Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
SIFA YA MZALIWA WA KWANZA; MWANAUME ANAWEZA KUWA NA WAZALIWA WAKWANZA HATA ISHIRINI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Sifa namba moja ya mzaliwa wa kwanza ni kuwa wakwanza kwa Mama aliyemzaa. Yaani kifungua mimba kwa Mama yake.
Mwanaume unapozaa na mwanamke asiye na mtoto na ambaye hajawahi kuwa na mtoto. Mtoto atakayezaliwa hapo ndiye mzaliwa wa kwanza. Hiyo weka kichwani.
Niiweke sawa hapa.
Ukioa wanawake watatu au wanne ambao hawajawahi kuwa na watoto. Kisha ukawapa mimba wakazaa watoto. Hao watoto wote ni wazaliwa wa kwanza kwako.
Kwa sababu uzaliwa wa kwanza unatoka kwa Mwanamke sio kwa mwanaume.
Kila mwanamke anazaa familia na boma lake linalojitegemea. Uzaliwa wa kwanza upo kwa mwanamke anayezaa.
Mzaliwa wa kwanza yeyote ni mtawala. Anaweza kupewa mamlaka ya kuongoza ukoo na himaya. Ndio maana kwa wanawake kuzaa mtoto wa kwanza wakiume kwao ni muhimu na advantage ila hawatakuambia.
Sifa ya pili ya mzaliwa wa kwanza ni, mzaliwa wa kwanza sharti awe mtoto wa kiume.
Mwanaume hapaswi kutanguliwa. Yeye ndiye kichwa. Yeye ndiye kiongozi. Yeye ndiye kifungua mimba.
Hapa tunazungumzia mambo ya kimwili na kimaumbile, na kiroho.
Ila sizungumzii masuala ya kihisia na Kiakili.
Kihisia na kiakili mzaliwa wa kwanza anaweza kuwa yeyote. Hata mtoto aliyezaliwa mwishoni kiakili au kihisia anaweza kuwa wakwanza.
Kwa sisi Watibeli, mzaliwa wa kwanza sharti awe wakwanza kuzaliwa kwa Mama yake. Kisha awe wakiume.
Ibrahim alikuwa na wazaliwa wakwanza wawili. Ishmael na Isaka. Lakini Isaka ndiye akampa madaraka.
Katika Familia ya Yakobo, alikuwa na wazaliwa wakwanza wanne, lakini akampa Yusufu mamlaka na kumuacha Reuben. Halikadhalina na Familia ya Daudi.
Familia ya Lameck ambapo Nuhu alipewa mamlaka licha ya kuwa alitoka kwa mke mdogo.
Nataka kusema nini?
Mwanaume unapoanzisha himaya na kuwa na wanawake wengi lazima ujue faida na hasara zake.
Ujue jinsi ya kuzitumia faida na hasara hizo.
Unapozaa na wanawake wengi. Tayari unatengeneza mazingira ya migogoro hasa ya kimamlaka.
Mtoto wako wa kwanza wa mwanamke huyu sio mkubwa kwa mtoto wa kwanza kwa mwanamke mwingine. Hilo weka akilini. Mpaka hapo huo ni mgogoro.
Pia, unapooa mwanamke mwenye watoto. Lazima ujue kwenye maisha yako huna mzaliwa wa kwanza. Kama watoto wako watakuwa wametanguliwa na watoto wa wengine.
Yaani umuoe mwanamke aliyezaa. Mtoto wako huwezi kumuita mzaliwa wa kwanza kwa mwanamke aliyekwisha kuzaa watoto. Hiyo power hana.
Mtoto wako ni mdogo kwa ndugu zake upande wa mkeo au mwanamke uliyezaa naye.
Fikiria mtoto unayemuona wakwanza kwako, kumbe ni wamwisho au watano kwa ndugu zake.
Fikiria kitu chako cha kwanza kwa wengine nichamwisho.
Nimemaliza! Wabishi hamtakosekana.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam