Sielewi kwanini Bima ya Afya kwa wote inashindikana Tanzania!!

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Habarini,
Kwanini lakini kitu cha muhimu kama hiki hakitiliwi maanani?

Watu wanapanga kuandamana kwaajili ya masilahi ya wanasiasa badala ya maandamano kwaajili ya BIMA YA AFYA KWA WOTE kwani ndiyo shida ya Watanzania walio wengi.

Ni bora wapinzani mkawekeza kwenye matatizo ya wananchi siyo kwenue SIASA za maslahi
 
Kwa hiyo hilo la bima siyo la kisiasa? Ikiandamana kisa bima utaonekana umeandamana kwa mambo ya mziki? Au mambo ya dini?
 
Marekani wameshindwa kuwa na bima ya Afya kwa wote , Tanzania unadhani itawezekana?
 
Wasemaji wa awamu ya 6 Lucas Mwashambwa Tlaatlaah ChoiceVariable uzi unawahusu huu
gentleman,
hata kabla ya mpango wa bima ya afya kwa wote kukufikia wewe na wadau wengine wa JF,

ni muhimu sana wananchi wote kuzipa kipaumbele afya zao kwa kua na bima za afya za gharama za kawaida, kuliko kukimbilia kununua matoleo mapya ya iphones kwa gharama kubwa na itapendeza zaidi :1Head:
 
Mbona unakimbia mada hebu tuliza mihemko. Wananchi wanauliza BIMA za afya walizoahidiwa na ccm ziko wapi?
 
Gentleman,
kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 kuna viupaumbele vingi sana ndani yake, vinavyogusa maisha ya waTanzania wote moja kwa moja, ambavyo ni wazi vyote ni muhimu sana na vitatekelezwa kwa wakati muafaka ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani hiyo waliyoichagua waTanzania wenyewe oct.2025.

ni muhimu sana wadau wa JF na waTanzania wote,
kua wastahimilivu na wenye subra kwenye mambo hayo ambayo yako katika hatua mbalimbali za kutekelezwa na kutimizwa :1Head:
 
Tulishasema

Kwann haiwezekani , Kwa Tanzania ningumu mno Kwa sababu hatuzalishi vifaa tiba achana vitu kama miundombinu majengo na madaktari
 
Habarini,
Kwanini lakini kitu cha muhimu kama hiki hakitiliwi maanani?

Watu wanapanga kuandamana kwaajili ya masilahi ya wanasiasa badala ya maandamano kwaajili ya BIMA YA AFYA KWA WOTE kwani ndiyo shida ya Watanzania walio wengi.

Ni bora wapinzani mkawekeza kwenye matatizo ya wananchi siyo kwenue SIASA za maslahi
Hiyo bima kwa wote bora isiwepo maana utakuwa ni mradi tu wa kuongezea wahuni fedha na bado huduma nyingi utaambiwa ulipie hazipo kwenye bima maana tunaona hizi bima zilizopo sasa kwa watumishi wanao katwa fedha nyingi lakini huduma nyingi badi wanaingia mifukoni
 
Wanaochangia ni wangapi na wanaotakiwa kupata huduma ni wangapi?
 
CHIF Hii Inawekwa Tzs 1500/= Upate Panadol
 
Gentleman,
kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025-2030 kuna viupaumbele vingi sana ndani yake, vinavyogusa maisha ya waTanzania wote moja kwa moja, ambavyo ni wazi vyote ni muhimu sana na vitatekelezwa kwa wakati muafaka ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani hiyo waliyoichagua waTanzania wenyewe oct.2025.

ni muhimu sana wadau wa JF na waTanzania wote,
kua wastahimilivu na wenye subra kwenye mambo hayo ambayo yako katika hatua mbalimbali za kutekelezwa na kutimizwa :1Head:
UTAPELI
 
Back
Top Bottom