Sijaelewa vema mikopo ya wastaafu TPB Bank. Nifahamisheni tafadhali

Sijaelewa vema mikopo ya wastaafu TPB Bank. Nifahamisheni tafadhali

VYEMELO

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2020
Posts
349
Reaction score
464
Mimi ni mstaafu Serikalini. Ni mmojawapo wa wastaafu tuliohamisishwa kujiunga na Benki ya Posta, nikahamasika kwelikweli hata nikahama Benki ya NMB. Jambo mojawapo lililonivutia kuhamia Benki ya Posta ni utaratibu mzuri wa mikopo kwa wastaafu; ilionekana kuwa na unafuu mkubwa ikilinganishwa na Benki ya NMB.

Sasa, nimekumbana na jambo limenichanganya.

Tarehe 12/04/2019 nilikopeshwa na Benki ya Posta 10.5m/= kwa makubaliano ya kuwa nalipa deni hilo kwa kukatwa kutoka pensheni yangu ya mwezi 285,177.53 kwa muda wa miaka 2.9.

Nimepata dharura nikaenda Benki kuhuisha mkopo, kwamba, niangaliziwe deni lililobaki ili likatwe kutokana pesa nitakazokopeshwa tena na hesabu zikawa kama ifuatavyo:

Kwa kiwango changu cha pensheni nitakopeshwa 11.5m/=. Deni lililobaki hadi sasa ni 9.16m/= hivyo litakatwa na nitabaki na 2.34m/=.
Nimeshtuka Benki wamenieleza ati deni langu ni la mkataba wa miezi 72 (miaka 6), kwa hiyo, nitakatwa hiyo 285,177.53 kila mwezi kwa muda huo, yaani kwa hesabu rahisi, Benki ya Posta itapata 20,532,782.16!

Ndugu zangu, hata kama siyo mtaalam wa hesabu za kibenki, kwa interest rate gani mtu unaweza kukopa 10.5/= halafu ulipe zaidi ya 20/=! Kweli?

Naamini ndani ya JF hii wapo wastaafu; lakini pia, wapo wataalam wa masuala ya mikopo ya kibenki; naamini wamo humu watumishi waadilifu wa Benki ya Posta pia; Naomba msaada wenu wa Ushauri maana nahisi naibiwa na Benki hii.

Mbarikiwe.
 
Mkuu mbona kama vile hesabu zako haziko sawa?

Na unapo sema ukatwe 285,177 kwa miaka 2.9 una mwana miaka 2 na miez 9?(Miezi 33) au miaka 2.9 x12 ambayo inakuja miez kama35??

Whatever the case naona kwa hip hela wala inakua haijarudi mbona??

Kwani mkataba mliandikiana vipi?
 
Tunaishukuru benki kwa kukufanyia ilicho kufanyia. Nyie wafanyakazi wa serikali mlikua mnajiona miungu watu mlipokua kwenye ajira halafu mlikishabikia sana chama. Endelea kuisoma namba. Mlipokua kwenye ajira mlihisi ninyi hamtaisoma namba.
 
Kabla ya ku-saini mkataba ulipitia na kuelewa vigezo na masharti ya mkopo?

Hilo ndio tatizo la wengi tunakubali ku-saini bila kusoma na kuelewa tunachoki-saini.
 
Enyi wastaafu tarajiwa!!
Yanayomkuta huyu mstaafu iwe fundisho.
Huwezi kupokea kiinua mgongo uimalize halafu uje kukopa tena hiyo pension ya kila mwezi.NEVER EVER
Mabenki msiwakopeshe wastaafu,waacheni na kinachowabakia.
 
Hongera kwa kustaafu mkuu,na mungu akubariki kwa hilo,nami pia namuomba sana Mungu anijarie nistaafu salama.

Back to the topic, hainiingii akilini kwa mtumishi uliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 ukipokea mshahara na huku ukiwa na Uhuru wa kukopa pesa toka mabenki tofauti hadi unastaafu unarudi tena kuanza kukopa badala ya kuanza kula pesa zako bila stress wewe unajipa stress tena,naamini kuna sehemu ulikosea mkuu ndo maaana hadi umri huo bado unakopa badala ya kuanza kupumzika wewe unakuwa tena mtumwa( pole kama nitakuwa nimekukosea heshima)

Na ukute hapo tayari una miaka miwili tu tangu ustaafu lakini tayari umemaliza Millioni 70+ na hazikukutosha ,kama mamilioni ya pensheni hayakumaliza changamoto zako unadhani pesa ya mikopo ndo itamaliza shida za maisha ulizonazo(nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza)

Umri wa utumishi ndo umri wa kujijenga,ukstaafu pesa unayopata ni yakula bata huku ukisubiri raia wakuimbie paranda litalia,parapanda x2,sasa wewe eti unasema kuna kitu ulikuwa hujakiweka sawa ndo maana ukamua kukopa ili ukiweke sawa,kukopa kwenyewe umekopa ndani ya miezi miwili unarudi tena kukopa hii inaonesha wewe ni mtu wa aina gani,unapenda starehe,pombe na pengine makahaba,maana hainiingii akili ukope m 10 ndani ya miezi miwili unarudi tena kurenew mkopo wewe utakuwa na changamoto kubwa sana kwenye hicho kichwa chako( nisamehe. Kama nitakukwaza maana kiumri wewe ni sawa na baba yangu ila kimatendo ni sawa na mtoto)

Pambana na hali yako,watu kama ninyi mnamatatizo sana ukiwa kijana unakuwa huna ujuzi wa kuanzisha miradi Leo hii umezeeka unaanza kukopa na kuwa mtaalamu wa miradi mbalimbali,ulishindwa kuanzisha hata genge la kuuza Karanga ukiwa katika umri wa miaka 20+ sasa hivi uko at 60+ utaweza kweli au ni kupoteza pesa tu ?.

Mwisho nakushauri uturie nyumbani ulee familia yako achana na mikopo na miradi yako hewa isiyo na tija,wewe pesa ya pensheni 70M + umemaliza ndani ya miaka miwili,ukakopa 10+M umemaliza ndani ya miezi miwili bado tena unarudi kukopa? Kitu ambacho hujui ni kuwa baada ya kustaafu ni muda muafaka kwa muhusika kusimamia miradi aliyoianzisha ungali katika utumushi na kula matunda yake na sio muda wa kuanzisha miradi hapo utachemka sana.

Nisamehe kama nitakuwa nimekukwaza
 
Hivi ikitokea huyo mstaafu amefariki, huo mkopo inakuwaje?
 
Tunaishukuru benki kwa kukufanyia ilicho kufanyia. Nyie wafanyakazi wa serikali mlikua mnajiona miungu watu mlipokua kwenye ajira halafu mlikishabikia sana chama. Endelea kuisoma namba. Mlipokua kwenye ajira mlihisi ninyi hamtaisoma namba.
Unaitafuta laana kwa speed ya jet!!
 
Enyi wastaafu tarajiwa!!
Yanayomkuta huyu mstaafu iwe fundisho.
Huwezi kupokea kiinua mgongo uimalize halafu uje kukopa tena hiyo pension ya kila mwezi.NEVER EVER
Mabenki msiwakopeshe wastaafu,waacheni na kinachobakia.
Acha aisome namba. Mitano tena
 
Unaitafuta laana kwa speed ya jet!!
Kama na wewe ni walewale walamba viatu vya sisiemu kisa unaajira serikali na ulishiriki kuiba/kulinda Kura za wizi. Your day is coming. Shukrani za CCM Ni Kama za yule mnyama beast of burden.
 
Mkuu unajua changamoto anazopitia au umeamua tu kumponda na mu-essay wote huo.
 
Mkuu unajua changamoto anazopitia au umeamua tu kumponda na mu-essay wote huo.
Hakuna cha changamoto mkuu,mimi mwenyewe mtumishi siwezi nikastafu nikapitia maisha anayopitia huyu mzee. Nina uzoefu na wastaafu wengi akiwemo baba yangu mdogo ambaye kwa sasa ni kama baba yangu mzazi, kastaafu baada ya pensheni kala na makahaba Leo hii ni mtumwa wa mikopo ya ajabu ajabu kama ya huyu mleta uzi.
 
Mikopo ya Bank ina mambo yaliyofichwafichwa sana... Yani ni faida tupu kwao...

Cc: mahondaw
 
JF ilipofikia ni pabaya. Mtu analeta hoja ya msingi watu wanaanza kumuattack matumizi yake ya ujana na pesa!!.
Yan noma sana walimwengu[emoji1][emoji2][emoji3][emoji2][emoji3]
 
Mimi ni mstaafu Serikalini. Ni mmojawapo wa wastaafu tuliohamisishwa kujiunga na Benki ya Posta, nikahamasika kwelikweli hata nikahama Benki ya NMB. Jambo mojawapo lililonivutia kuhamia Benki ya Posta ni utaratibu mzuri wa mikopo kwa wastaafu; ilionekana kuwa na unafuu mkubwa ikilinganishwa na Benki ya NMB.

Sasa, nimekumbana na jambo limenichanganya.

Tarehe 12/04/2019 nilikopeshwa na Benki ya Posta 10.5m/= kwa makubaliano ya kuwa nalipa deni hilo kwa kukatwa kutoka pensheni yangu ya mwezi 285,177.53 kwa muda wa miaka 2.9.

Nimepata dharura nikaenda Benki kuhuisha mkopo, kwamba, niangaliziwe deni lililobaki ili likatwe kutokana pesa nitakazokopeshwa tena na hesabu zikawa kama ifuatavyo:

Kwa kiwango changu cha pensheni nitakopeshwa 11.5m/=. Deni lililobaki hadi sasa ni 9.16m/= hivyo litakatwa na nitabaki na 2.34m/=.
Nimeshtuka Benki wamenieleza ati deni langu ni la mkataba wa miezi 72 (miaka 6), kwa hiyo, nitakatwa hiyo 285,177.53 kila mwezi kwa muda huo, yaani kwa hesabu rahisi, Benki ya Posta itapata 20,532,782.16!

Ndugu zangu, hata kama siyo mtaalam wa hesabu za kibenki, kwa interest rate gani mtu unaweza kukopa 10.5/= halafu ulipe zaidi ya 20/=! Kweli?

Naamini ndani ya JF hii wapo wastaafu; lakini pia, wapo wataalam wa masuala ya mikopo ya kibenki; naamini wamo humu watumishi waadilifu wa Benki ya Posta pia; Naomba msaada wenu wa Ushauri maana nahisi naibiwa na Benki hii.

Mbarikiwe.
Umeliwa
 
Back
Top Bottom