PostGE2025 Sigrada: Watu wanakufa kwa mawazo, kesi haziishi mahakamani

PostGE2025 Sigrada: Watu wanakufa kwa mawazo, kesi haziishi mahakamani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe (CHAUMMA) Sigrada Mligo ametoa wito kwa Serikali kuongeza watendaji wa Mahakama akiwemo Hakimu wa Mahakama ya ardhi, ili kupunguza vifo vya Wananchi kwa kukosa haki kutokana na kesi zao kukaa muda mrefu Mahakamani.

Sigrada ameeleza hayo jana, Desemba 11, 2025 wakati akizungumza mambo mbalimbali juu ya maendeleo ya Mkoa wa Njombe, katika kikao kazi cha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka pamoja na Madiwani, CMT na viongozi wote wa taasisi na sekta binafsi za Mkoa huo.

"Mkoa mzima wa Njombe tuna Hakimu mmoja wa Mahakama ya ardhi ambaye anazunguka Wilaya zote kwa hiyo kesi nyingi, zinacheleweshwa. Inafika mahali Mzee amehangaika na kesi Miaka 10 na watu wanakufa kwa 'stress', kesi haiishi kila siku yeye ni kuhudhuria Mahakamani", amesema Sigrada.

Aidha, Sigrada amesema kuna kila sababu pia ya kurekebisha ili kila Wilaya iweze kuwa na Mwenyekiti wa Baraza Wilaya ambaye atakuwa Hakimu, ili kupunguza kucheleweshwa kwa kesi hususani za ardhi ambazo zipo kwa kiasi kikubwa Mkoani Njombe.


 
Mambo ya Haki hayapaswi kufanyiwa mizaha,Mahakama kuwa na mahakimu wachache, Hospital kuwa na madaktari wachache,ni kuwanyima Binadamu Haki ya msingi sana!
 
Kwa tulipo fikia hatuna mahakama ya kuaminika mpaka sasa ni bora tukamalizana na kamati ya wazee mtaani kwetu.
 
Nimemsikiliza kwa masikio yangu mawili lakini sijamuelewa
 
Ipo bajeti ya kununua latest luxurious vehicles ila sio kuajiri mahakimu wa kutoa haki kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom