Sijajua Serikali inatumia kipaumbele gani kujenga barabara za lami katika baadhi ya maeneo

Sijajua Serikali inatumia kipaumbele gani kujenga barabara za lami katika baadhi ya maeneo

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Hii barabara inajengwa Chanika mwisho,Lukooni mtaa wa Chabupu umbali wa mita 300 tu.

Barabara hii imepita mbele ya ofisi yangu kabisa inasemekana ni barabara kubwa inayotakiwa kuunganisha Chanika na Buza japo sina uthibitisho kamili.

Hakuna mradi wowote wa kiserikali kwa sasa na wala haitumiki kwa shughuri zozote muhimu ila inajengwa na Slaa alipita kujigamba kwamba anawajengea wananchi barabara.

Cha ajabu Chanika hapahapa kuna barabara muhimu inayoelekea stand kuu ya chanika ambayo ni muhimu ni mbovu na Haina rami na umbali unakadiriwa kuwa mita 600 tu ,na hata stand yenyewe haina sakafu ni vumbi tu na daladala nyingi huwa haziingii kule zinaenda kugeuzia Chanika Msumbiji ktk kituo cha mafuta cha Meruni.

Nilipata wasaha wakumuuliza msimamizi wa kazi hiyo kwa kampuni iliyopewa tenda (Southern Link LTD) kama wamepewa tenda yakurekebisha barabara ile ya stand akasema hapana.

Sambamba na hilo kuna barabara ya rami pia inajengwa Maeneo ya Pugu shule inaingia mtaani kabisa(Pale pugu shule kwenye kona unapoanza mteremko upande wa kushoto ndipo inapoanzia) nako hakuna mradi wowote muhimu ili hali kuna maeneo muhimu hayana miundombinu thabiti.

Hawa hutumia vigezo gani kujenga hizi roads.
 

Attachments

  • 0190C46A-B470-48CD-84DC-AD12E0349896.jpeg
    0190C46A-B470-48CD-84DC-AD12E0349896.jpeg
    860.9 KB · Views: 4
  • 8999A1E9-C142-420F-BCDE-97FF5703D45B.jpeg
    8999A1E9-C142-420F-BCDE-97FF5703D45B.jpeg
    1 MB · Views: 3
Nchi hii kila kitu kinaendeshwa kisiasa. Zipo barabara nyingi muhimu zimeongelewa muda mrefu ila imeishia hewani. Kuna Madaraja yalikatika wakati wa mvua mpaka leo hayaja tengenezwa. Angalia barabara kama ya mbezi-mpiji-mabwepande-bunju ambayo ingepunguza foleni barabara ya bagamoyo road mpaka leo hakuna kitu. Kiuhalisia Tanzania ni moja ya nchi yenye vipaumbele vibovu ambavyo vipo kuwanufaisha watawala.
 
Mkuu hiyo barabara inayowekwa rami ni ile ambayo ipo opposite na ile barabara ya kwenda stand (kituo kikubwa cha police)?
 
Acheni RAMI iwekwe jamani,Mama yupo moto sana
Mkuu wewe na mchangiaji mmoja
Rami~Lami
 
Back
Top Bottom