuri mkubwa kwa malori ya tanzania ni aina ya mashambulizi , yapo mengi yanayothibitisha hujuma za pk kwa watanzania na tanzania (1)kuanza na vikao vya kujaribu kuitenga tanzania na mataifa mengine jirani, (2)kuhusika kwa majeshi ya rwanda moja kwa moja kuyahujumu majeshi ya tanzania yaliopo huko drc kwa mwavuli wa kulinda amani wa un, haya na mengineyo mengi ya kiintelijensia yanatufanya tuwe tayari kwa lolote dhidi ya huyu dikteta , anaweza akaamua lolote BAYA MUDA WOWOTE DHIDI YA WATANZANIA !
Kuhusu # 1, it is impossible kama viongozi wetu ni wazuri, lakini tumeshuhudia Malawi. Haiwezekani tuwe na matatizo na nchi mbili tofauti at the same time. Something wrong somewhere, evaluate yourself and Be smart. Kuhusu # 2, kwanini tumepeleka majeshi DRC in the first place?
 
hivi huo uamuzi kaufikia baada kushauriana na wataalamu wake au kaufanya mwenyewe out of anger. Final consumer ndo ataumia ; lorry haliwezi kosa kazi nyingine ya kufanya. Ataiua nchi yake na asipoangalia watampindua wao wenyewe!
 
Kuhusu # 1, it is impossible kama viongozi wetu ni wazuri, lakini tumeshuhudia Malawi. Haiwezekani tuwe na matatizo na nchi mbili tofauti at the same time. Something wrong somewhere, evaluate yourself and Be smart. Kuhusu # 2, kwanini tumepeleka majeshi DRC in the first place?

mgogoro wa malawi sio wa leo, unayo historia ndefu, tangu enzi za mwalimu, na sasa umechagizwa na siasa za mama banda ni kiongozi mtata hata nyumbani kwake! Kwanini umelenga moja kwa moja DRC na si kwingineko ambapo majeshi yetu yalikuwepo na yanaendelea kuwepo? mfano lebanoni, liberia, darfu , comoro nk Sisi ni sehemu ya dunia hii na kamwe hatuwezi kuishi kama kisiwa hata kama tungekuwa na kila kitu majeshi yetu kongo ni kuitikia mwito halali wa jumuiya ya kimataifa ya kulinda usalama wa wananchi wa DRC dhidi ya uasi unaoungwa mkono na serikali ya mdhalimu kagame. Acha ushabiki siyo kila jambo ni kupinga tu, kikwete kwa hili hana doa ! watusi mtahangaika sana na chuki zenu na mwisho wenu ni mbaya.
 
kwa msaada tu, watanzania wengi ni miongoni mwa jamii chache sana duniani tuliokuwa tunaamini mlinyanyaswa sana na wahutu na mlikuwa mnahitajia msaada wetu ili kuponya madhara ya genocide lakini mungu ametufunulia tumejua sura yenu halisi, watusi ni ndumi lakuwili awe ni mazaliwa wa tanzania, uganda au rwanda au popote pale sasa ni handle with care hata mtanzania mtoto mchanga kabisa analijua hilo sasa.
 
tutawapeleka mizigo hadi mpakani wenyewe watasombelea kwa magari yao
 
Mama Banda mkorofi, Kagame ni mkorofi na JK ni daktari wa kutibu wakorofi? I don't buy any story and I' m against war, there are too many diplomat ways to resolve these issues. TZ ikiingia vitani na Rwanda/Malawi, tutakakula mawe na kusaga meno, JK na wapambe wake wataendelea na masafari yao nje. Unakumbuka mabomu ya Gongo la mboto, JK aliondoka kama nothing happened, the man doesn't care, its all about matanuzi
 
ndugu yangu wala sioni sababu kukubishia maoni yako, kila shetani na mbuyu wake

Utawala wa JK nyerere walikuwepo approx 25yrs

Utawala wa mzee A. H Mwinyi walikuwepo-10 yrs

Utawala wa Mzee wa uwazi na ukweli bwana mkapa walikuwepo-10yrs

zaidi ya miaka arobaini na tano (45yrs) ni mangapi wamefanya kwa taifa hili na wangapi tumezaliwa tukawakuta hawa ndugu?

Cha jabu utawala wa mh kikwete mambo si mambo, jirani zetu takribani wote mfadhaiko, hata sisi wenyewe watanzania humu ndani mambo yamebadilika tunaishi kwa mashaka, mabomu, tindikali, kuchinjana, kutesena nk

Tujiulize katika utawala huu nini kimetokea?

>Utawala wa ------ ni 3 much
 
Mama Banda mkorofi, Kagame ni mkorofi na JK ni daktari wa kutibu wakorofi? I don't buy any story and I' m against war, there are too many diplomat ways to resolve these issues. TZ ikiingia vitani na Rwanda/Malawi, tutakakula mawe na kusaga meno, JK na wapambe wake wataendelea na masafari yao nje. Unakumbuka mabomu ya Gongo la mboto, JK aliondoka kama nothing happened, the man doesn't care, its all about matanuzi

vita ya malawi/rwanda haitakuwa vita ya kwanza kupiganwa na watanzania! tulishapigana vita nyingi sana na nyingine zikiwa hazina hata masilahi kama inavyoelekea kuwa kwa vita ya rwanda kutokea DRC . Vita ni vita lolote laweza kutokea ila malengo ni lazima yafikiwe.tumepigana katika vita ya ukombosi kusini mwa afrika, tuliikomboa comora, nk endelea na umbea
 
kwa msaada tu, watanzania wengi ni miongoni mwa jamii chache sana duniani tuliokuwa tunaamini mlinyanyaswa sana na wahutu na mlikuwa mnahitajia msaada wetu ili kuponya madhara ya genocide lakini mungu ametufunulia tumejua sura yenu halisi, watusi ni ndumi lakuwili awe ni mazaliwa wa tanzania, uganda au rwanda au popote pale sasa ni handle with care hata mtanzania mtoto mchanga kabisa analijua hilo sasa.
Another foolish theory, mipaka iliwekwa na Babylon ili watutawale kirahisi, we are one. Nenda nje hasa ulaya na marekani utagundua waafrica wote ni one. Wanashirikiana almost katika kila kitu, ni wewe na CCM wenzako mnaoeneza ubaguzi, mlianza na dini, mkaja na ukanda, sumu ambayo itawamaliza
 
vita ya malawi/rwanda haitakuwa vita ya kwanza kupiganwa na watanzania! tulishapigana vita nyingi sana na nyingine zikiwa hazina hata masilahi kama inavyoelekea kuwa kwa vita ya rwanda kutokea DRC . Vita ni vita lolote laweza kutokea ila malengo ni lazima yafikiwe.tumepigana katika vita ya ukombosi kusini mwa afrika, tuliikomboa comora, nk endelea na umbea

Yaani wewe ni zuzu kweli. Unashabikia vita! Njoo huku Goma basi ufanye mazoezi. Kawaida watu wenye maneno mengi kama wewe huwa action ni zero. Njoo huku uwaepushe watanzania wenye kupenda amani. Njoo usikie risasi zinavyolia uone kama hutajinyea. Stupid is as stupid says.
 
vita ya malawi/rwanda haitakuwa vita ya kwanza kupiganwa na watanzania! tulishapigana vita nyingi sana na nyingine zikiwa hazina hata masilahi kama inavyoelekea kuwa kwa vita ya rwanda kutokea DRC . Vita ni vita lolote laweza kutokea ila malengo ni lazima yafikiwe.tumepigana katika vita ya ukombosi kusini mwa afrika, tuliikomboa comora, nk endelea na umbea
Unakumbuka baada ya vita ya mtukula? wengi wa wale waliopigana vita, ndio hao wapo mitaani wakiomba omba baada ya kupata vilema na serikali ya CCM imewatupa kabisaa. Unakumbuka hali ya maisha ilivyokuwa ngumu? do you really wanna go there again? Ain't got no time to talk to you and don't waste your valuable time to talk to me, just nenda kajiandikishe jeshini uende vitani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom