Sijamuelewa Mtukufu juu ya Tausi wa ikulu

Sijamuelewa Mtukufu juu ya Tausi wa ikulu

Ilikuwa hatari kwa afya za wazee wastaafu bila barakoa. Niliwaona walivyojiachia bila kinga; hasa mzee Mwinyi
 
Hahaha, nadhani jamaa walikuwa wakimshangaa tu kimoyomoyo
Tausi wenyewe walikuwa wameshakaa nao pale Ikulu, Wala sio kitu kipya kwao..eti tausi 25 kila mmoja
Huwezi kujua, pengine masharti ya mganga wake.
 
Ujue mtu akishindwa kazi ya kupima watu Covid-19, lazima azushe zushe vitu vingine ambavyo havina kichwa wala mguu ili mradi ajiineshe kafanikiwa tu.

Watu wako katika pandemic, yeye anaita wastaafu kuwapa tausi?

Hao wazee wengine wanakaribia miaka 100 wakipata kirusi hapo na kufa atakubali kuchukua lawama?
Jamaa anawapongeza eti hawajavaa barakoa.

Viongozi wetu ni wanafiki sijawahi kuona.

Angalia mawaziri wote akiwemo pm wakiwa bungeni au mahala popote wanavaa barakoa ila wakienda kwa rais wanavua ili kumfurahisha mshikaji.

Hao wazee jamaa anataka wanase covid-19 waage Dunia.
 
Leo ikulu chamwino mtukufu rais Magufuli amewapa zawadi ya tausi 25 kwa kila moja kwa marais watatu wastaafu na idadi hiyo kwa mjane wa baba wa taifa mama maria Nyerere ,nampongeza kwa hilo na nijambo la kizalendo sana

Lakini nikirudisha kumbukumbu zangu vizuri nyuma nakumbuka mtukufu alimpa kenyata tausi wake binafsi huko chato alipomtembelea mapumzikoni

Sasa kutokana na kuwa nauelewa mdogo uliopelekea kufeli std 7 nilielewa kuwa Tanzania kuna tausi wengi
Ila chakunichanganya Leo nikuwa Mtukufu amesema Tz hakuna Tausi ila waliletwa na Baba wa taifa hayati Mwalim Nyerere
Sasa naomba kueleweshwa zaidi na ninyi mliosoma zaidi kuwa Tanzania kuna Tausi wengi zaidi ya wale waikulu?
Au hatawale aliopewa rais kenyata walikuwa Mali ya Ikulu?

Naombeni kueleweshwa
Mkulu alijimilikisha..... Baada ya kuona watu hawakufurahishwa na hilo ameamua kuwapa wenzake ili asionekane kama ni yeye peke yake mwenye hao Tausi. Nyerere aliwaacha pale hakuwachukua na waliofuata wakafanya vile vile. Jamaa kaamua kuwapa kinguvu maboss wake wa zamani na hakuna wa kuataa maana wanajua. Kama walikuwa wanawataka hao Tausi wangefanya hivyo wakati wa utawala wao.
 
Kwa alichofanya Rais Magufuli kugawa hao ndege Tausi kwa Marais wastaafu, Je inawezekana hao ndege watu wakafuga kama Kuku au Njiwa nyumbani? Au itahitaji kibali maalumu kufuga.

Ikitokea hao waliopewa wakiwapa ndugu zao nao wakafuge kutakuwa na shida yoyote?
Nafikiri kama umefuatilia vizuri utagundua kuwa wamepewa na "vibali" vya kuwatunza. Kama na wao watawapa ndugu zao wasisahau kuomba vibali.
 
Ukifata utaratibu ni ruksa tu,mbona huku kwetu jamaa anao anajifugia tu.
Ukifuata utaratibu inakua ruksa kama zilivyo nyara nyingine za Serikali kama nyama za kuwinda na kadhalika.
 
Tausi ndege ambao asili yao ni India huku Tanzania au Africa si asili ya ndege. Mwl Nyerere wakati wa utawala wake alipotembelea India katika moja ya safari zake alipewa zawadi ya Tausi naye alikuja na kuwaweka Ikulu ya Dar. Tausi wamekuwa wakizaliana na wakati mwingine huruka toka ikulu na kuzunguka katika baadhi ya maeneo yaliyoko jirani na ikulu. Ndege hawa kwa sasa ni kama nyala za serikali, mtu binafsi kuwa nao ni mpaka uwe na kibali cha kuwafuga.
 
Kwani kwa akili yako hiyo ndogo unajua hawazaliani na kuongezeka ni kama mawe

Acha ujinga ww
Nadhani mjinga anahitaji kueleweshwa ndiomaana akauliza

Yeye swali lake ni rahisi, Tausi aliopewa Kenyatta ni wale wa Ikulu au walikuwa mali binafsi ya Magufuri? Na kama ilikuwa mali binafsi aliwatoa wapi?

Kumbuka wale wa Ikulu hata wakizaliana wakawa laki moja au milioni wanabaki kuwa mali (nyara) ya serikali na hutolewa kwa kibali maalumu kama alivyofanya Rais leo.
 
Leo ikulu chamwino mtukufu rais Magufuli amewapa zawadi ya tausi 25 kwa kila moja kwa marais watatu wastaafu na idadi hiyo kwa mjane wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere, nampongeza kwa hilo na ni jambo la kizalendo sana

Lakini nikirudisha kumbukumbu zangu vizuri nyuma nakumbuka mtukufu alimpa Kenyatta tausi wake binafsi huko Chato alipomtembelea mapumzikoni

Sasa kutokana na kuwa nauelewa mdogo uliopelekea kufeli std 7 nilielewa kuwa Tanzania kuna tausi wengi, Ila cha kunichanganya Leo nikuwa Mtukufu amesema Tanzania hakuna Tausi ila waliletwa na Baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere

Sasa naomba kueleweshwa zaidi na ninyi mliosoma zaidi kuwa Tanzania kuna Tausi wengi zaidi ya wale wa ikulu?

Au hata wale aliopewa Rais Kenyatta walikuwa Mali ya Ikulu?

Naombeni kueleweshwa
Sababu kubwa ya yale maigizo ni homa ya uchaguzi mkuu
 
Jamaa anawapongeza eti hawajavaa barakoa.

Viongozi wetu ni wanafiki sijawahi kuona.

Angalia mawaziri wote akiwemo pm wakiwa bungeni au mahala popote wanavaa barakoa ila wakienda kwa rais wanavua ili kumfurahisha mshikaji.

Hao wazee jamaa anataka wanase covid-19 waage Dunia.
Ni sehemu ya maajabu. Ndugai na Majaliwa Bungeni barakoa hawaziachi kabisa ila nadhani kuanzia leo hawatavaa tena
 
Mkulu alijimilikisha..... Baada ya kuona watu hawakufurahishwa na hilo ameamua kuwa wenzake ili asione lane kama ni yeye peke yake mwenye hao Tausi. Nyerere aliwaachia pale hakuwa chukua na waliofuata wa kafanya vile vile. Jamaa kaamua kuwapa kinguvu na hakuna wa kuataa maana kama walikuwa wanawataka wangefanya hivyo wakati wa utawala wao.
Halafu katibu wa Ikulu akaleta mawenge pale eti muheshimiwa ana roho nzuri, amewagawia wenzake ila yeye hajajigawia kwamba ufanyike utaratibu na yeye apate kabla hajastaafu. Hii awamu viongozi wengi wanajifanya hamnazo
 
Nadhani mjinga anahitaji kueleweshwa ndiomaana akauliza

Yeye swali lake ni rahisi, Tausi aliopewa Kenyatta ni wale wa Ikulu au walikuwa mali binafsi ya Magufuri? Na kama ilikuwa mali binafsi aliwatoa wapi?

Kumbuka wale wa Ikulu hata wakizaliana wakawa laki moja au milioni wanabaki kuwa mali (nyara) ya serikali na hutolewa kwa kibali maalumu kama alivyofanya Rais leo.
Maelezo yalitolewa siku ile ile
 
Ujue mtu akishindwa kazi ya kupima watu Covid-19, lazima azushe zushe vitu vingine ambavyo havina kichwa wala mguu ili mradi ajiineshe kafanikiwa tu.

Watu wako katika pandemic, yeye anaita wastaafu kuwapa tausi?

Hao wazee wengine wanakaribia miaka 100 wakipata kirusi hapo na kufa atakubali kuchukua lawama?
Hiki mnachoita pandemic ni kama ukichaa ambao umeingia duniani. Kwa akili za kawaida huwezi kuwafungia raia wako ndani miezi 3 kisa mafua
 
Wastaafu wenzie walivitunza na kuwaacha Tausi hapo Ikuli; ila yeye ameyachukua nakuyapeleka kwake Chato sijui kwa kigezo gani. Kama akisema Chato ni Ikulu ndogo mbona Ikulu ndogo zingine za mikoani hawapo?
Ameona aibu kua yeye amekua wa mwisho kuingia Ikulu ila amekua wa kwanza kujigawia na kugawa Tausi adi kwa marafiki wake tofauti na watangulizi wake...leo ameona na watangulizi wake awape ili ahalalishe Tausi kuonekana kwenye bustani na makazi yake.
 
Kwa nini wasifuge kware, maana unaweza kuta mayai ya kware ni dawa ya korona
 
Back
Top Bottom