Seneta Edwin Sifuna Azindua The Equitable Party, Atangaza Kuingia Kwenye Kinyang’anyiro cha Urais 2027

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Seneta wa Kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna amezindua rasmi The Equitable Party (TEP), akichukua uongozi wa chama hicho na kutangazwa kuwa mbeba bendera wake wa Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Lakini TEP si chama kilichoanzishwa leo.

Dkt. Gilbert Marava Shanga, Mkenya anayeishi Marekani, ndiye aliyeanzisha na kusajili chama hicho mwaka 2022 pamoja na washirika wake.

Katika hafla rasmi iliyofanyika Sarova Stanley Nairobi, Shanga pamoja na Waanzilishi wengine waliongoza mchakato wa mabadiliko ya uongozi, ambapo waliamua kujiondoa na kumkabidhi Sifuna uongozi wa chama. Hatua hiyo sasa imemweka Sifuna rasmi kwenye usukani wa TEP, huku chama kikimtangaza kuwa Mgombea wake wa urais 2027.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi kadhaa wa kisiasa, akiwemo Gavana wa Siaya James Orengo, Gavana wa Transzoia George Natembeya, Maseneta Godfrey Osotsi, Richard Onyonka na Boni Khalwale, pamoja na Wabunge akiwemo Babu Owino na Caroli Omondi.

Lakini hapa ndipo Wananchi wengi wamebaki na maswali. Je, Linda Mwananchi iko wapi au imeenda wapi? Imetokomea?

Siku chache tu zilizopita, Linda Mwananchi Movement ilipata ushindi katika mzozo wake na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), na jina hilo likahifadhiwa kwa muda wa siku 90. Hata hivyo, kuhifadhi jina hakumaanishi kwamba tayari ni chama kilichosajiliwa kikamilifu.

Ikumbukwe mnamo September 27, 2026 Viongozi wa Linda Mwananchi walimtangaza Sifuna kama mgombea wao wa urais 2027, wakisema wangetangaza chama atakachotumia katika uchaguzi mwanzoni mwa Oktoba.

Sasa, badala ya kusubiri mchakato wa Linda Mwananchi kukamilika, Sifuna ameibuka na The Equitable Party kama chombo chake cha kisiasa. Hii pia inakuja wakati wanasiasa kadhaa wakitafuta vyama vyao wenyewe au kuimarisha vyama vilivyopo kabla ya uchaguzi wa 2027. Fahamu kwamba vyama vidogo vinazidi kuwa muhimu katika mazungumzo ya miungano, huku wanasiasa wakivitumia kama majukwaa ya kujadiliana kuhusu nafasi, ushawishi na miungano.

Kwa hiyo, uzinduzi wa TEP si tu kuhusu jina jipya la chama. Sifuna sasa ana chombo rasmi kinachotajwa kuwa kitakachobeba azma yake ya kuwania urais, huku maswali yakibaki kuhusu nafasi ya Linda Mwananchi na uhusiano wake na mpango huu mpya.

Na kwa kuwa James Orengo, George Natembeya, Babu Owino na viongozi wengine wameonekana kwenye uzinduzi, swali lingine litakalofuatiliwa ni kama TEP itabaki kuwa chama cha Sifuna pekee au itakuwa sehemu ya mpangilio mpana wa kisiasa kuelekea 2027.

Kwa sasa, jambo moja liko wazi: Sifuna ametoka kwenye harakati za kujenga “brand” ya Linda Mwananchi na sasa ameweka chama mezani.

Swali ni: Linda Mwananchi sasa itabaki kama vuguvugu tu, au bado itaunganishwa na safari hii ya The Equitable Party(TEP)?
 
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amezindua rasmi The Equitable Party (TEP), chama atakachotumia kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Uzinduzi huo ulifanyika jijini Nairobi Jumapili, Oktoba 4, 2026, huku Sifuna akitajwa kuwa kiongozi mpya wa chama hicho na mgombea wake wa urais.

Kiongozi wa awali wa TEP, Gilbert Marava, alisema chama hicho kimeamua kurekebisha muundo wake wa uongozi ili kumpa Sifuna na washirika wake nafasi ya kujiunga nacho na kuendeleza safari yao ya kisiasa.
Hatua hiyo inampa Sifuna jukwaa rasmi la kisiasa kupitia chama hicho anapojiandaa kuwania urais mwaka ujao.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi kadhaa wanaohusishwa na vuguvugu la Linda Mwananchi, wakiwemo Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Siaya James Orengo na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya.
The Equitable Party, yenye kaulimbiu ya “Tusawazishe,” sasa inaingia katika maandalizi ya uchaguzi wa 2027 huku Sifuna na washirika wake wakitafuta kuimarisha uungwaji mkono wao kote nchini.
Hatua hii inaashiria mwanzo wa awamu mpya katika safari ya kisiasa ya Sifuna, ambaye sasa anajipanga kushindana na viongozi wengine watakaowania urais mwaka 2027.
 
ok.🐒
 
Wangapi wapo na sifuna weka mikono kwa juu
 
View attachment 3683600Seneta wa Kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna amezindua rasmi The Equitable Party (TEP), akichukua uongozi wa chama hicho na kutangazwa kuwa mbeba bendera wake wa Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Lakini TEP si chama kilichoanzishwa leo.

Dkt. Gilbert Marava Shanga, Mkenya anayeishi Marekani, ndiye aliyeanzisha na kusajili chama hicho mwaka 2022 pamoja na washirika wake.

Katika hafla rasmi iliyofanyika Sarova Stanley Nairobi, Shanga pamoja na Waanzilishi wengine waliongoza mchakato wa mabadiliko ya uongozi, ambapo waliamua kujiondoa na kumkabidhi Sifuna uongozi wa chama. Hatua hiyo sasa imemweka Sifuna rasmi kwenye usukani wa TEP, huku chama kikimtangaza kuwa Mgombea wake wa urais 2027.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi kadhaa wa kisiasa, akiwemo Gavana wa Siaya James Orengo, Gavana wa Transzoia George Natembeya, Maseneta Godfrey Osotsi, Richard Onyonka na Boni Khalwale, pamoja na Wabunge akiwemo Babu Owino na Caroli Omondi.

Lakini hapa ndipo Wananchi wengi wamebaki na maswali. Je, Linda Mwananchi iko wapi au imeenda wapi? Imetokomea?

Siku chache tu zilizopita, Linda Mwananchi Movement ilipata ushindi katika mzozo wake na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), na jina hilo likahifadhiwa kwa muda wa siku 90. Hata hivyo, kuhifadhi jina hakumaanishi kwamba tayari ni chama kilichosajiliwa kikamilifu.

Ikumbukwe mnamo September 27, 2026 Viongozi wa Linda Mwananchi walimtangaza Sifuna kama mgombea wao wa urais 2027, wakisema wangetangaza chama atakachotumia katika uchaguzi mwanzoni mwa Oktoba.

Sasa, badala ya kusubiri mchakato wa Linda Mwananchi kukamilika, Sifuna ameibuka na The Equitable Party kama chombo chake cha kisiasa. Hii pia inakuja wakati wanasiasa kadhaa wakitafuta vyama vyao wenyewe au kuimarisha vyama vilivyopo kabla ya uchaguzi wa 2027. Fahamu kwamba vyama vidogo vinazidi kuwa muhimu katika mazungumzo ya miungano, huku wanasiasa wakivitumia kama majukwaa ya kujadiliana kuhusu nafasi, ushawishi na miungano.

Kwa hiyo, uzinduzi wa TEP si tu kuhusu jina jipya la chama. Sifuna sasa ana chombo rasmi kinachotajwa kuwa kitakachobeba azma yake ya kuwania urais, huku maswali yakibaki kuhusu nafasi ya Linda Mwananchi na uhusiano wake na mpango huu mpya.

Na kwa kuwa James Orengo, George Natembeya, Babu Owino na viongozi wengine wameonekana kwenye uzinduzi, swali lingine litakalofuatiliwa ni kama TEP itabaki kuwa chama cha Sifuna pekee au itakuwa sehemu ya mpangilio mpana wa kisiasa kuelekea 2027.

Kwa sasa, jambo moja liko wazi: Sifuna ametoka kwenye harakati za kujenga “brand” ya Linda Mwananchi na sasa ameweka chama mezani.

Swali ni: Linda Mwananchi sasa itabaki kama vuguvugu tu, au bado itaunganishwa na safari hii ya The Equitable Party(TEP)?
TEP itabadiishwa jina kuwa Linda Mwananchi Movement (LMM)
 
Uzinduzi wa Linda Mwananchi wajikite kuelezea sera za chama na wapange safu za viongozi ngazi zote waachane na mambo ya kumsema kasongo
 
Back
Top Bottom