Mtili wandu
JF-Expert Member
- Dec 15, 2012
- 8,257
- 11,499
Sina jibu nilitaka uende ukacheki km ulivyofanya huko mkuu.Mkuu Kwa wastani wanauzwaje huko ardhi iwapo nahitaji heka10-15 naweza andaa angalu sh. Ngapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sina jibu nilitaka uende ukacheki km ulivyofanya huko mkuu.Mkuu Kwa wastani wanauzwaje huko ardhi iwapo nahitaji heka10-15 naweza andaa angalu sh. Ngapi?
Ila ulinisikitisha ulipopita hapa kwetu huyo abiria wako aliomba apumzike kidogo hapa kwangu kutoa uchovu ukamkatalia
Hapo Dumila Centre kuna Mkuu wangu wa Shule pale Dakawa High School, Mzee Kijame allstaafia hapo na anafanya vizuri sana kwenye ufugaji na kilimo. Mtafute mwambie namsalimia halafu muombe akuoe ABC nzuri zaidi za fursa hapo!!Moja ya daraja zuri kabisaView attachment 3155007
Mkuu nakuja pm speed mno. Halafu pia nimwambie anadalimiwa na mtoto wa shule?😹😹Hapo Dumila Centre kuna Mkuu wangu wa Shule pale Dakawa High School, Mzee Kijame allstaafia hapo na anafanya vizuri sana kwenye ufugaji na kilimo. Mtafute mwambie namsalimia halafu muombe akuoe ABC nzuri zaidi za fursa hapo!!
Mkuu ahsantee. January nakuja huko nipo seriou sana.Wakati mwingine uje na Kilosa nikutembeze vijijini ujionee fursa za wazi kuanzia:-
Dumila na mateteni-kilimo Cha Nyanya
Kilangali, Tindiga, Kivungu- Kilimo Cha mpunga
Zombo, Ulaya-kilimo Cha mahindi
Lumuma, Pwaga, Mnozi, Ruaha mbuyuni, Kitati, Kidete n.k - kilimo Cha vitunguu na Mahindi
Sehemu zote hizo mazao mchanganyiko kama mbaazi, ufuta, kunde, maharage, alizeti n.k yanalimwa sana pia ufugaji wa kuku, Bata, kanga, mbuzi, nguruwe, Ng'ombe, punda n.k
Karibu Kilosa
Mkuu tulikuwa masaa hakuna aliyeomba kupumzika huyu atakuwa ni mwingine.wapi ulipo mkuu?Ila ulinisikitisha ulipopita hapa kwetu huyo abiria wako aliomba apumzike kidogo hapa kwangu kutoa uchovu ukamkatalia
Sawa ahsantee sana. January nitakuwa likizo hivyo likizo yangu nittaitumia vizuri mno.Sina jibu nilitaka uende ukacheki km ulivyofanya huko mkuu.
Nilivyoona tu hata robo yake Bado hatuja yamaliza mkuu. Na huo uwekezaji wanao fanya ni kupata chakula na Hela ya mboga basiKumbe bado kuna maeneo mengi tu ya kufanya uwekezaji hapa Tanzania
Mkuu huku nilipo nkama ardhi yote yenye rutuba wat washaichangamkia kitambo sana sasa hayo maeneo ambayo bdo vijana hawajaamua ndo ya kuweka kambi. nashukulu kwa huu uzi wako mkuu!Na hapo nimetembela wilaya kama 2 tu na sio sehem zote mkuu
Karibu sanaMkuu ahsantee. January nakuja huko nipo seriou sana.
Mkuu makazi yangu yatakuwa Turiani hapo na mishe zote zitakuwa huko ndani ndaniHingera kwa kuamua kuoambana na kushare na wana JF fursa sio kila saa wawaze ngono tu.
Binafsi nimelima sana na kufanya biashara ya Mahindi Tunguli miaka 2005. Nimefika hadi huko Idibo na askari wake wale sungusungu walikuwa maarufu sana kipindi cha nyuma na tuliwatumia kutishia masai wakati wa mapigano ya wamasai na wakulima miaka hiyo.
Kwa upande wa Mvomero japo we umekosea ukaandika Mvumero nimelima sana huko na hata sasa nalima mpunga kwenye skimu ya umwagiliaji Dakawa chini ya UWAWAKUDA.
Nimefurahi kuona umefika hadi Maskati. Huko nilikuwaga na mchepuko wakati nahangaika kwenye biashara. Hapo Hembeti nikipataga mtoto mmoja mzuri sana miaka hiyo. Sasa ameolewa yule binti Tillya.
Niliishi sana Turiani maeneo ya Kilimanjaro nikichezea Mtibwa Sugar kipindi hiko tukiwa na akina Mkangwa na Zuberi Katwila.
Huko fursa nje nje bro. Njoo tulime mpunga hapa Dakawa au tulime miwa tuuze Mkulazi au tulime nyanya mateteni, Mbigili na Dumila.
Ahsantee sana mkuuKaribu sana
Kabisa mkuu. Binafisi niliwiwa kushare hapa Ili mwenye kuthubutu na athubutu tu. Na atakae acha basi nafisi yake itamshitaki daima.Mkuu huku nilipo nkama ardhi yote yenye rutuba wat washaichangamkia kitambo sana sasa hayo maeneo ambayo bdo vijana hawajaamua ndo ya kuweka kambi. nashukulu kwa huu uzi wako mkuu!
Heshima kwenu wakuu!
Niliazimia siku Moja nitembelee morogoro wilaya ya Gairo na Mvumero! Hatimae ikawadia na ikaenda sawa sawia kabisaa...
Kutoka kahama Hadi Gairo morogoro safari ilianza saa2:30.
Gari ilikuwa na changamoto kadhaa hasa kuharibika na Hadi kufika saa9 arasiri nikawa nimewasili salama Gairo.
Fuatana Nami nikupitishe Kwa machache kati ya mengi niliyoyaona.
Nilianza kuangalia Fursat zilizopo kandokando ya barabara kuu ya yaani ya kwenda Dar.
Fursat za uwekezaji zilizo Nje Nje nilizo ziona.
Maeneo hayo unaweza Jenga shule, ufugaji na kilimo Cha umwagiliaji japo itakupasa uchimbe kisima Kwa maji ya Uhakika
Safari yangu ndefu Sasa imetoka Barabara kuu na kushika barabara ya IYOGWE barabara hii itanipeleka hadi mpakani kati ya Morogoro na Tanga(Gairo &Tanga)
Nikiwa na usafiri wa pikpik Mimi pamoja na mwenyeji wangu. Sikuwa na budi ya kuweka full Tank maana nilihakikishiwa sitajutia kabisa na safari.....
Tukaanza ardhi yenye rutuba kiasi baridi kiasi likituandama huku milima ya uluguru ikiwa imefunikwa na wingu zito na mwonekano maridhawa kabisa.View attachment 3154970
Safari yetu iliendelea vizuri kabisa Na Hivi ndivyo vijiji nilivyo vipita Gairo ukielekea mpakani.
Br ya iyogwe:-
chakwale,
Nguyami,
Idibo,
itaragwe,
makuyu na Iyogwe.
(Kuna baadhi ya vijiji sikuona ubao) Pikipiki ilikuwa masaa....
Vijijini Hivi vipi wilaya ya Gairo morogoro
Na vinafaa sana Kwa ufugaji ila mifugo kama kuku,nguruwe ama ng'ombe wa maziwa kwani ni makazi ya watu.
Ukifuga mbuzi bila shaka utasumbuana na wakazi.
Nimefika mpakani Sasa
Sasa unaingia Mkoa wa Tanga..
View attachment 3154977
Baada tu ya kutoka mpakani Kuna mto nahisi ndo unatenganisha Gairo na kikunde.
Hapo unakutana na mto na wakazi wake waliendelea na shughuli za kilimo Cha mwagilia.
Kwa namna nilichoona pale jinsi ya eneo lilivyo na kinachofanyika pale niliona ni mzaha mkubwa. Maji ni ya lutekenya tu lakini kinacholimwa ni kidogo sana ardhi Ina rutuba Hali ya hewa nzuri.
Nilipofika KIKUNDE SENTA Nilikuta vijana wamekaa wanaotoa moto hawana habari na wengine nikawaona wanaranda tu mtaani kwenye vijiwe nilisitikika sana kuona vijana hawana habari kabisa na fursa nilizo ziona Mimi!!
Ukweli ni kwamba pamoja na ardhi kuanzia kikunde nk Inakubali sana Kwa mazao kama mahindi, maharage,mihogo, Kwa kifupi karibia Kila zao la nafaka linakubali maeneo hayo
Wenyeji watatusaidia hapa.
Tu
View attachment 3154979
View attachment 3154981
Ardhi yenye rutuba mito yenye maji lakina hakuna mazao ya umwagiliaji!
View attachment 3154983
Ardhi inalipa sana Kwa kilimo Cha matunda kwani Kwa macho yangu nimeona miti ya miembe(kienyeji) imestawi sana na Bahati nzuri lazima bondeni kuwe na mto
Ardhi ni nzuri Kwa uwekezaji wa kilimo na huku Sasa hata ufunge ng'ombe wa kwenda kuchunga na jioni uwarudishe panastahili!
Shauku Bado ikiwa inahitaji kuendelea kusonga mbele zaidi na kuona namna halisi ya Nchi ya maziwa na Asali
Baada ya kutoka Kikunde Kuna vijiji kama..
kikunde,
ludewa,
mafulila,Tunguli,
Lusane
Hapo Tunguli Kuna pori kubwa na zuri Kwa kilimo na ufugaji barabara ya uhakika japo ni vumbi.
Tunguli ni pazuri sana Kwa uwekezaji mkubwa.
Nimeona Kwa macho yangu watu wakifyeka pori Kwa ajiri ya
kilimo nk.
View attachment 3154985
View attachment 3154986
Hatimae kipande Cha Tanga nikakimaliza na kuingia wilaya ya Mvumero (morogoro)
Swadakta kabisaa mazingira & Hali ya hewa ilinivutia kuliko kifani!!!
Ikanilazimu kutoka moyoni nipambatize Kwa jina jipya la Thailand.
Kwani sehemu hii ni sehemu ambayo kijogorafia imekaa kama ughaibuni(Thailand japo sijafika)
Misitu minene yenye ukijani kibichi kabisa kama paradiso! Ukiangalia baadhi ya clip za Thailand utakubaliana Nami pasina shaka yoyote Ile!
Kwa wale wafanyakazi unayependa mazingira kama Yale ni muda wako Sasa wa kwenda kuona huko kwenye vijiji Hivi...
kibati,
kibogoji,
masimba,
Difinga,
Apendae,
Kwakwempe,
magotwe,
Kwa Dole
Lusanga
Tuliani,
manyiga,
mlaguzi.
Dakawa,
Hembeti,
Magole,
Dumila feli,
Dumila,
Hapa Kwa Retirement panafaa mnoo Kuna baadhi ya sehem nzuri,nzuri sana,na nzuri kabisa!!!
Ni juu Yako wewe Sasa wapi utapapenda
Hapo nimeunganisha Hadi Dumila.. maeneo yote hayo unalima muda wowote ukitaka
Niliona Kwa macho yangu Nchi hii Ina Tiririka maziwa na Asali.
************************
Pamoja na hayo yote nilichojifunza nikuwa
Vijana wa maeneo Tajwa ni wavivu usipime!
Nilicho shangaa nikaenda kupata supu halafu tukakoswa limao na kuletewa limao la unga zile zinauzwa kwenye pakiti Ili Hali ardhi Ile ukipanda mti haihitaji hata kumwagilia Cha ajabu limao ni anasa na vijana wapo tu.
Vijana nawaomba tutoke mjini kama huna issue ya maana.
Manyanza Toka magetoni Toka Dar uachane na biashara ya kupiga chabo wazaramo wakimwanga ladhi.
Niishie hapa nitaendelea kwenye comment
View attachment 3154987
Haya ndiyo mazingira murua kabisa ya baadhi ya vijiji/vitongoji Tajwa hapo juu.View attachment 3154988
Fenesi hili nilijipatia Kwa Tsh1000 hapo ni Kwa Apendae.
Ardhi yenye maziwa na Asali.View attachment 3154992View attachment 3154993
Sehemu tulivu sana huku sauti ndege za ndege zikiimba utukufu wa Mungu!!View attachment 3154998hapo passion3 zinauzwa Kwa 200 ndizi2 sh 2000 embe2 dodo og zinauzwa500.View attachment 3155001View attachment 3155000
Tafadhar Endelea kubaki hapa.
View attachment 3155002
Nyumba hizi uzionazo ni kando kando ya barabara.uzuri ni kwamba njia inapitika Kwa Uzuri bila shida yoyote.
NB: Picha zote hizi zimepigwa kiangazi 17/11/2024.
Kama mahitaji video zipo nzuri kabisaa!! Niwezeshe vocha iwe ya jero ama buku niweke hapa nitumie Pm.
Ahsanteen sana.
Mkuu vipi kuhusu mbegu mnazotumia ni za kisasa? Maana niliona ni fupi sana zingine ndo Bado kabisa hata hazijataka kuvunwaKaribu sana
Mkuu uko sawa sana. Lakini itanibidi nithubutu tu Kwa namna yoyote Ile.Chunga tu hayo maeneo wanaloga haswa, weka budget ya ushirikina kwenye investment cost!
Mkuu uko sawa sana. Lakini itanibidi nithubutu tu Kwa namna yoyote Ile.
Tulikodi pikipiki 1 Kwa 20k nikaweka mafuta30kGharama ya usafiri wa pikipiki ilikuaje mkuu,