Kama taifa tunayo shida kubwa mahali,tunashindwa kuyaona mambo ya msingi ni yapi, tunaishia kuharibu badala ya kurekebisha mapungufu yetu, kiongozi wa nchi na mfumo mzima unaotakiwa kuona na kuelekeza na kurekebisha yale yasiyokuwa na manufaa, au yenye athari kwa taifa na watu wake, ni kama haupo au umezidiwa na wale wanaozingatia manufaa yaobinafsi au manufaa ya kundi la wachache, ama kwa kushauri vibaya, au kupotosha kwa ushauri unaolenga manufaa ya wachache na sii maslahi mapana ya taifa hili .
Kwenye siasa, uhuru, haki, uzingativu wa sheria na Katiba ya taifa letu ni kama tumelaaniwa kama taifa. Silaha inayotumiwa ikiwa ni kung'ang'ania Katiba iliyopo, kukandamiza wenye nia njema na taifa hili kwa kuwatumia polisi na mamlaka zingine za utoaji haki na usimamizi wa sheria mbalimbali, kwenye chaguzi, mamlaka za kiuchuguzi na zile zinazofanana na hizo.