Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Hongera sana Kuna sehemu umetaja nimewahi kuishi miaka ya nyuma, umenikumbusha mbali sana
Difinga
Dihinda
Lusanga
Madizini
Turiani
Kidudwe
Mtibwa
Upande wa tanga nimetoka 2022 hapo kikunde mafulila Kuna mgodi wanapaita seita
Difinga kuna ardhi nzuri sana kwa Kilimo, tatizo barabara mbovu kutoa mazao na wachawi..
 
Huko mvomero sijanunua Bado maana nilikuwa sijawahi fika. Lengo lilikuwa kuangalia wapi nilirudi nikiwa vizuri ninunue hapo.

Nilinunua Gairo heka5 za kumbukumbu kwanza.
 
Mkuu hongera sana, Mimi pia mwaka huunilifanya safari kama hii ila Mkoa wa Tabora nikotokea Kahama. Nilienda Mambali, Itumbili mpaka Jibese. Hata Kahama maeneo mazuri yapo
Itumbili kazikwa Babu yangu huko. Shida ya huku ardhi hazina rutuba na upatikanaji wa maji ni mgumu mvua ndo hivyo za kulenga na manati.

Hongera pia mkuu mara zote Huwa ni hivyo.
 
Itumbili kazikwa Babu yangu huko. Shida ya huku ardhi hazina rutuba na upatikanaji wa maji ni mgumu mvua ndo hivyo za kulenga na manati.

Hongera pia mkuu mara zote Huwa ni hivyo.
Kumbe huko ndio chimbuko lenu, sikujua kama rutuba ni kipengele, Mimi napenda uwekezaji wa ufugaji kuliko kilimo.
Umeshatembelea Halmashauri ya Mlele, Ile barabara ya kutoka Tabora mpaka Mpanda? Maeneo ya Inyonga ni pazuri sana kwa kilimo na ufugaji.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Nikweli mkuu ni pazuri ila kama nilivyokuambia huku shida yetu Nia ardhi ishalimwa Hadi rutuba ikaisha na mvua Huwa sio za uhakika sana.

Chimbuko letu ni bariadi babu alienda kutafuta ardhi kipindi hicho yakiwa Bado mapori na Yana rutuba akaishi huko Hadi kufa. Nasisi ni Vyema kufuata nyayo zake
 
Upatapo muda njoo nikutembeze umalila mbeya vijijini ili upate Siri ya kwanini hakuna mnyakyusa mwembamba
Yupo jamaa nafanya nae kazi tunamwita mwamposa. Asee mshikaji ni mwembamba Hadi kapinda. somebody mwakimila.

Mkuu Ahsantee sana tuombe uzima mbeya sijawahi fika lkn amini nitakuja na nitakuja kweli.
 
Yupo jamaa nafanya nae kazi tunamwita mwamposa. Asee mshikaji ni mwembamba Hadi kapinda. somebody mwakimila.

Mkuu Ahsantee sana tuombe uzima mbeya sijawahi fika lkn amini nitakuja na nitakuja kweli.
Huyo amekulia mbeya mjini kwenye tabu na shida za dunia sio mbeya vijijini kwenye asali na maziwa yanayonisahulisha mijengo ya Dar es salaam
 
Umemaliza kabisa kule watu bado wanaamini ushirikina kuliko chochote, Yani mambo ya hovyo sana
Wachawi wala awasumbui kama una jua code wewe ni kuwakamata wazee ilo limeisha . Kuna sehemu tulikuwa na mradi mkubwa wa kilimo wakawa wamekausha bwawa la maji ikabidi tuwaibukie wazee wakafanya yao na kuchinja ngombe na wakawatahadhalisha kuwa wazee wametoa baraka zote asije akajaribu mtu yoyote kuleta mchezo baadae maji yakaludi bwawa lote likafilika na kilimo kinaendelea hadi leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…