Sheria inasema ukifanya kazi mahali kwa muda wa zaidi ya miezi 6 wewe unahesabika ni mwajiriwa.
Lakini kabla hujaanzisha kesi inabidi ujipange sana,ninachojua watu kama hao huwa wanajipanga sana hawakurupuki na usikute kuna wenzako kama wewe walijaribu kuanzisha kesi kama wewe wakafeli.
Ni jambo linahitaji busara sana.
wahusika wa kusuluhisha hiyo kesi ni CMA/wizara ya kazi.
Lakini hakikisha kabla hujaenda uwe na vithibitisho kwamba kweli wewe ni mfanyakazi wao na umefanya kazi hapo kwa hiyo miezi 12.
Kama hakuna mkataba wowote uliosaini hakikisha uwe na kitambulisho,kama hauna kitambulisho hakikisha makaratasi ya kuonesha malipo yako ya kila mwezi,ukikosa hivyo basi upate hata daftari la attendance/mahudhurio.
Hivyo ndio vitu utaulizwa ukifika mahakamani na kama hauna hivyo vitu utafeli halafu utabaki na uadui tu,utaishi maisha ya wasiwasi bila mpango.
Jitafakari kwa hilo.