Uchaguzi 2020 Sijafurahishwa na idadi ya watu waliojitokeza kwa Tundu Lissu kwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Dodoma

Uchaguzi 2020 Sijafurahishwa na idadi ya watu waliojitokeza kwa Tundu Lissu kwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Dodoma

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Niwe muwazi mimi binafsi nina amini katika mabadiliko, mabadiliko ndiyo chachu ya maendeleo sehemu yoyote ile.

Nimeona na nimekuwa nikifatilia mikutano yote ya mgombea wetu hapa Dar na kuna afadhali kidogo japo mkutano wa segerea na kawe ulikuwa hauna watu sana, atleast kule Mbagala.

Naanza kupata picha, pengine kuna kitu hakipo sawa CHADEMA.

Tusi-conclude kuwa wanaoenda kwenye kampeni za CCM wanafata wasanii tu, hapana.

Ila kama wanafata wanancho wengi wanafata wasanii huko CCM basi sawa, ila pia basi kwa uwingi huohuo na kwa aina ya kukubalika kwa chama chetu basi walitakiwa pia wafate/waje kwa wingi kwenye kampeni zetu.

Kuna mikoa hadi sasa sinaelewa nini hasa kimetokea kutokana na uchache wa watu waliohudhuria tena kwenye viwanja vidogo sana ambavyo tumwchagua kufanyia kampeni.

Tuliona watu kule mwanza na tulifarijika sana na hilo na hadi tukatumia ndege nyuki (drones) kupiga picha za kampeni zetu. Ila baada ya hapo sikuona tena picha za juu (za drone) kwenye kampeni zetu.

Kilichotokea shinyanga, tabora na sasa dodoma ni aibu. Chama kitafute namna au kubadili mbinu ya kampeni ili tuweze kuvuta watu wengi waje kusikiliza sera.

Chini ni picha ya watu waliohudhuria kampeni hii leo huko Dodoma.

tapatalk_1599226773981.jpg
tapatalk_1599226805598.jpg
 
CCM wananichekeshaga sometimes, utadhani ni Mwanamke kisirani, ukiwaletea picha za watu wamejaa kwenye mkutano wanakwambia hao sio wapiga kura, ukileta picha za kubumba zinazoonyesha hakuna watu wanakwambia kuna tatizo, Chadema haikubaliki...... "Enyi Wagalatia msio na akili, nani kawaroga??"
 
Pamoja na hayo kuna watu wengi tu wako upande huo hasa watumishi ila huwezi kuwaona wanaenda huko.
Wanasubiri Oktoba kwenye sanduku
Ok, ila ilibidi wahudhurie kwa wingi kusikiza sera na ndio maana kukawa na mikutano. Vinginevyo kusingekuwa na mikutano, wangekuwa wanasubiri tu tarehe ifike wapige kura
 
Ccm wananichekeshaga sometimes, utadhani ni Mwanamke kisirani, ukiwaletea picha za watu wamejaa kwenye mkutano wanakwambia hao sio wapiga kura, ukileta picha za kubumba zinazoonyesha hakuna watu wanakwambia kuna tatizo, Chadema haikubaliki...... "Enyi Wagalatia msio na akili, nani kawaroga??"
Kamanda achana na hao ccm, watu ni muhimu kwenye kampeni. Leo dodoma hakuna watu kabisa, kuna tatizo chadema
 
Hizo ni ngome za Magufuri! Labda ambao wameshangaza ni Mwanza.
Kingine ambacho naona wananchi wameanza kukiona, matumaini ya kushinda CHADEMA hayapo kabisa.Na uko uwezekano Wapiga kura wengi wasijititokeze 28.10.2020.
 
Back
Top Bottom