Sijamuelewa Mtukufu juu ya Tausi wa ikulu

Ilikuwa hatari kwa afya za wazee wastaafu bila barakoa. Niliwaona walivyojiachia bila kinga; hasa mzee Mwinyi
 
Hahaha, nadhani jamaa walikuwa wakimshangaa tu kimoyomoyo
Tausi wenyewe walikuwa wameshakaa nao pale Ikulu, Wala sio kitu kipya kwao..eti tausi 25 kila mmoja
Huwezi kujua, pengine masharti ya mganga wake.
 
Shukrani kwa mchango
Japo upo partially kwenye mada

Nikuulze Covid si imeyeyuka kwa maajabu Tz?
Nipo partially kwenye mada maana yake nini?

Define maajabu, unajuaje hili jambo ni ajabu na hili si ajabu?
 
Jamaa anawapongeza eti hawajavaa barakoa.

Viongozi wetu ni wanafiki sijawahi kuona.

Angalia mawaziri wote akiwemo pm wakiwa bungeni au mahala popote wanavaa barakoa ila wakienda kwa rais wanavua ili kumfurahisha mshikaji.

Hao wazee jamaa anataka wanase covid-19 waage Dunia.
 
Mkulu alijimilikisha..... Baada ya kuona watu hawakufurahishwa na hilo ameamua kuwapa wenzake ili asionekane kama ni yeye peke yake mwenye hao Tausi. Nyerere aliwaacha pale hakuwachukua na waliofuata wakafanya vile vile. Jamaa kaamua kuwapa kinguvu maboss wake wa zamani na hakuna wa kuataa maana wanajua. Kama walikuwa wanawataka hao Tausi wangefanya hivyo wakati wa utawala wao.
 
Nafikiri kama umefuatilia vizuri utagundua kuwa wamepewa na "vibali" vya kuwatunza. Kama na wao watawapa ndugu zao wasisahau kuomba vibali.
 
Ukifata utaratibu ni ruksa tu,mbona huku kwetu jamaa anao anajifugia tu.
Ukifuata utaratibu inakua ruksa kama zilivyo nyara nyingine za Serikali kama nyama za kuwinda na kadhalika.
 
Tausi ndege ambao asili yao ni India huku Tanzania au Africa si asili ya ndege. Mwl Nyerere wakati wa utawala wake alipotembelea India katika moja ya safari zake alipewa zawadi ya Tausi naye alikuja na kuwaweka Ikulu ya Dar. Tausi wamekuwa wakizaliana na wakati mwingine huruka toka ikulu na kuzunguka katika baadhi ya maeneo yaliyoko jirani na ikulu. Ndege hawa kwa sasa ni kama nyala za serikali, mtu binafsi kuwa nao ni mpaka uwe na kibali cha kuwafuga.
 
Kwani kwa akili yako hiyo ndogo unajua hawazaliani na kuongezeka ni kama mawe

Acha ujinga ww
Nadhani mjinga anahitaji kueleweshwa ndiomaana akauliza

Yeye swali lake ni rahisi, Tausi aliopewa Kenyatta ni wale wa Ikulu au walikuwa mali binafsi ya Magufuri? Na kama ilikuwa mali binafsi aliwatoa wapi?

Kumbuka wale wa Ikulu hata wakizaliana wakawa laki moja au milioni wanabaki kuwa mali (nyara) ya serikali na hutolewa kwa kibali maalumu kama alivyofanya Rais leo.
 
Sababu kubwa ya yale maigizo ni homa ya uchaguzi mkuu
 
Ni sehemu ya maajabu. Ndugai na Majaliwa Bungeni barakoa hawaziachi kabisa ila nadhani kuanzia leo hawatavaa tena
 
Halafu katibu wa Ikulu akaleta mawenge pale eti muheshimiwa ana roho nzuri, amewagawia wenzake ila yeye hajajigawia kwamba ufanyike utaratibu na yeye apate kabla hajastaafu. Hii awamu viongozi wengi wanajifanya hamnazo
 
Maelezo yalitolewa siku ile ile
 
Hiki mnachoita pandemic ni kama ukichaa ambao umeingia duniani. Kwa akili za kawaida huwezi kuwafungia raia wako ndani miezi 3 kisa mafua
 
Wastaafu wenzie walivitunza na kuwaacha Tausi hapo Ikuli; ila yeye ameyachukua nakuyapeleka kwake Chato sijui kwa kigezo gani. Kama akisema Chato ni Ikulu ndogo mbona Ikulu ndogo zingine za mikoani hawapo?
Ameona aibu kua yeye amekua wa mwisho kuingia Ikulu ila amekua wa kwanza kujigawia na kugawa Tausi adi kwa marafiki wake tofauti na watangulizi wake...leo ameona na watangulizi wake awape ili ahalalishe Tausi kuonekana kwenye bustani na makazi yake.
 
Kwa nini wasifuge kware, maana unaweza kuta mayai ya kware ni dawa ya korona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…