Sifa yetu mbaya kwenye utoaji wa Demokrasia na Haki za Raia ndio zitapunguza idadi ya watalii nchini

Sifa yetu mbaya kwenye utoaji wa Demokrasia na Haki za Raia ndio zitapunguza idadi ya watalii nchini

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Tunapoteza mabilioni kutembeza msafara wa rais nchi nzima kutangaza vivutio vyetu vya utalii!? Tumesahau kwamba utangazaji wa vivutio vya kitalii ni fani inayofanywa na wenye weledi mkubwa na pia watu wenye kukubalika duniani sio kwa madaraka yao bali kwa moral authority yao.

Ni vizuri rais Samia akajua kuwa wapo watanzania maarufu na wanaokubalika zaidi duniani kuliko yeye ambao wangeweza kuutangaza utalii wetu kwa uzuri zaidi na kwa gharama nafuu kabisa.

Tunapaswa kusafisha sifa mbaya tuliyojijengea miaka 5 hivi iliyopita: demokrasia mbovu na uvunjaji wa haki za raia vinafukuza watalii kwa maelfu!
 
Nasikia walikuwa wanakuja vizuri tu, tuliposema mdudu yupo, wakakata mguu.

Kumbe lengo ndo hili sasa, waache kuja, tutalii wenyewe kwa pesa za tozo
 
Kama taifa tunayo shida kubwa mahali,tunashindwa kuyaona mambo ya msingi ni yapi, tunaishia kuharibu badala ya kurekebisha mapungufu yetu, kiongozi wa nchi na mfumo mzima unaotakiwa kuona na kuelekeza na kurekebisha yale yasiyokuwa na manufaa, au yenye athari kwa taifa na watu wake, ni kama haupo au umezidiwa na wale wanaozingatia manufaa yaobinafsi au manufaa ya kundi la wachache, ama kwa kushauri vibaya, au kupotosha kwa ushauri unaolenga manufaa ya wachache na sii maslahi mapana ya taifa hili .

Kwenye siasa, uhuru, haki, uzingativu wa sheria na Katiba ya taifa letu ni kama tumelaaniwa kama taifa. Silaha inayotumiwa ikiwa ni kung'ang'ania Katiba iliyopo, kukandamiza wenye nia njema na taifa hili kwa kuwatumia polisi na mamlaka zingine za utoaji haki na usimamizi wa sheria mbalimbali, kwenye chaguzi, mamlaka za kiuchuguzi na zile zinazofanana na hizo.
 
Back
Top Bottom