Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Nataka niongee kama mwananchi mkazi wa jimbo la KAWE bila kuingiza chembe hata moja ya itikadi au kugusa maslahi ya mtu binafsi. Nataka nizungumze ukweli mtupu kulingana na matendo ya huyu bwana siku zote.
JE, GWAJIMA ANAWEZA KULETA UPENDO NA AMANI KAWE?
Naomba nisiwe mnafki niuseme tu ukweli, huyu bwana amesikika wazi wazi kabisa akionesha chuki dhidi ya viongozi imani ziingine tena kwa kutamka wazi wazi na jamii inasikia. Vipi katika jimbo la KAWE wale wasiokua wa imani yake watampokeaje ikiwa amewajengea chuki ya muda mrefu? Je, hata kama yeye ana pesa, ataweza kuwanunua watu kinafki kupuuza uchungu wao na hasira dhidi yake na kwa matendo yake?
JE,GWAJIMA ATAWAPENDA WASIOKUA WATU WA KABILA LAKE? SIYO MBAGUZI WA KIKABILA?
Huyu bwana kuna wakati ilipita audio Clip katika mitandao ya kijamii akihamasisha watu wa kabila lake kuungana na kutengeneza kundi lenye nguvu kwa ajili ya kuwashughulikia wale wanaompinga aliyeko madarakani. Je, KAWE hakuna wanaompinga aliyeko madarakani? Akiwa mbunge KAWE kuna atakayesalia atakayekuwa siyo wa kabila la Gwajima?
GWAJIMA ALISEMA YEYE KUA MWANASIASA NI KAZI YA CHINI SANA, SASA ANATAKA NINI?
Huyu bwana akihutubia waumini wake alisikika kwa ulimi wake kua yeye hawezi kua mwanasiasa kwa vile ni kazi ya chini sana kwake, alionekana akiidhalilisha na kuishusha sana kazi ya siasa, sasa anaitaka ya nini? Kwanini asiwaachie wanaoipenda kazi hii yeye anaitaka ya nini?
CCM KWANINI MSINGEWEKA MTU MWINGINE KAWE?
Katika kitu ambacho CCM kimejidhalilisha sana ni kuweka mtu ambaye tunajua kabisa ameichafua jamii na hasafishiki , huenda wamefanya pasipo kujua na wanataka chama chao kiendelee kukataliwa. Najua walichokitaka zaidi ni ile nguvu kubwa ya pesa wakidhani atazitumia kummaliza Mdee kisiasa. Hili linaweza kufanikiwa au lisifanikiwe kwa sababu huyu mtu hana rafiki si kwenye jamii, siyo kwa imani ziingine wala kwenye siasa. Haya maneno anayozungumza ni ya mdomoni mwake tu ila tunajua moyo wake umejawa na kitu gani