Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SIDNEY POITIER AMEFARIKI DUNIA LEO AKIWA NA MIAKA 94
Mwanangu yuko mbali na mimi wakati anakua hapa Dar es Salaam mara nyingi nikimuhadithia movies tulizokuwa tukizipenda wakati sisi wadogo na pia wale waigizaji maarufu nyakati zetu.
Tukipita mjini nikawa namuonyesha majumba ya senema tuliyokuwa tukienda.
Haya majumba ya senema wakati yeye anapata akili yalikuwa yote yamefungwa si majumba ya senema tena.
Majumba kama Odeon, Empire, Empress, Chox na Azania baadae ikabadilishwa jina na kuwa Cameo.
Hivi ndivyo alivyokuja kumjua Sidney Poitier na kufahamu ''Nickname'' yangu.
Leo mwanangu baada ya kupata taarifa ya kifo cha Sidney Poitier akanirushia taarifa iliyokuwa na video clips za senema zake maarufu.
Mwaka wa 1969 napita nje ya ofisi ya British Airways ghafla natupa jicho namuona Sidney Poitier na Harry Belafonte wamesimama nje ya ofisi hiyo ya BA.
Sikupoteza muda niliwafuata nikawasalimia na kuwaomba autograph na wote wakanipa.
Nilikuwa sina karatasi kwa hiyo nikatoa kitambulisho changu cha East African Cargo Handlinng Services (EACHS) ambacho kilikuwa kikubwa mfano wa kiganya cha mkono.
Nyuma ya kitambulisho hicho ndipo waliponiandikia majina yao.
Chini hapo nimeweka picha ya Sidney Poitier aliyonipatia Araf Sykes baada ya kukuta picha hiyo kwenye maktaba ya picha ya baba yake.
Nimependa kuiweka kama ilivyokuja kwangu.
Picha hiyo ilipigwa nyumbani kwa Ally Sykes alipowaalika Sidney Poitier na Harry Belafonte nyumbani kwake Magomeni Mikumi kwa chakula cha jioni.
Picha ya pili ni Ahmed Rashad akimpokea Sidney Poitier Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.