Kwa ujumla Wakristo na Waislam wa Tanzania, hawana ugomvi kabisa. Tofauti yao kubwa ni kuwa mwingine anaingia Kanisani, mwingine anaingia msikitini, zaidi ya hapo, hakuna tofauti yoyote. Kulikuwa na ujenzi wa kanisa jipya, nilishuhudia waislam wamekuja kuchangia, kwa sababu ya mahusiano mazuri pamoja na kusaidiana miongoni mwa wahusika.
Kinachotokea sasa ni kila alichokisema Mwalimu Nyerere kuwa mtu aliyefilisika kisiasa hujificha kwenye kivuli cha dini au kabila, yaani badala ya ya mtu kutafuta hoja zinazoweza kumfanya aungwe mkono, anataka aungwe mkono kwa sababu ni watu wa dini au kabila lake. Anataka watu wasiuone udhaifu wake bali waione dini au kabila lake, kisha waseme tumwunge mkono kwa sababu ni wa dini yetu au kabila letu.
Udhaifu wa Samia na Serikali yake ndiyo umetufikisha hapa. Anataka afunike uovu ule mkubwa wa mauaji alioufanya kwa hadaa ya udini, lakini kwa vyovyote hawezi kufanikiwa. Atawaokota hao mashekhe wanafiki wa BAKWATA na mawakala wao, lakini siyo waislam na wakristo wa kweli. Huko mtaani wakristo na waislam hawana matatizo kabisa.