Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Wakati mwingine uje na Kilosa nikutembeze vijijini ujionee fursa za wazi kuanzia:-
Dumila na mateteni-kilimo Cha Nyanya
Kilangali, Tindiga, Kivungu- Kilimo Cha mpunga
Zombo, Ulaya-kilimo Cha mahindi
Lumuma, Pwaga, Mnozi, Ruaha mbuyuni, Kitati, Kidete n.k - kilimo Cha vitunguu na Mahindi

Sehemu zote hizo mazao mchanganyiko kama mbaazi, ufuta, kunde, maharage, alizeti n.k yanalimwa sana pia ufugaji wa kuku, Bata, kanga, mbuzi, nguruwe, Ng'ombe, punda n.k

Karibu Kilosa
 
Hapo Dumila Centre kuna Mkuu wangu wa Shule pale Dakawa High School, Mzee Kijame allstaafia hapo na anafanya vizuri sana kwenye ufugaji na kilimo. Mtafute mwambie namsalimia halafu muombe akuoe ABC nzuri zaidi za fursa hapo!!
Mkuu nakuja pm speed mno. Halafu pia nimwambie anadalimiwa na mtoto wa shule?😹😹
 
Mkuu ahsantee. January nakuja huko nipo seriou sana.
 
Mkuu makazi yangu yatakuwa Turiani hapo na mishe zote zitakuwa huko ndani ndani
Kwahiyo sehemu alikuwa hapa sio😂😂
 
Mkuu huku nilipo nkama ardhi yote yenye rutuba wat washaichangamkia kitambo sana sasa hayo maeneo ambayo bdo vijana hawajaamua ndo ya kuweka kambi. nashukulu kwa huu uzi wako mkuu!
Kabisa mkuu. Binafisi niliwiwa kushare hapa Ili mwenye kuthubutu na athubutu tu. Na atakae acha basi nafisi yake itamshitaki daima.
 

Chunga tu hayo maeneo wanaloga haswa, weka budget ya ushirikina kwenye investment cost!
 
Mkuu uko sawa sana. Lakini itanibidi nithubutu tu Kwa namna yoyote Ile.

Nina heka 200 handeni ndugu, ardhi safi, maji ya kuchimba, nina tractor na nimesafisha 40 hela 20 sasa, nilichezeshwa mno, nikatafuta wambulu 3 ( nao si haba kishirikina ) nikawanunulia na mifugo, siwalipi, wanajiendesha kwa tractor, mifugo na vibarua, na nimewapa target wasafishe angalau hela 150

Mimi Kule sitarudi mpaka Wageni wewe wengi!
 
Gharama ya usafiri wa pikipiki ilikuaje mkuu,
Tulikodi pikipiki 1 Kwa 20k nikaweka mafuta30k

Pkpk nyingine ilikuwa ya mwenyeji wangu niliweka mafuta ya30k

Jumla na kula na kuwapa Hela wanazengo pale tulishuka kupiga story nikama 160k tu halafu kula tulikubu 8000 tu watu nne matunda tulipewa Bure kama maembe na ndizi.

Nchi hii inawatu wachangamfu kweli. Unafika nakuanza kupiga story kama mnafahamina asee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…