Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
1. Wanajali zana pesa kuliko kumtumikia Mungu.
2. Wanaamini Yesu sio Mungu.
3. WANA MADHABAHU ZAO, hata maombi wanaomba kwa madhabahu ya mtumishi huo, sio kwa Jina la Yesu, wanaamini madhabahu yao ina nguvu, kumbe Nguvu zetu zinapaswa zitokane na Roho.
4. Injili zao muda mwingi ni za miujiza tu, kujisifia kuwa wana upako, hawahubiri wokovu, toba, utakatifu na uongozi wa Roho. Hii haimaanishi Mungu hawezi fanya miujiza, wanaifanya, ila wao wanaifanya ya shetani, hawana Mungu. Mungu anataka kwanza roho yako, mengine utazidishiwa.
5. Akiwa anahubiri, ANAKUWA NA LICHAWA PEMBENI la kupromote kurudia kile alichotamka, ili kumpa mori na kuhamasisha waumini, hii ni kwasababu hawana Roho Mtakatifu wa kugusa mioyo ya watu, wanatumia nguvu za mwili kuaminisha waumini kile wanachohubiri.
6. Wanapenda sana KUSIFIWA NA WAUMNINI wao kuliko hata kumsifia Mungu, wanapenda kutangazwa sana wao kuliko hata kumtangaza Mungu.
7. WANA KIBURI CHA PESA utafikiri za kwao kumbe ni zile zile sadaka mnatoa anajifanya za kwake na yeye ni tajiri, wanapenda sana kusifia serikali, kwasababu wanaiogopa.
8. WANATEMBEA NA MABODIGADI hata mahali pasipo na ulazima, ila waumini wanaowahubiria hawana ulinzi wowote.
9. WANAPENDA ANASA, muda mwingi wapo mitandaoni kurusha picha walivyovaa vizuri na kuwatamkia watu ahadi za mambo mema, badala ya kutangaza injili iletayo wokovu wa roho.
10. WANACHANGANYA BIASHARA NA INJILI. Huwezi kutumikia mabwana wawili, never.
11. Wanapinga Nguvu za Mungu, kwa maana ya ROHO MTAKATIFU, ujazo wa Roho na kuomba kwa Roho. Hutakuja kuwaona wanahubiri ujazo wa Roho, ni kwasababu hawanaye.
12. WANAUJENGA ZAIDI MWILI KULIKO ROHO. Majority ni masharobaro, hata hujui wanamtafuta Mungu maombi na kufunga saa ngapi. Hatusemi mtu awe mchafu, ila unashangaa wao muda wote wamevaa kisharobaro, wanajichubua, wanaujali mwili zaidi kuliko hata roho zao.
13. MAHUBIRI YAO MAKAVUUU HATA KAMA UTAONA KUNA MIUJIZA. Ni kwasababu hawana Roho Mtakatifu, ila roho mchafu. Hiyo miujiza jua ni ya shetani, shetani naye hufanya miujiza ili kulaghai.
14. WANAVAA NGOZI YA KONDOO KUJIFANYA NI WATAKATIFU ILI WAWAPATE WENGI, lakini kumbe ni mbwa mwitu walaluao. Mabinti wengi wana siri nzito sana na hawa manabii wa uongo wa kisasa" Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali." (Mathayo 7:15)
15. Wapo kwa ajili ya kuwadanganya watu wasimwabudu Mungu wa kweli." Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi."(Mathayo 24:4-5).
16. WANAFANYA MIUJIZA KWA NJIA ZISIZO ZA KI MUNGU ili waweze kuwapoteza watu. " Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule."(Mathayo 24:24).
17. WANAMWABUDU, WANAMTANGAZA NA KUFANYA KAZI ZA MPINGA KRISTO. " Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho."(1Yohana 2:18)
18. Hawamkubali Yesu hata kama wanajionyesha kuwa wanamwamini lakini kazi zao siyo za Kikristo kwa hiyo hawana Mungu ndani yao. " Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana.
19. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia." (1Yohana 2:22-23)
20. Kazi zao hazitokani na Mungu. " Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani." (1Yohana 4:1).
21. MAFUNDISHO YAO NI YA UONGO. " Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia." (2Petro 2:1).
22. UNABII WAO NI KWA MTAZAMO WAO NA MAAGIZO KUTOKA KUZIMU. " Ndipo BWANA akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao." (Yeremia 14:14).
23. Wengi wanaigiza na kulitaja jina la Bwana visivyo katika unabii wao na miujiza yao ili watu wajue kuwa wanatumiwa na kumbe siyo kweli. " Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?" (Mathayo 7:22).