Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,160
Alafu sioni sababu ya kugawa-gawa tausi ndege flani ambaye watu wanapaswa kuja kumuona hapa tz magogoni na sio kutoa mbegu wakafugwe nchi zingine, tunapoteza ule upekee wake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alafu utakuta mtu hata hawataki anajikuta anasukumiziwa mitausi inaenda kumkata hesabu ya kuwatunzaWastaafu wenzie walivitunza na kuwaacha Tausi hapo Ikuli; ila yeye ameyachukua nakuyapeleka kwake Chato sijui kwa kigezo gani. Kama akisema Chato ni Ikulu ndogo mbona Ikulu ndogo zingine za mikoani hawapo?
Ameona aibu kua yeye amekua wa mwisho kuingia Ikulu ila amekua wa kwanza kujigawia na kugawa Tausi adi kwa marafiki wake tofauti na watangulizi wake...leo ameona na watangulizi wake awape ili ahalalishe Tausi kuonekana kwenye bustani na makazi yake.
Next time wazee wapewe digidigi wakachinje wale kisusio na wajukuuKwa nini wasifuge kware, maana unaweza kuta mayai ya kware ni dawa ya korona
Leo ikulu chamwino mtukufu rais Magufuli amewapa zawadi ya tausi 25 kwa kila moja kwa marais watatu wastaafu na idadi hiyo kwa mjane wa baba wa taifa Mama Maria Nyerere, nampongeza kwa hilo na ni jambo la kizalendo sana
Lakini nikirudisha kumbukumbu zangu vizuri nyuma nakumbuka mtukufu alimpa Kenyatta tausi wake binafsi huko Chato alipomtembelea mapumzikoni
Sasa kutokana na kuwa nauelewa mdogo uliopelekea kufeli std 7 nilielewa kuwa Tanzania kuna tausi wengi, Ila cha kunichanganya Leo nikuwa Mtukufu amesema Tanzania hakuna Tausi ila waliletwa na Baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere
Sasa naomba kueleweshwa zaidi na ninyi mliosoma zaidi kuwa Tanzania kuna Tausi wengi zaidi ya wale wa ikulu?
Au hata wale aliopewa Rais Kenyatta walikuwa Mali ya Ikulu?
Naombeni kueleweshwa
Kikwete mtoto wa mjini pale pale mbona kampa za kimafumbo mafumbo,Alafu utakuta mtu hata hawataki anajikuta anasukumiziwa mitausi inaenda kumkata hesabu ya kuwatunza
Kwani wapi nimeandika watu wafungiwe ndani miezi mitatu?Hiki mnachoita pandemic ni kama ukichaa ambao umeingia duniani. Kwa akili za kawaida huwezi kuwafungia raia wako ndani miezi 3 kisa mafua
kenge kweli, kati yangu na wewe nani anawashwa sasa, we si ndio umemtaja kwenye mjadala ambao hausikiInaelekea huwa kuna kitu anakufanyia. Sio kwakuwashwa huko
Haha ni wazi hawa tausi wamegeuka kuwa mzigo kwa wastaafu yani zawadi imewalemeaKikwete mtoto wa mjini pale pale mbona kampa za kimafumbo mafumbo,
Mara ya kwanza wakati anatoa shukurani kwa niaba ya wenzake alisema, "sasa hawa tausi na kule kwangu msoga na vicheche wale, sijui ila hayo tuachie sie"
Halafu mara ya pili wakati amekaribishwa kutoa salamu akasema, "tunashukuru kwa zawadi ya tausi lakini wengine hatuna utaalamu wa kuwafuga hawa. Tumezoea kufuga kuku, kanga na bata. Hawa tausi hawa muheshimiwa Rais itabidi tuombe na wataalamu wa Ikulu watusaidie utaalamu". Mwisho wa kunukuu
Hizi statement za mzee wa Msoga zina ujumbe ndani yake
Duh,tuwakumbushe watuambieHalafu katibu wa Ikulu akaleta mawenge pale eti muheshimiwa ana roho nzuri, amewagawia wenzake ila yeye hajajigawia kwamba ufanyike utaratibu na yeye apate kabla hajastaafu. Hii awamu viongozi wengi wanajifanya hamnazo
Usafiri ndege kama ilivyokuwa mabox matatu(@ 5kg) ya kikombe cha babu wa Madagascar.Hahaha, nadhani jamaa walikuwa wakimshangaa tu kimoyomoyo
Tausi wenyewe walikuwa wameshakaa nao pale Ikulu, Wala sio kitu kipya kwao..eti tausi 25 kila mmoja