Kuna kisa kimoja kilitokea ulaya lakini. Mwanaume anaishi na mkewe na mtoto m'moja. Siku moja yule mwanamke wakaja rafiki zake wa kike ambao ni mashost wa muda mrefu sana tokea enzi za utoto.
Ni wadada wanaopenda sana usichana na hadi wakati huo wameshaingia umri wa ndoa walikuwa bado hawajaolewa wanaishi maisha ya kuwa huru kufanya lolote na kudate wanaetaka.
Sasa siku moja walikuja vijana ambao walikuwa wanajuana na wale wadada, wakawatoa out ili wakale bata. Yule dada akamwambia mume wake kuwa anamtoko na wenzake, mume wake akamuuliza kuwa wanaenda wapi na occasion ni ipi yaani mtoko unahusiana na kitu gani, birthday, dinner, shopping au nini? Mwanamke hakuwa na jibu zaidi ya kusema yeye na mashosti zake wanaenda onana na rafiki wengine so ni good time tu.
Jamaa akamwambia hajapenda hiyo idea mwanamke akang'aka kuwa atakwenda na yeye sio mtoto mdogo kuamuliwa. Jamaa akaepusha zogo akakaa kimya. Bi dada akatoka out akaenda zake. Ule usiku hakurejea kama alivyoahidi. Na simu yake ilikuwa ikiita tu.
Siku kama ya Tatum's jamaa akiwa ameshaingiwa na hofu ya kutosha asijue nini kimempata mkewe akapata simu kutoka hospital wakitamka kufika maana mkewe ameanza kupata fahamu. Akaenda na kukuta mkewe yupo hospital maelezo ya daktari ni kuwa aliwekewa kilevi yeye na wenzake pia na walitelekezwa hotelini hadi staff wa hoteli walipohisi hali isiyo ya kawaida ya ukimya na kufungua mlango wa chumba na kuwatoa wakiwa hawajitambui na kuwafikisha hospital.
Baada ya kupata fahamu askari waliwahoji na ndipo walielezea kuwa walipatwa na hiyo hali baada ya kunywa vinywaji ila hawakumbuki baada ya kuingia hotelini hapo maana walipoteza ufahamu. Vipimo vilionyesha walibakwa na hata wao walihisi kubakwa. So kesi ikafunguliwa na upelelezi ukaanza mara moja.
Waliporejea nyumbani mwanaume akiwa ana hasira kifuani. Yule dada kwa kuwasiliana na wenzake wakawatafuta wale jamaa kupitia mawasiliano ya simu na mtandaoni. Baadae walipata ujumbe wa vitisho kupitia namba ambayo haionekani "Unknown number" ukiwaelekeza kudrop chargers ama wanaleak video tapes zao mitandaoni. Jamaa maana waliwarekodi wakiwa wanawaingilia wakiwa hawajitambui na walishiriki wakiwa wamelewa kabisa so hawakuwa wakijitambua. Wale wadada hawakusita na wakafikisha hizo sms polisi na kuendelea na upelelezi wa polisi ikiwamo kushare hizi story kwenye mitandao ya jamii na vituo vya habari.
Huyu dada akaanza alikuja kuona mwanaume wake hana time na habari za hiyo kesi wala kushirikiana nae kutafuta hawa watu. Akaanza kumlaumu, mwanaume akampa Makavu yake live. Akamwambia nilikwambia usiende popote siku ile ila ukaniambia wewe ni mtu mzima haupangiwi unaamua kwa uhuru wako. Haujaniheshimu mimi wala haujamheshimu binti yetu ambaye kesho atakuja kuwa mkubwa na kukuta story kuwa mama yake alibakwa na wanaume aliotoka nao out huku baba yake akiwa nyumbani na mtoto mdogo.
Mwanamke akawa anamlamu jamaa kuwa yeye hakupanga haya yatokee alitoka tu out kupata good time na rafiki zake ila haya mengine ni uhalifu. Jamaa akamkata asiendelee kumletea ligi. Hawajakaa sana siku kadhaa tokea siku ya tukio mume akapata video ya ngono iliyorekodiwa kwenye tukio na kuambiwa amuonye mkewe na wenzake wasiendelee na kesi wakaifute wala wasije kutokea mahakamani ikitakiwa kufanyika hivyo.
Jamaa akamuonyesha mkewe na kumpatia nyaraka za talaka assign. Mwanamke alilalamika sana kuwa mwanaume wake hana utu kumuacha kipindi kigumu kama hicho kwenye maisha yake. Akapost social media video akiwa analia na kuelezea hiyo story yake nadhani ilikuwa ni TikTok. Watu waligawanyika, wapo waliosapoti maamuzi ya mume wake wakisema mwanamke kiburi chake kimemponza na wapo waliomtetea mwanamke na kusema yeye alitoka na marafiki kula Good time ila kama wasingefanyiwa uhalifu wa kuwekewa vilevi kwenye kinywaji asingekubali kwenda hotelini na wanaume wengine.
Wanawake huwa wanaviburi sana na hii ni sifa ya mwanamke anayesikiliza akili yake inataka nini huwa hainaga matokeo mazuri. Ni vema kumsikiliza mwanaume pale anapoonyesha kutoridhika na maamuzi yako au jambo lolote unalomwambia.