Mkuu Joka Kuu umenikumbusha mbali!
Tulikuwa tunaishi Drive In Estate, mafleti next to Banyikwas, nyumba zimeungana na kutenganushwa na ukuta. Mzee wa Kihangaza, mke Mhangaza, alikuwa na mabinti 4 bomba sana!, Hope, Daines, Betty na Ngola na kaka yao mmoja Mzomu. Hapo ndipo vikao vilipo fanyikia!.
Kesi hiyo ilikuwa na similarities nyingi na Kesi ya Mauaji Mwanza, Mzee wangu, Andrew Mayalla ndio alikuwa RSO wa Mwanza, Jaji alikuwa Nassor Mzavas, DPP alikuwa William Sekule, Mzee wangu alitetewa na wakili Murtaza Lakha, ndie pekee alichomoka, wengine wote walikula mvua nyingi!.
Murtaza Lakha alinifanya nitamani kuwa wakili, by then ukikosa 1st class forget law, ndio nika-opt journalism, he was the best na mpaka sasa bado sijaona wakili yoyote Tanzania aliye vaa viatu vyake!.
P