Mimi ni mstaafu Serikalini. Ni mmojawapo wa wastaafu tuliohamisishwa kujiunga na Benki ya Posta, nikahamasika kwelikweli hata nikahama Benki ya NMB. Jambo mojawapo lililonivutia kuhamia Benki ya Posta ni utaratibu mzuri wa mikopo kwa wastaafu; ilionekana kuwa na unafuu mkubwa ikilinganishwa na Benki ya NMB.
Sasa, nimekumbana na jambo limenichanganya.
Tarehe 12/04/2019 nilikopeshwa na Benki ya Posta 10.5m/= kwa makubaliano ya kuwa nalipa deni hilo kwa kukatwa kutoka pensheni yangu ya mwezi 285,177.53 kwa muda wa miaka 2.9.
Nimepata dharura nikaenda Benki kuhuisha mkopo, kwamba, niangaliziwe deni lililobaki ili likatwe kutokana pesa nitakazokopeshwa tena na hesabu zikawa kama ifuatavyo:
Kwa kiwango changu cha pensheni nitakopeshwa 11.5m/=. Deni lililobaki hadi sasa ni 9.16m/= hivyo litakatwa na nitabaki na 2.34m/=.
Nimeshtuka Benki wamenieleza ati deni langu ni la mkataba wa miezi 72 (miaka 6), kwa hiyo, nitakatwa hiyo 285,177.53 kila mwezi kwa muda huo, yaani kwa hesabu rahisi, Benki ya Posta itapata 20,532,782.16!
Ndugu zangu, hata kama siyo mtaalam wa hesabu za kibenki, kwa interest rate gani mtu unaweza kukopa 10.5/= halafu ulipe zaidi ya 20/=! Kweli?
Naamini ndani ya JF hii wapo wastaafu; lakini pia, wapo wataalam wa masuala ya mikopo ya kibenki; naamini wamo humu watumishi waadilifu wa Benki ya Posta pia; Naomba msaada wenu wa Ushauri maana nahisi naibiwa na Benki hii.
Mbarikiwe.