Maendeleo ni ya watu, na si vitu. Maana hiyo ni mpaka hapo asilimia 80+ ya Watanzania watakapomudu kula milo mitatu ya wastani, kuwa na makazi yanayofaa binadamu kuishi, kuwa na huduma za elimu bora, afya, maji na usafiri wa kukidhi kwa wastani.
Zaidi ya hayo, kuwa na uhuru wa kutonyanyaswa na polisi, uhuru wa kutoa maoni, kuishi kwa amani bila hofu yeyote, kumchagua wampendaye kuwaongoza.
Sidhani haya yatapatikana katika miaka mingine 60 ijayo. Kama unaaamini yatapatikana niambie, vipi?
Ni mada nzuri, tena umeweka mhtasari ulio shiba kabisa!
Nami ningetamani hayo uliyoyaeleza hapa yapatikane katika uhai wa kizazi hiki, na ninaamini yangewezekana kwa sehemu kubwa kutimia kama tungefanikiwa kuwa na viongozi 'determined' kabisa kuyatimiza. Viongozi ambao kuwepo kwao si kwa minajiri ya kujinufaisha au kujitafutia sifa.
Viongozi ambao wamejitoa kabisa kwa Tanzania yenye mafanikio hayo.
Viongozi ambao wanajua ni vipi vipaumbele vinavyotakiwa kufanywa ili kufika huko kwa haraka, na wako tayari kuwekeza raslimali katika maeneo hayo ya vipaumbele.
Viongozi wanaojua kwamba maendeleo hayo ya nchi yetu hayaletwi kwetu na watu wengine, bali kazi kubwa ya kuyaleta ni sisi wenyewe; kwa hiyo wangehimiza na kuelimisha wanchi waielewe hali hiyo na kuwapa nyenzo muhimu za kufanya hivyo
Ili uweze kutatua tatizo linalokukabili ni lazima ujuwe tatizo lenyewe lilivyo. Kwa hiyo viongozi hawa wanatakiwa kuwa na ufahamu mzuri kabisa ni wapi hasa panapotupa shida ya kutokwenda mbele haraka ili kufikia lengo hilo uliloliweka kwenye mada yako.
Viongozi wanaojipigia tu mradi liende, matokeo yake ni yaleyale ya kuzungukia humo humo tulimokwishapitia bila ya kwenda mbele.
Tazama, tupo kwenye hatua nzuri sana kuinuka kwa haraka na kufika huko unakokutamani. Chukulia mifano ya maji na umeme, kwa mfano, tukidhamiria kweli katika miaka mitano ijayo tukisema tunataka maji na umeme viwe vimesambaa maeneo yote ya nchi, hili kweli linaweza kutushinda? Inahitajika pesa kiasi gani ndani ya miaka mitano kufanya hili,- piga hesabu. Umeme, kama bwawa la Julius Nyerere litaweza kuzalisha umeme kiasi kile, kwa nini usiweze kusambaa na kumfikia kila mwananchi; lakini sasa nasikia mipango ya upigaji, akina Makamba wanaisuka na kupoteza lengo; wanatafuta umeme wa Jua/Upepo, n.k., tena wa kulangua! Usiniambie siutaki huo, lakini hiyo kwa wakati huu ni kupoteza lengo tu na kutafuta upigaji kwenda mbele.
Kwani hawa raia (wengi wao wako vijijini) wakulima wa jembe la mkono, zaidi ya asilimia 60, wako huko vijijini, ndio unaowazungumzia kwa huduma ulizo orodhesha hapo wazipate?
Kiongozi anayetafuta maendeleo ya nchi kwa kwenda kuleta watu toka nje waje hapa kuwainua hawa wananchi kutokana na hali zao duni, unamwamini kweli?
Fanya kazi na hawa watu huko makazini kwao wachakalike, wapate haki ya juhudi zao, utaona nchi inabadilika haraka sana. Unakwenda kutafuta watu, tena toka nje waje wawakamue hawa hawa unaotaka wapate maji, umeme , n.k., itakuchukua muda gani kufika huko!