Siendi Mkoani Ng'ooo!! Dar es salaam is the future! Mikoani ni didimizo la uchumi binafsi

Siendi Mkoani Ng'ooo!! Dar es salaam is the future! Mikoani ni didimizo la uchumi binafsi

Well i give you the benefit of the doubt!!!!!!!!! Fine! Okay! Mikoani KIDOGOOO kuna wabishi ila usisahau principle ya MAJORITY RULES MINORITY RIGHTS!!!!!!!!! Sasa je majority wa mkoani wanasimamia wapi?

Then km majority rules.....basi raia wangeongoza nchi..ila watu wachache sana ktk serikali wana rule, hata ktk uchumi kuna wachache sana wamjiweka pale juu...........hizi elimu za fasta huwapotosha sana watoto wa geti, wanaoendeshwa kwa story za kwenye birthday.Ndio maana yule dada wa south na akina wema sepetu huwa wanakuwa ktk mitandao ya kijamii wakionyesha hela na kujiita wachakarikaji.
 
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jamani HUU NI MTAZAMO WANGU BINAFSI LARA 1!! (Hii sio dini na mimi sio nabiii so sitegemei wote mseme AMINA kuitikia pasi kupinga hoja yangu! You may agree to disagree! Ila jamani tutunze staha na ustaarabu wetu! Tuwe wavumilivu na ubishi uwe wa hoja tu si kutukanana! Aksanteni.

BACK TO TOPIC

Naomba nieleweke sisemi mikoani ni kubaya ama hapafai kuishi all i am saying is the future is brighter in Daresalaam, kuliko mikoani. Kwa mambo mengi Jiji la Wazaramo limetishaaaa!!! Siropoki tu ama kuleta ushabiki nina grounds zangu za kutoa hii hoja binafsi, kwanini huning'oi mjini hata kwa greda!

1. Mkoani watu wamerizika ila Dsm chochote utakacho achieve WE BADO SANAAAAAAA! People are moving mountains. Mkoani mtu akiwa na nyumba 2, magari 2, anaheshimika si kitoto na anahesabika kati ya wenye uwezo. Ila mjini unaweza kuwa hata na commercial buildings 3 ila kwenye list hata hujanukia kuwamo! Kabisaaaa! So huku DSM haurelax, ni mpambano 24/7. Ofisini ukianza ujenzi wa tubanda twako, utasikia flani ana ghorofa 2, na amenza kujenga commercial! Unabakia Whaaaaaaaat? Kumbe mimi bado sanaa eeeh? Unakaza buti. Ukijikamua kupeleka mtoto IST, unasikia jirani yako kapeleka U.K au U.S Orange Country huko. WITH THE CITY IT IS NEVER ENOUGH!!! Ila mkoani watu wanakusifia unajiona umefikaaa, ukistuka ushazeeka. Kama unabisha jiulize ulivotoka jijini kwenda shamba watu uliowaacha wako wapi na wewe uko wapi?

2.Mji COMPETITION IS TOUGH! DEADLY! Ukiwa mkoani una C.P.A wewe bonge ya bosiii! Mkuu wa branch. Mjini C.P.A kama 30 hivi ofisi moja, na wenzio sio tu kuwa ni C.P.A bali hadi CIMA, CFA, ACCA, MBA, hadi Cerificate za law humo humo, degree 3! Yaani usifikiri na hivo vyeti wamepozi wanakungoja uwafikie? Nooooooo! Wanaongeza continuously, graduation baada ya graduation. Yaani hadi ushinde competition ulimi unaning'inia hoi bin taaban. Automatically unajikuta una aspirations kubwaa, sky is the limit, unajiburuzaje usiachwe nyuma? In the end unajikut na wewe ni somebody! Ila mkoani CPA kila mtu anakuita Bosi, basi na wewe unajiona bosi kweli kweli unabweteka. Matokea yake ulioanza nao unasikia wako UN! IMF! US EMBASY! Unabakia nilisomaga nao wale! You remain wondering how you became second rated in life since mligraduate wote UDSM, BCOM, Accounting 2004!!!!!! Tena wewe ulikuwa kipanga wao!

3. Life is damn expensive!!!!! Money is never enough! Akili inakuchemkaa utapataje hela zaidi! Comforts zinageuka luxury matokeo yake suala la kusaka pesa unaligeuza Vita vyako binafsi! Huku umeajiriwa, utawaza biashara, utawaza kila kitu ilimradi jiji lisikushinde. In the end you become a master wa kusaka mahela hadi unatoboa! I got a friend ni Monitoring and Evaluation Manager wa NGO kubwa tu, hapo hapo ana ki NGO chake, hapo hapo Analima kilimo mkoa huko, hapo hapo ana Kampuni, na juzi kapata U Country director NGO ingine anahama kule! Kote huko kupambana na bills na kuokota kila senti. We mkoani ukiwa kwenye NGO kubwa tu, hio pesa life ilivo affordable utapanga li mansion na kuwa mtu wa kuheshimika hadi basi!

4. Fursa hapa mjini ni nyingi mnoooo! Sijui hata nianzie wapi kwenye hili! I have a cousin, aligraduate 2010 ila pasi zake hazikuwa nzuri so akapewa hela na uncle mkopo wa 5m atafute ustaarabu, sio mtu na degree kula kulala tu. Akafungua ki pub tu local na fremu ya pembeni akawa anauza pombe reja reja wine, wisky na vingine. Mungu kambarikia the business is now BIG! Kalipa 5m za watu na naprofit ya laki 6 daily akitoa cost zote duka limekuwa la jumla sio rejareja tena. Na pub ameitanua imekuwa bar. Wala hatafuti kazi tena! Kazi gani utalipwa laki 6/day? Mjini ukiwa na ubongo kidogo tu, hakuna linaloshindikana.

5. Ukiwa mjini unakuwa na VISON KUBWA! BIG DREAMS! BIG AMBITIONS! BIG ASPIRATIONS! SKY IS THE LIMIT! Yaani people always look at the BIGGER PICTURE! Kwa jinsi mambo yanavoenda race automatically you think of next century like tomorrow! Dogo tu nilimuuliza ukiwa mkubwa utajenga nyumba? Akanijibu nani ajenge nyumba? sijengi nyumba najenga GHOROFA!!!!!! And he is like 8yrs! Small Boy Big thoughts!!!! (Zikiwa kubwa sanaa ndo wanauza sembe na meno ya tembo!) Jirani yangu alikuwa FN manager multinational moja, mshahara 4m na nini, akaacha baada ya miaka kadhaa tu! Kila mtu anamwambia kijana umebugi men! Kuresign ni blander kubwa uliyoifanya! Akawaambia No! Mi sikwenda pale like niwe nimeajiriwa pale like forever! Mpaka nizeeke! Mi nilienda kutafuta MTAJI! Baaaaaaaass! Nyie 3M mnaiona ya maana sanaa bt sio, kwa mwaka its approximately 36m, of wish i wanna make that per month or 2. Hio 36, ukitoa expenses na mda ninaoshinda ofisini, saving ni marginal sanaa! Siku hizi ana yard ya magari, analima huko mkoani, na ku import mavitu toka china! Ametajirika 20 times QUICKER, kuliko alivokuwa multinational. And he is only 34. HE SAW THE BIGGER PICTURE!!!!!!!!!!!!

Bottom line is kama unaweza rudi DSM ucheze na BIG BOYS in the CHAMPIONS LEAGUE!!! ILa kama imekubidi kukaa mkoani usiwaze kimkoa mkoa! THINK BIG ki darisalma darisalama! Ukijihisi umetoka kimaisha njoo town upimishane na uliowaacha ubavu! Itakusaidia kutokurizika na kubakia nyumaaa!

Having said that may i also stress that MAISHA POPOTE! WEWE TU NA AKILI YAKO! ni msemo wenye nguvu ila hufifizwa na mazingira na attitude ya watu waliokuzunguka!

Karibuni kwa HOJA ZENU!

du! e bwana e, kumbe na huku upo ee? I like this.....
 
Haha..kama ni kuchuma vyepesi ...ulikuwa na haja gani kusoma au kuhalalisha kwa vyeti?Wala si mabishano ila ni reasoning too?

Madada poa nao hujisikia sana kujiamini wanapojua lugha nyingi za wateja wao, au kuonekana wasomi ktk biashara zao,na mara nyingi huwaponda sana wenzio wanaoongea Lugh moja ya kimataifa.Waswahili wengi hukimbizana na vyeti ili wawe huru ponda wengine wanaofanikiwa bila kupitia hizo njia.......ni kua buse elimu..

Umeinvest 15yrs kupata vyeti na si elimu ya ku badili dunia inayokunguka...?Once mna exhaust mazingira waliyojenga wengine nchi itakuwa mbaya sana.

HAHAAAAAAA! MIND YOU IM BELOW 25, SO YOU CAN IMAGINE I WAS HOW OLD IF YOU MINUS THOSE 15YRS! Nilikuwa minor hata contract kuingia siruhusiwi so the best thing to do at that time ilikuwa kwenda shule! nA SIKWENDA COZ NAITEGEMEA SHULE INITOE KIMAISHA NOOO! Ilikuwa kufuta tu ujinga, kukua, kupata hadhi kwenye jamii kama msomi na kumfurahisha mzazi wangu Baaaaaaaaaass BT NOW ITS TIME FOR CHAMPIONS LEAGUE!

DARESALAAM NDO KILA KITU! HABARI NDO HIYO!!!!!!!!!!! Japo wote mkija huku mahindi na mchele tutapata wapi? LOLEST!
 
Hahahaaaaaaaaa! Afu mnakuwaga na ugwadu si mchezo!!!!!!!! Sie mission town tunaagiza shots za mawazo nyie miznga mi 3 mitatu, haswaa watu wa mgodini! Pombe shurti mchafue meza japo hamnywi zote kwa mpigo!


Umeona eeeennhhh!!
 
Hoja ya msingi ni Dar es Salaam mtu unafanya kazi gani na unaishi wapi? Na je, wenzako ni akina nani? Vinginevyo nawashauri vijana kwenda mikoa kuna fursa nyingi. Hapa Dar panafaa wenye mitaji mikubwa na kazi zenye nafasi ya kuiba.

Napingana na wewe! Uko wap katika level ya maisha sidhani kama inajalisha! Issue ni kuwa unataka kuwa wapi na utafanya nini kufika hapo unapopataka?

Watu wengi walizaliwa vijini sitimbi ndani ndani huko! BUT THEY HAD A BIGGER VISION KUWA SITIMBI SIO KITU! WAKADANDIA MALORI WAKAJA DSM UPEPO UNAPOVUMA, WAKA PERSVERE NA WAMETOKA KIMAISHA!!!!!! WENGINE WALIKOMAA NA VITABU KUJA VYUONI WAMENASA HAPA HAPA! ITS ALL ABOUT SURVIVAL OF THE FITTEST!!!!!!!!

IN LIFE WE ALL GET A FEW CHANCES, IF YOU DONT GRAB THOSE CHANCES BY THE BALLS YOU WILL ALWAYS WONDER HW YOU BECAME SECOND RATED IN LIFE!
 
Akili ya utafutaji pesa haina uhusiano na mahali ulipo. Kama uko gifted katika utafutaji popote utapiga kazi. Hii mentality ya Dsm ndo kila kitu haina mashiko.
 
Akili ya utafutaji pesa haina uhusiano na mahali ulipo. Kama uko gifted katika utafutaji popote utapiga kazi. Hii mentality ya Dsm ndo kila kitu haina mashiko.

Pole sana! Mbona mikoani hakuna vyumba vya kupamga vinavolipiwa 50000 kwa mwezi? Huku kwetu mpaka chumba cha buki5 unapata! Chezea Bongo wewe? Ukiwa Bongo mtaji!
 
Hoja ya msingi ni Dar es Salaam mtu unafanya kazi gani na unaishi wapi? Na je, wenzako ni akina nani? Vinginevyo nawashauri vijanakwenda mikoa kuna fursa nyingi. Hapa Dar panafaa wenye mitaji mikubwa na kazi zenye nafasi ya kuiba.

Kazi sipo Mkuu zenye nafasi za Kuiba hizo na Mimi mnipe? Haya tuelekeze hizo fursa zilizopo mikoani! Ni zipi hizo Mkuu? Kumbe wafanyakazi walio Dar wanaharufu ya Ufisadi? Ndo maana Dar Gari ni nyingi mno! Utakuta mtu mshahara wake ni laki3 na anafamilia. Na anakaa nyumba ya kupanga kwa mwezi analipa kodi laki3 na anamiliki Gari ya milioni15. Kumbe ufisadi serikalini tu kwa watumishi wengine unaitwa wizi! Kweli Dar ni kiboko!
 
kwani unadhani shida ni vyeti, au mengine unayodhani...shida ni kwamba elimu yako haikusaidii badili mazingira ili yawe favourable kwako na wengine.Ila ni kutumia walichobadili wengine.Pengine umenielewa.

Nature na survival ya binadamu ni kubadili mazingira yaweze msaidia, na elimu ni mojawapo ya tools ,muhimu.Naona elimu yako ni msaada wa kutumia walivyojenga wengine ndio maana unajitahidi sana kutuonyesha kuwa unavyo vyeti vya akuhalalisha wewe kuchagua mji wenye maendeleo waliyoleta wengine ili ukatumbue tena big.Sioni hata kwanini ulisoma km lengo ni kudandia waliyofanya wengine.Si ungejituma km wengine wanaoosha sura na kuuza sura tuu.

Siamini kuwa wasomi wa kibongo ni wa hovyo hivyo...wanasoma ili watumbue na si kuzalisha in abundant..ndio maana ma CCM yanasoma ili yapate uhalali wa kukaa palipo na vya kuiba hata km ni kuwalaza watanzania 100,000 + njaa.......

Kwa heri....ungezaliwa down town Manahatan ungekuja Africa?
mkuu mwaka huu nimesoma kitabu kimoja kinaitwa 'the tipping point" kuna chapter inaitwa the rule of few. inaelezea kwamba asilimia 80 ya kazi hufanywa na asilimia 20 tu ya watu!!. hivyo hivyo hata fursa na utajiri wa nchi yetu unaonwa na watu wa chache sana. kama mtu haoni inatakiwa kumuonea huruma sana. mtoa mada nae ni mtu wa kuonewa huruma. hebu muulize madini atachimba dar?, viwanda vya sukari atajenga dar?, kahawa atalima dar?, akitaka kuanzisha kiwanda cha kauri atajenga dar?, akitaka kulima chochote je atalima dar?, akitaka aanzishe steel industry siku moja aje kuwa kama mukeshi ambani ataanzisha dar na amesema hatoki?. tukubalieni tu kitu kuna wengine genes make up zao zinawaruhusu kuwa watumwa tu na kufanyia kazi wengine na ndio maana wanaangaika kukusanya mavyeti wakijua vitawalinda kwa ma master wao.
 
mkuu mwaka huu nimesoma kitabu kimoja kinaitwa 'the tipping point" kuna chapter inaitwa the rule of few. inaelezea kwamba asilimia 80 ya kazi hufanywa na asilimia 20 tu ya watu!!. hivyo hivyo hata fursa na utajiri wa nchi yetu unaonwa na watu wa chache sana. kama mtu haoni inatakiwa kumuonea huruma sana. mtoa mada nae ni mtu wa kuonewa huruma. hebu muulize madini atachimba dar?, viwanda vya sukari atajenga dar?, kahawa atalima dar?, akitaka kuanzisha kiwanda cha kauri atajenga dar?, akitaka kulima chochote je atalima dar?, akitaka aanzishe steel industry siku moja aje kuwa kama mukeshi ambani ataanzisha dar na amesema hatoki?. tukubalieni tu kitu kuna wengine genes make up zao zinawaruhusu kuwa watumwa tu na kufanyia kazi wengine na ndio maana wanaangaika kukusanya mavyeti wakijua vitawalinda kwa ma master wao.
Na hizi zote ulizosema ndipo kuna hela za wanaoweza inunua serikali yoyote duniani.....pamoja na wanasiasa wote jumlisha wapambe wao.
 
HAHAAAAAAA! MIND YOU IM BELOW 25, SO YOU CAN IMAGINE I WAS HOW OLD IF YOU MINUS THOSE 15YRS! Nilikuwa minor hata contract kuingia siruhusiwi so the best thing to do at that time ilikuwa kwenda shule! nA SIKWENDA COZ NAITEGEMEA SHULE INITOE KIMAISHA NOOO! Ilikuwa kufuta tu ujinga, kukua, kupata hadhi kwenye jamii kama msomi na kumfurahisha mzazi wangu Baaaaaaaaaass BT NOW ITS TIME FOR CHAMPIONS LEAGUE!

DARESALAAM NDO KILA KITU! HABARI NDO HIYO!!!!!!!!!!! Japo wote mkija huku mahindi na mchele tutapata wapi? LOLEST!

Hamna shobo....kwa huu mchanganyiko naona upo dunia yako.Nadhani ukibadilisha boyfriend utakuwa na fikra nyingine.


Sound like hakuna mahusiano ya shule na hiyo league.....kufta ujinga bado, kwani bado unadhani elimu ndio utu wako ndio hadhi yako....km ulikwenda wafurahisha wazazi i can imagine the kind of person you are.....hata hiyo hadhi sijui km umeipata, hata km ulidhani itakusaidia ongea point ktk waliozichanga na wasomi, jaribu fanya tafiti wanakuonaje km si irritating ......

wewe unadhani kila mtu mkoani analima na kila aliye dara halimi?Pengine unawaona wakiwshaoga na kupendeza kwa afya baadaya kufanya kizoezi kikubwa chenye kipato.
 
Napingana na wewe! Uko wap katika level ya maisha sidhani kama inajalisha! Issue ni kuwa unataka kuwa wapi na utafanya nini kufika hapo unapopataka?

Watu wengi walizaliwa vijini sitimbi ndani ndani huko! BUT THEY HAD A BIGGER VISION KUWA SITIMBI SIO KITU! WAKADANDIA MALORI WAKAJA DSM UPEPO UNAPOVUMA, WAKA PERSVERE NA WAMETOKA KIMAISHA!!!!!! WENGINE WALIKOMAA NA VITABU KUJA VYUONI WAMENASA HAPA HAPA! ITS ALL ABOUT SURVIVAL OF THE FITTEST!!!!!!!!

IN LIFE WE ALL GET A FEW CHANCES, IF YOU DONT GRAB THOSE CHANCES BY THE BALLS YOU WILL ALWAYS WONDER HW YOU BECAME SECOND RATED IN LIFE!

Lala 1, I also strongly disagree with you. Why limit yourself to Dar es Salaam alone? You must put your head where your pillow is. You Lala 1, the individual, your pillow is in Dar es Salaam. The likes of Kaunga her pillow is in Dodoma. Mohamed Mtoi his pillow is in Arusha. For an optimistic young man, life is everywhere. You made it very clear that some come people come here in search for education and they are stark. Why are they stark is because of the diseases I personally term "Dar es salaamosis" the very disease you are propagating. By the way Karibu Handeni kuna plot za madini. Ukifika nitafute
 
[/B]Btw im BEYOND PROUD OF THOSE CERTIFICATES CAUSE I EARNED EACH N EVERYONE OF THEM! I invested more than 15yrs in that quest! Anyways They are MY certificates and i am proud of them, think what you may!!!!!!

Hahahaha,,,,,,,my sister be very careful,change your perception unless you will end up building houses and buying cars saying you have prosper,,,,being rich is far more than what you think ila never be too proud of certificates what matters is to use your talents,gifts and principles towards success,,,now have been in dsm and if you want to start from the bottom you wont be a millionaire(tshs),,,trust me
 
mkuu mwaka huu nimesoma kitabu kimoja kinaitwa 'the tipping point" kuna chapter inaitwa the rule of few. inaelezea kwamba asilimia 80 ya kazi hufanywa na asilimia 20 tu ya watu!!. hivyo hivyo hata fursa na utajiri wa nchi yetu unaonwa na watu wa chache sana. kama mtu haoni inatakiwa kumuonea huruma sana. mtoa mada nae ni mtu wa kuonewa huruma. hebu muulize madini atachimba dar?, viwanda vya sukari atajenga dar?, kahawa atalima dar?, akitaka kuanzisha kiwanda cha kauri atajenga dar?, akitaka kulima chochote je atalima dar?, akitaka aanzishe steel industry siku moja aje kuwa kama mukeshi ambani ataanzisha dar na amesema hatoki?. tukubalieni tu kitu kuna wengine genes make up zao zinawaruhusu kuwa watumwa tu na kufanyia kazi wengine na ndio maana wanaangaika kukusanya mavyeti wakijua vitawalinda kwa ma master wao.

Red giant & nicholas u are real great dynamic thinker!kuleni gwala kokote mliko aisee.mkuu red author wa "the tipping point" ni nani?
 
Nilishawahi sikia jamaa wa kutosha wa makundi haya wakijisifu kuwa ni wachakarikali sana......wauaza unga, wauza mirundi, mapromoter wa sanaa,Machangu, na hata waganga wa kienyeji wanaokwenda Masqat, south Africa na sehemu nyingine kwa ufadhili wa wateja matajiri na baadae nao kufungua vijiwe huko..huwa nao wakirudi mitaani huwaita wengine wajinga.


Sipendi jua mbali na hiyo elimu ambayo kwa maelezo yako ni wazi haina kazi sana ktk maisha yako,zaidi ya kuwanyamazisha watu waliochoka sikia povu ktk mijadala kimjini(Kwako unaita elimu kwa ajili ya heshima), na ile dhan aya kufurahisha wazazi.Ila isijekuwa ni aina hii ya kazi ndio inakupa jeuri mjini..

Hata wema sepetu baada ya makasheshe kibao...aliibukia Dubai kufanya shopping ambayo magazeti ya udaku yaliishia shabadia bila hta mmoja kuuliza imekuweje ghafla huyu dada from miseries hadi kuwa mfujahela wa level hiyo?Ni kazi gania kafanya hadi wasanii wengine wasiweze, au hata wasomi wasiweze....watakuambia ni wachakarikaji mjini.
 
kabla hata ya kusoma uzi huu leo hii nimekata tiket yangu ya mkoani tu dar nataka ku-risk kazi yangu ya 2.5M gross. huu uzi umeniongezea nguvu na kuendelea mbele (risk & return) huezi amini ila ticket iko mfukoni seat ya mwisho kabisa gari ishajaa three days before. nimesimamisha kumalizia cpa yangu hakuna sehemu ya review class, mba imesimama na pia nagombana na wife kila siku sitaki kwenda home ambaye nae yuko mkoa mwingine kisa distance hata ka-fast jet ni ngumu kwa geografia ilivyo. najilipua dar ambapo pia nina getto tayari na vi-M kadhaa kama kumi hivi vimesahaurika sehemu fulani kama kianzio ajira zikigoma
 
Red giant & nicholas u are real great dynamic thinker!kuleni gwala kokote mliko aisee.mkuu red author wa "the tipping point" ni nani?
jamaa alieandika the tipping point anaitwa malcom gladwell ni jamaa anaheshimika sana kwa uandishi, kitabu chake kingine kinaitwa brink: the power of thinking without thinking
 
Kipenda roho ni dawa, lakini kila ugonjwa una dawa yake, hivyo basi ugonjwa wa lara 1 ni kuishi Dar si mikoani hilo limeeleweka kutokana na mada yake hii na sifa alizozimwaga hapa. Jambo moja la msingi tuelewe wengine zile vurugu, usumbufu na misururu mirefu unapokwenda kazini na kurejea nyumbani mtu unapoteza karibu masaa matano kwa siku hii kwa Lara 1 ni perfect life ever.

Zamani nilifikiri kama
lara 1, lakini leo nimeshaondokana na fikra hizo na kabisa mizunguko ya hapa na pale ndani ya hii global village (ulimwenguni) kwa anayeona Dar ndio perfect life namwacha na ipo siku atanifuata mkoani, pengine atajisikia amechelewa kwa vile aliyewahi ameshashika pazuri zaidi na kubaki kwenda pembezoni. Hata huko wenzetu waliotutangulia kwa maendeleo waishio mjini ni wa kiwango cha akina yakhe lakini walo nacho wamejichimia huko pembezoni kulikotulia na mjini wanaenda tu kuangalia vitegauchumi vyao na kisha kurejea makwao.

Waliotulia wanataka utulivu usio na usumbufu
Maisha ya Dar es Salaam ni usumbufu mtupu, na kwa wanaopendelea labda ni wale wa born Dar na kuona ubora wa maisha ni Dar tu kama walivyo wamarekani au wa ulaya wasioona pande nyingine za dunia zilivyo na kuona kwao ndio kila kitu wakati akikosa pay cheque wiki moja tu utamu wa maisha hupotea ghafla.

Mtu unahitaji kujali muda wako kwa kutopata usumbufu barabarani, lakini kwa Dar waenda kwa miguuu wanawahi kufika home kuliwa waendesha magari hii ndio raha anayotaka
lara 1. Ushindani wa kibiashara mitaa ya pale kariakoo karibu na makutano ya msimbazi na Uhuru maduka ya mobile phone za mchina zaidi yanakaribia elfu yakiuza bidhaa zilezile za mchini na kwa bei ileile, kuna wanaoshinda siku nzima bila kupata mteja haya ndiyo maisha ya mleta mada anayotaka. Kwa wanaotaka kiwanja gharama ya kukipata ni sawa na gharama ya kujenga nyumba. Ukitaka shamba basi umbali wa kulifikia ni sawa na safari ya kutoka makao ya mkoa kwenda wilayani haya ndiyo maisha ayapendayo lara 1. Ukitaka ama ukiwa na shida ya kufika mahala kwa vile lazima upitie downtown (city center) inabidi ujiulize na kutafakari kama kuna umuhimu au uahirishe hadi wakati mwingine kutokana na kufikiria usumbufu wa parking ya gari, au uwezekano wa kupata nafasi ya kudandia daladala, plus muda utakaopoteza na pengine usifanikiwe kwa sababu ya kuchelewa njiani.

Maisha ya walio wengi na kabisa waliotulia wanapenda kuishi sehemu iliyotulia na ambayo haimpi usumbufu wa kuingia na kutoka mjini, parking isiyo na usumbufu, kwenda mara moja kwenye shopping center na kupata anachohitaji, kuwa na watu anaofahamiana na kuishi nao kama wenzi wa maisha nk. Pia Nyumba yenye nafasi, bustani ya matunda, maua na mbogamboga viwanja vya midium size vinavyouzwa mikoani ambavyo ukubwa wake ni 35 X 35 or 35 X 65 hadi raha mtu unakuwa na michungwa, mapera, mapapai, michenza, maembe, mbogamboga, mahindi nk vinavyoizunguka nyumba yako na kubadilisha sura ya mahali kuonekana kama sayari ya pekee, kiwanja cha aina hiyo Dar nadra mno maana hicho kitagawanywa kwa makazi ya familia 4.

Watu wanapenda mikoani licha ya hoja za baadhi ya wadau hapa, pia ni sababu ya utulivu, kukwepa usumbufu usio hitajika na ambao unakwepeka kwa kuishi mikoani, rahisi kupata shamba linalofikika kirahisi kulifanya kijiranchi pakupumzika siku ukijisikia kuchoka na hewa ya mjini na huko unaburudika na hali ya hewa tulivu huku ukifurahia maisha ya viumbe ulivyovihifadhi kwanye ranchi yako kama mbuzi, ng'ombe, kuku hawa huleta burudani ya ajabu, pamo ukipitia sehemu kadhaa kuangalia shamba lako lilivyosheheni mazao mbalimbali kama paradiso yako na familia yako.

Kwa waliotembeatembea wengi watapenda sana maisha ya mikoani, ndio maana mimi nimeamua kibanda cha bongo bora nikipangishe tu nifaidi maisha ya mikoani ambako kuna fursa nyingi zisizo na uswahili mwingi, na unachokusudia huhitaji kutumia nguvu nyingi sana katika kuwafikia walengwa kwani wapo na wanajuliakana.

Sina maana ya kumgeuza nia mleta mada, ila tu lengo ni kujaribu kuonyesha upande mwingine wa sarafu ambao mleta mada hakuweza kutuletea ili tuweze kupima hoja yake kwa mapana na marefu wapi kunafaa na kuangalia advantages na disadvantages kwa pande zote.
 
Back
Top Bottom