GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
“Kikubwa kilichotuleta Arusha ni mechi ya Ligi Kuu dhidi ya KMC, mchezo ambao utachezwa tarehe 25 majira ya saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.”
“Tangu nimekuwa msemaji wa timu yenu timu haijawahi kuja Arusha hivyo nikaona hii ni nafasi nzuri ya kuja tuonane. Nimefurahi kwa mapokezi mazuri na hii inaonyesha Wanasimba wana imani na timu yao. Tumeileta mechi Arusha kwa kutambua thamani na mchango wa Wanaarusha kuipambania timu yao.”
“Mechi ilikuwa imeshapangiwa uwanja, na kutoka uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na kambini kwetu ni dakika mbili lakini tukasema tuipeleke Arusha wakaione timu yao. Mara ya mwisho Arusha kuiona Simba ilikuwa ni Novemba 22, 2020 tulicheza na Coastal Union na kuwafunga bao 7-0.”
“Tumewaletea Wanasimba timu yao wafurahie kuiona. Sababu nyingine ni umuhimu wa mchezo wenyewe, wote mnafahamu tupo kwenye vita kubwa ya kupambania kwenda Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Mechi ngumu kama hizi lazima upeleke kwa watu wagumu wagumu, baada ya tathmini watu wagumu wanapatikana wapi, tukasema tupeleke Arusha.”
“Mchezo wa Jumamosi tunahitaji ushindi, hatuna option nyingine, tena ushindi mkubwa.”
“Wanasimba wa Arusha ni watu wa kipekee, nusu na robo ya mkoa huu ni mashabiki wa Simba. Kwahiyo tumekuja nyumbani, tunaamini hapa nyumbani Arusha tutapata tunachokitaka. Mnyama kwa mapenzi yake Mungu na juhudi za Wanaarusha, Mnyama anakwenda kutakata Mei 25. Kuleta timu hapa sio jambo la bahati mbaya.”
“Wanasimba wa Arusha mna kazi kubwa ya kuhakikisha Simba inakwenda Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Msimu ujao tunahitaji kuongeza alama za CAF, na njia pekee ni kushikiri Ligi ya Mabingwa Afrika sababu ndio michuano yenye pointi nyingi.”
“Nafasi bado ipo wazi ya kwenda Ligi ya Mabingwa msimu ujao lakini lazima tuambiane ukweli nafasi hiyo ni ngumu. Sisi kwa ukongwe wetu tukisimama imara Mnyama atapata nafasi.”- Ahmed Ally
Chanzo: Simba Sports Club
Mlikuwa wapi kuipambania Timu iwe Bingwa NBC na mnahangaika sasa ili ishike nafasi ya Pili na mje mjivunie nayo?