Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Hongera sana Kuna sehemu umetaja nimewahi kuishi miaka ya nyuma, umenikumbusha mbali sana
Difinga
Dihinda
Lusanga
Madizini
Turiani
Kidudwe
Mtibwa
Upande wa tanga nimetoka 2022 hapo kikunde mafulila Kuna mgodi wanapaita seita
Difinga kuna ardhi nzuri sana kwa Kilimo, tatizo barabara mbovu kutoa mazao na wachawi..
 
Hii nchi ni neema kila kona. Hata Dodoma wanayosema kame kuna neema.
Ukienda Njombe, Mbeya, Katavi mpaka Kigoma ni neema tupu.
Waiskarl wanagombea ardhi ya Kabgwani wakati huku kwetu ni PARADISO iliojikalia tu.
Siku tutakapo amka tutakuwa tumechelewa. Hongera kuchukua hatua.
Umenunua heka ngapi ?
Huko mvomero sijanunua Bado maana nilikuwa sijawahi fika. Lengo lilikuwa kuangalia wapi nilirudi nikiwa vizuri ninunue hapo.

Nilinunua Gairo heka5 za kumbukumbu kwanza.
 
20241117_114331.jpg
 
Mkuu hongera sana, Mimi pia mwaka huunilifanya safari kama hii ila Mkoa wa Tabora nikotokea Kahama. Nilienda Mambali, Itumbili mpaka Jibese. Hata Kahama maeneo mazuri yapo
Itumbili kazikwa Babu yangu huko. Shida ya huku ardhi hazina rutuba na upatikanaji wa maji ni mgumu mvua ndo hivyo za kulenga na manati.

Hongera pia mkuu mara zote Huwa ni hivyo.
 
Itumbili kazikwa Babu yangu huko. Shida ya huku ardhi hazina rutuba na upatikanaji wa maji ni mgumu mvua ndo hivyo za kulenga na manati.

Hongera pia mkuu mara zote Huwa ni hivyo.
Kumbe huko ndio chimbuko lenu, sikujua kama rutuba ni kipengele, Mimi napenda uwekezaji wa ufugaji kuliko kilimo.
Umeshatembelea Halmashauri ya Mlele, Ile barabara ya kutoka Tabora mpaka Mpanda? Maeneo ya Inyonga ni pazuri sana kwa kilimo na ufugaji.
 
Heshima kwenu wakuu!

Niliazimia siku Moja nitembelee morogoro wilaya ya Gairo na Mvumero! Hatimae ikawadia na ikaenda sawa sawia kabisaa...

Kutoka kahama Hadi Gairo morogoro safari ilianza saa2:30.

Gari ilikuwa na changamoto kadhaa hasa kuharibika na Hadi kufika saa9 arasiri nikawa nimewasili salama Gairo.

Fuatana Nami nikupitishe Kwa machache kati ya mengi niliyoyaona.

Nilianza kuangalia Fursa zilizopo kandokando ya barabara kuu ya yaani ya kwenda Dar.

Fursa za uwekezaji zilizo Nje Nje nilizo ziona.

Maeneo hayo unaweza Jenga shule, ufugaji na kilimo Cha umwagiliaji japo itakupasa uchimbe kisima Kwa maji ya Uhakika

Safari yangu ndefu Sasa imetoka Barabara kuu na kushika barabara ya IYOGWE barabara hii itanipeleka hadi mpakani kati ya Morogoro na Tanga(Gairo &Tanga)

Nikiwa na usafiri wa pikpik Mimi pamoja na mwenyeji wangu. Sikuwa na budi ya kuweka full Tank maana nilihakikishiwa sitajutia kabisa na safari.....

Tukaanza ardhi yenye rutuba kiasi baridi kiasi likituandama huku milima ya uluguru ikiwa imefunikwa na wingu zito na mwonekano maridhawa kabisa.View attachment 3154970

Safari yetu iliendelea vizuri kabisa Na Hivi ndivyo vijiji nilivyo vipita Gairo ukielekea mpakani.

Br ya iyogwe:-
chakwale,
Nguyami,
Idibo,
itaragwe,
makuyu na Iyogwe.
(Kuna baadhi ya vijiji sikuona ubao) Pikipiki ilikuwa masaa....

Vijijini Hivi vipi wilaya ya Gairo morogoro

Na vinafaa sana Kwa ufugaji ila mifugo kama kuku,nguruwe ama ng'ombe wa maziwa kwani ni makazi ya watu.

Ukifuga mbuzi bila shaka utasumbuana na wakazi.

Nimefika mpakani Sasa
Sasa unaingia Mkoa wa Tanga..

View attachment 3154977
Baada tu ya kutoka mpakani Kuna mto nahisi ndo unatenganisha Gairo na kikunde.
Hapo unakutana na mto na wakazi wake waliendelea na shughuli za kilimo Cha umwagiliaji.

Kwa namna nilichoona pale jinsi ya eneo lilivyo na kinachofanyika pale niliona ni mzaha mkubwa. Maji ni ya kutekenya tu lakini kinacholimwa ni kidogo sana ardhi Ina rutuba Hali ya hewa nzuri.

Nilipofika KIKUNDE SENTA Nilikuta vijana wamekaa wanaotoa moto hawana habari na wengine nikawaona wanaranda tu mtaani kwenye vijiwe nilisitikika sana kuona vijana hawana habari kabisa na fursa nilizo ziona Mimi!!

Ukweli ni kwamba pamoja na ardhi kuanzia kikunde nk Inakubali sana Kwa mazao kama mahindi, maharage,mihogo, Kwa kifupi karibia Kila zao la nafaka linakubali maeneo hayo

Wenyeji watatusaidia hapa.


Tu

View attachment 3154979

View attachment 3154981
Ardhi yenye rutuba mito yenye maji lakini hakuna mazao ya umwagiliaji!
View attachment 3154983
Ardhi inalipa sana Kwa kilimo Cha matunda kwani Kwa macho yangu nimeona miti ya miembe(kienyeji) imestawi sana na Bahati nzuri lazima bondeni kuwe na mto

Ardhi ni nzuri Kwa uwekezaji wa kilimo na huku Sasa hata ufunge ng'ombe wa kwenda kuchunga na jioni uwarudishe panastahili!

Shauku Bado ikiwa inahitaji kuendelea kusonga mbele zaidi na kuona namna halisi ya Nchi ya maziwa na Asali

Baada ya kutoka Kikunde Kuna vijiji kama..

kikunde,
ludewa,
mafulila,Tunguli,
Lusane

Hapo Tunguli Kuna pori kubwa na zuri Kwa kilimo na ufugaji barabara ya uhakika japo ni vumbi.

Tunguli ni pazuri sana Kwa uwekezaji mkubwa.

Nimeona Kwa macho yangu watu wakifyeka pori Kwa ajiri ya
kilimo nk.
View attachment 3154985
View attachment 3154986
Hatimae kipande Cha Tanga nikakimaliza na kuingia wilaya ya Mvomero (morogoro)

Swadakta kabisaa mazingira & Hali ya hewa ilinivutia kuliko kifani!!!

Ikanilazimu kutoka moyoni nipambatize Kwa jina jipya la Thailand.

Kwani sehemu hii ni sehemu ambayo kijogorafia imekaa kama ughaibuni(Thailand japo sijafika)

Misitu minene yenye ukijani kibichi kabisa kama paradiso! Ukiangalia baadhi ya clip za Thailand utakubaliana Nami pasina shaka yoyote Ile!

Kwa wale wafanyakazi unayependa mazingira kama Yale ni muda wako Sasa wa kwenda kuona huko kwenye vijiji Hivi...

kibati,
kibogoji,
masimba,
Difinga,
Apendae,
Kwakwempe,
magotwe,
Kwa Dole
Lusanga
Tuliani,
manyiga,
mlaguzi.
Dakawa,
Hembeti,
Magole,
Dumila feli,
Dumila,

Hapa Kwa Retirement panafaa mnoo Kuna baadhi ya sehem nzuri,nzuri sana,na nzuri kabisa!!!

Ni juu Yako wewe Sasa wapi utapapenda

Hapo nimeunganisha Hadi Dumila.. maeneo yote hayo unalima muda wowote ukitaka

Niliona Kwa macho yangu Nchi hii Ina Tiririka maziwa na Asali.
************************
Pamoja na hayo yote nilichojifunza nikuwa
Vijana wa maeneo Tajwa ni wavivu usipime!

Nilicho shangaa nikaenda kupata supu halafu tukakoswa limao na kuletewa limao la unga zile zinauzwa kwenye pakiti Ili Hali ardhi Ile ukipanda mti haihitaji hata kumwagilia Cha ajabu limao ni anasa na vijana wapo tu.

Vijana nawaomba tutoke mjini kama huna issue ya maana.
Manyanza Toka magetoni Toka Dar uachane na biashara ya kupiga chabo wazaramo wakimwanga ladhi.

Niishie hapa nitaendelea kwenye comment
View attachment 3154987
Haya ndiyo mazingira murua kabisa ya baadhi ya vijiji/vitongoji Tajwa hapo juu.View attachment 3154988
Fenesi hili nilijipatia Kwa Tsh1000 hapo ni Kwa Apendae.



Ardhi yenye maziwa na Asali.View attachment 3154992View attachment 3154993
Sehemu tulivu sana huku sauti ndege za ndege zikiimba utukufu wa Mungu!!View attachment 3154998hapo passion3 zinauzwa Kwa 200 ndizi3 sh 200 embe2 dodo og zinauzwa500.View attachment 3155001View attachment 3155000
Tafadhar Endelea kubaki hapa.
View attachment 3155002
Nyumba hizi uzionazo ni kando kando ya barabara.uzuri ni kwamba njia inapitika Kwa Uzuri bila shida yoyote.


NB: Picha zote hizi zimepigwa kiangazi 17/11/2024.

Kama mahitaji video zipo nzuri kabisaa!! Niwezeshe vocha iwe ya jero ama buku niweke hapa nitumie Pm.

Ahsanteen sana.
👏👏👏
 
Kumbe huko ndio chimbuko lenu, sikujua kama rutuba ni kipengele, Mimi napenda uwekezaji wa ufugaji kuliko kilimo.
Umeshatembelea Halmashauri ya Mlele, Ile barabara ya kutoka Tabora mpaka Mpanda? Maeneo ya Inyonga ni pazuri sana kwa kilimo na ufugaji.
Nikweli mkuu ni pazuri ila kama nilivyokuambia huku shida yetu Nia ardhi ishalimwa Hadi rutuba ikaisha na mvua Huwa sio za uhakika sana.

Chimbuko letu ni bariadi babu alienda kutafuta ardhi kipindi hicho yakiwa Bado mapori na Yana rutuba akaishi huko Hadi kufa. Nasisi ni Vyema kufuata nyayo zake
 
Upatapo muda njoo nikutembeze umalila mbeya vijijini ili upate Siri ya kwanini hakuna mnyakyusa mwembamba
Yupo jamaa nafanya nae kazi tunamwita mwamposa. Asee mshikaji ni mwembamba Hadi kapinda. somebody mwakimila.

Mkuu Ahsantee sana tuombe uzima mbeya sijawahi fika lkn amini nitakuja na nitakuja kweli.
 
Yupo jamaa nafanya nae kazi tunamwita mwamposa. Asee mshikaji ni mwembamba Hadi kapinda. somebody mwakimila.

Mkuu Ahsantee sana tuombe uzima mbeya sijawahi fika lkn amini nitakuja na nitakuja kweli.
Huyo amekulia mbeya mjini kwenye tabu na shida za dunia sio mbeya vijijini kwenye asali na maziwa yanayonisahulisha mijengo ya Dar es salaam
 
Umemaliza kabisa kule watu bado wanaamini ushirikina kuliko chochote, Yani mambo ya hovyo sana
Wachawi wala awasumbui kama una jua code wewe ni kuwakamata wazee ilo limeisha . Kuna sehemu tulikuwa na mradi mkubwa wa kilimo wakawa wamekausha bwawa la maji ikabidi tuwaibukie wazee wakafanya yao na kuchinja ngombe na wakawatahadhalisha kuwa wazee wametoa baraka zote asije akajaribu mtu yoyote kuleta mchezo baadae maji yakaludi bwawa lote likafilika na kilimo kinaendelea hadi leo
 
Back
Top Bottom