Siipendi CCM, lakini nawakumbusha wanaharakati wa Twitter kuwa huwezi kuua muziki mzuri, kujaribu kumshusha Diamond Platnumz ni uzuzu

CreativityCode

Senior Member
Joined
Aug 8, 2020
Posts
158
Reaction score
653
Diamond Platnumz ni mwanamziki mkubwa duniani,

Niko Ulaya na nimeshuhudia popote panapopigwa muziki wa afropop basi ni Nigeria, South Africa, DRC na Tanzania, nikisema Tanzania basi ni muziki wa Diamond Platnumz au kundi zima la WASAFI.

Mwaka 2017 nilikuwa Nairobi na kwenda club ambapo nilishuhudia karibu 90% ya muziki uliokuwa unapigwa basi ulikuwa ni wa Diamond ama msanii wa kundi lake, wakizidi sana walikuwa wanapiga muziki wa Nevy Kenzo "kamatia chini".

Ni akili iliyojaa matope tu kujaribu kuzuia nyota wa pop wa Tanzania Diamond Platnumz eti asishinde tuzo za BET2021 eti kwa sababu aliiunga mkono CCM kwenye uchaguzi wa 2020.

Huyu kijana nyota licha ya kwamba ana kipaji ni mtu mwenye juhudi zisizo na mfano hasa ukichukulia kwamba anatoka nchi iliyojaa vijana wavivu wa kufikiri na wasio na juhudi ya kutafuta mali.

Diamond Platnumz ameajiri vijana wengi sana na hivyo kuboresha maisha ya watanzania wengi bila ya kujali itikadi zao.

Diamond ni mfanya biashara hivyo hachagui afanye kazi na nani, hata siku CHADEMA wakija na pesa ndefu kwa nini asimuimbie Mwenyekiti Mbowe, kamanda wetu asiyetetereka?

ACHENI WIVU WA KIJINGA MUUNGENI MKONO KIJANA, LAKINI PIA MJUE KWAMBA SIYO KILA CHADEMA BASI ANAKUBALIANA NA NYIE, NA KWAMBA KILA ASIYEKUBALIANA NANYI BASI NI MATAGA.

CC: Martin M, Maria Sarungi, Kigogo et al mnazingua. Nilijua mna akili kumbe hakuna kitu.
 
Kwan hao activists madai yao ya msingi ni nn? Wana hoja yoyote? Maana hata suala la yanga na simba hakunaga utanzania. Mi nadhani kama ana vigezo atapata tuzo hata mtu akimsagia kunguni, kama hana vigezo asonge mbele.
Vigezo vyote vipo, zaidi mashabiki wengi wa Diamond wako Afrika yote wakiongozwa na Kenya
 
Alikemea maovu ya Serikali ya Nigeria lakini akaamua kukaa kimya kuhusu maovu ya Serikali ya Tanzania kwa sababu tu ni MNUFAIKA. AJIONGEZE imekula kwake yuko busy kusaka kura nchi nyingine za Africa. Litakuwa fundisho kubwa kwake hata kama atashinda kwamba kama anaweza kukemea yanayojiri Nigeria basi anaweza kabisa kukemea yanayojiri Tanzania pia.
 
Ila Kigogo na ndugu zake wamekoga matusi kwa hivi vitoto vinyoa viduku na visichana vipaka pods hatari, Nafikiri walihisi huko nako Raisi wao ni kama kwenye Siasa,kumbe kuna Raisi wao huko na hawanaga time na siasa kiviiiiile kama huku siasa za serikali.

Kule kuna kambi za upinzani kimuziki,

WCB vs KONDE BOY vs ALI KIBA.

Na Hawa wote walilipwa na CCM kwa ajili ya kampeni.

Haya waache wayakoge matusi huko maana dishi limepoteza direction
 
Ungejaribu na wewe,mbona unakemea humu JF na hujitokezi?
Leta ID yako kamili na jitokeze wazi kukemea mzee acha umama
 
Acha ujinga wewe! Kwani unadhani Maxence melo alikuwa mpumbavu kuruhusu watu watumie FAKE ID? Mbona wewe hutumii jina lako la kweli!!! Acha kudharau akina mama wewe! Bila mama yako leo hii usingekuwepo hapa duniani.
Ungejaribu na wewe,mbona unakemea humu JF na hujitokezi?
Leta ID yako kamili na jitokeze wazi kukemea mzee acha umama
 
Unauhakika kufanya hivyo ni uzuzu,yaweza kuwa kunyamaza ndio uzuzu zaidi.
 
Acheni kumpaisha huyo mpuuzi wenu ,eti mwanamuziki mkubwa dunia wtf?? Hamonaiz alienda naija alishangaa kwamba jamaa yenu hapigwi kabisa tofauti na wanavyojitapa.

Kama yeye alihamasisha kwenye majukwaa wasiwapigie kura wanaharakati basi na yeye zamu yake wacha wanaharakati wahamasishe na yeye asipigiw kura..UBAYA UBAYA TU.
 
Anapenda sifa sana huyo, yuko fake fake ndo maana hata mimi simkubali.. mtu anajisifia ana hela kuzidi wanigeria kumbe hana, anatuonaje sisi kutudangamya!
 
Acha ujinga wewe! Kwani unadhani Maxence melo alikuwa mpumbavu kuruhusu watu watumie FAKE ID? Mbona wewe hutumii jina lako la kweli!!! Acha kudharau akina mama wewe! Bila mama yako leo hii usingekuwepo hapa duniani.
Ndo upumbavu tunaosema kwenu nyumbu.
Diamond anayejulikana unataka aisemee vibaya serikali ila wewe unataka uisemee vibaya serikali huku umejificha(Keyboard worries).

Jinga kabisa,we kama unajiamini unajificha nn usijulikane
 
Kwa hyo harmonise we una upopoma wako ukamuamini kabisa,pumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…