Tumbili wa mjini
JF-Expert Member
- Nov 2, 2024
- 1,125
- 2,233
Kama kichwa cha hapo imeandika, mimi sijawahi kudumu na mwanamke zaidi ya miezi sita nitaeleza kwa visa vya wanawake watatu.
Wa kwanza nilidumu nae kwa mwezi mmoja, wakaenda kwao likizo baada ya hapo mahusiano yakaisha akawa ana dharau hata nikimwita mara anisimamishe njiani. Kama siku moja aliniambia nisubiri akatoe hela kwa wakala nikasimama kama robo saa hajatokeza. Kila nikimsemesha hajibu message baadae kabisa akanijibu eti alikuwa bado anatoa hela, huyu demu alikuwa analeta dharau sana
Wa pili alikuwa akiishi Magomeni, basi sasa nikadumu nae kwa miezi kama mitatu. Mwanzoni alikuwa yupo na heshima ila baadae akaanza madharau mpaka kufikia kunitukana, nikaacha a nae.
Wa tatu ndio nilimpenda sanaaaa sijawahi kupenda demu kiasi hiki, nilijitahidi kadri niwezavyo tufurahi pamoja na heshima nilimpa kama zote mwanzo alikuwa na wivu nilichelewa kujibu message anakasirika, nilidumu nae almost 6 months tukaja kuachana kisa simjibu message nikajitetea yakaisha. Sasa miezi kama minne imepita nimesafiri hajawahi kuniulizia chochote nilivyo mwambia kama amezingua akaleta kelele nyingi kwamba simpendi namchezea tu, akasema tuachane kwakuwa sina future nae basi na mimi nikamuitikia na sijawahi kumtafuta tena, ila uliniumiza sana kuachana nae.
Wanawake wote hao na wengine wengi niliowahi kuachana nao sijawahi kuona hata mmoja akinisemesha kunijulia hali
Swali?
Kosa langu ni lipi. Au ni focus kwenye mambo ya maana kama Lusaka noti niachane na mademu daima?