Sifa za Kiongozi Bora: Zitakusaidia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu

Sifa za Kiongozi Bora: Zitakusaidia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
9,327
Reaction score
5,206

Sifa za Kiongozi Bora: Zitakusaidia Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu​

___________________

1. Kiongozi bora ni mjuzi, siyo mjuaji. Mjuzi ni muelewa. Mjuaji ni mbabaishaji! Chenga!

2. Anaishi kwa maono na siyo maneno! Maono ni kuona kesho ukiwa leo! Maneno na hali ya kuwapotezea watu muda!

3. Anaishi kwa mipango thabiti, siyo mipango ya ghafla kama chafya! Mipango ya ghafla hufanywa na watafuta kiki!

4. Ni mtumishi wa watu siyo tishio la watu! Anajali utu kuliko vitu. Haogopwi, anaheshimika!

5. Yuko mbele katika kutafuta na nyuma katika kula. Anakula baada ya watu wake kushiba!

6. Anafundisha watu wake kuvua samaki na siyo kupokea samaki. Vya kupewa hulemaza akili!

7. Ni jasiri siyo jeuri! Ujasiri ni unyenyekevu. Unyenyekevu siyo kujikomba!

8. Anajiamini kwa sababu anajua kuna maisha baada ya uongozi. Hababaiki na cheo. Ukipata nafasi poa, akikosa sawa tu, hajisikii kufakufa!

9. Kiongozi bora hafanyi maamuzi magumu anafanya maamuzi sahihi. Maamuzi magumu ni kukomoana!

10. Kiongozi bora ana utulivu wa mwili na akili. Hakurupuki katika kutenda na kusema na kujibu!

11. Anaamini na kufanya maamuzi kwa tafiti na siyo hisia! Anaongozwa na Falsafa ya No research no right to speak na siyo umbea na majungu!

12. Anaona majibu katika kila changamoto na siyo changamoto kwa kila majibu!

13. Ni mkubwa kuliko changamoto za jamii. Linapotokea tatizo halalamiki na watu wake, wala hashangai na watu wake. Analimaliza na watu wake!

14. Ni muungwana siyo mshenzi! Mshenzi ni sawa na pembe la ng'ombe hata ukilifunika kwa kanga utalijua tu.

15. Ana masikio makubwa na mdomo mdogo. Anasikiliza sana na kuongea kidogo! Mungu alitupa mdomo mmoja na masikio mawili ili tusikie sana na kuongea kidogo.

16. Ni mbunifu siyo muigizaji. Anafanya kazi kuacha alama na siyo kuacha laana!

17. Anajipenda, hajipendelei. Kujipenda siyo kujipendelea! Chukua hii!

18. Anatumia kichwa kufikiri siyo tumbo! Tumbo hushawishi wizi!

19. Kiongozi bora siyo umri bali hekima na maarifa! Maarifa ni nini unajua, hekima ni wakati gani useme unachokijua!

20. Ni kioo cha jamii siyo kituko cha jamii! Kituko ni kituko tu. Unajilimbikizia mali za umma ukifa unaziacha. Wewe ni kituko!
 
Back
Top Bottom