Sijamwelewa wife jamani. ..

Mkuu mtoto darasa la pili na hakuna mdogo wake,mmmhhh kulikoni Mkuu? ni utashi au matatizo,maana..........

mipango ya maisha kaka, atakuja tuu kuna mambo ambayo tunafanya tukaona tuvute pumzi kidogo, hiyo ni mipango ya mwakani, itatimia tuu
 
Yamekuwa hayo?
 

Kaka asante sana mkuu, ushauri nimeupata na nimeshaongea nae, nimeamua kuwa mpole, lakini nitapima kwa siri sana ili nijue moja. Ila hata kama atakuwa si wangu itabidi tuu niwe mpole, 9yrs in marriage sitaweza kuanza afresh, ila ntafanya mpango nipate kupy yangu fasta
 
Lakini na kina baba muwe mnachagua maneno ya kuwambia watoto. hivi unavyomwambia mtoto utadhani we si mwanangu una maana gani, that is a kid for god's sake, why would you use such language in front of the kid?

Nakubali nilikosea wanaJF, nimeomba radhi tayari maana Mungu hakunijaliaga ule udhaifu wa wanaume wengi wa kogoma kuomba radhi, nimeona madhara yake, sitarudia, lakini pia inaweza kuwa imenisaidia!
 
Babukijana hakuna kiumbe mwenye roho ngumu kama mwanamke,we fikiria ni nadra sana tena sana mwanaume na akili zake kukubali kulala ndani ya chumba ambamo kuna suruali,viatu,koti n.k vya mwanaume mwingine,lakini mkeo akisafiri tena kwenye matrimonial home mlete mwanamke uone kama atakataa kulala,atajipigia usingizi vizuri tu!Hao ndo mama zetu mazee.
 

Mkuu hapo pia kuna ukweli ndani yake! Japo kwangu sijawahi ona, lakini kweli hayo mambo yanatokea.
 
By the way Calnde umesema my wife wako kajenga bonge la jumba Njiro,ushawahi kujiuliza alifanya biashara gani kupata huo mkwanja,maana isije ikawa kulikuwa na msaada tutani mazee!
 
mipango ya maisha kaka, atakuja tuu kuna mambo ambayo tunafanya tukaona tuvute pumzi kidogo, hiyo ni mipango ya mwakani, itatimia tuu
All the best Calnde na mai wife wako,i truly wish you happyness!
 
Shishi nakuona uko jamvini kwenye hii thread,mwaga lazi basi!
 
Ukweli ni kwamba Mama yako mpaka siku ameondoka duniani ndo utajua baba ulienae ndo waku au lah
 
By the way Calnde umesema my wife wako kajenga bonge la jumba Njiro,ushawahi kujiuliza alifanya biashara gani kupata huo mkwanja,maana isije ikawa kulikuwa na msaada tutani mazee!

Mkuu sina shaka na hilo. . .
Ni mwajiriwa wa juu tuu huko kwa serikali na kuna some investments ana anazo ambazo nw nimetop up mtaji tunarun pamoja. Hilo halina shaka
 
Mkuu sina shaka na hilo. . .
Ni mwajiriwa wa juu tuu huko kwa serikali na kuna some investments ana anazo ambazo nw nimetop up mtaji tunarun pamoja. Hilo halina shaka
Kama ni hivyo Mkuu tuliza ball,ganga yajayo.
 
Calnde pole aisee. maoni yangu ni kuwa uliyatamka yalookuwa moyoni mwako. kama ulikuwa unajihisi kuwa mbona mwanao hafanani na wewe hata chembe ( phenotypically speaking)... ulikurupuka kuyatoa mawazo yako...thinking out loud....hata mie ningejisikia vibaya sana mr. akisema hivyo. so sasa hapo u have to build that trust again kwa sbabu just saying that imetia nuksi ya kuwa ah! kumbe huniamini... bila trust your marriage cd be heading for a very rocky and rough ride. find ways of buidling the trust u just shattered. akikataa we ni PM tu ahahahhah!

mambo ya DNA...mmmmnh ukipata si wako???? u have to be prepared for whaterver outcome.
 
mkuu kweli nukigundua nieendelee, hapo sitaweza, atakufa mtu ati! Fikiria mtoto yupo darasa la pili, namlipia pesa nyingi mpaka nachanganyikiwa, alafu nieendelee nae! itakuwa kazi nzito. . .
Mungu saidia tuu awe wangu


Kwa nini uuwe? kama si wako jihesabu umetoa sadaka kwa yatima. Huyo mama kama amekudanganya hakufai kabisa achana naye. Tafuta mwaminifu. Utampata tu. Kama amenuna siku 3 kwa sababu ya kukaripia mtoto juwa huyo ana lake jambo na hilo la mtoto ni kisingizio tu. Au kuna zaidi ya hilo uliloeleza ambalo huwezi kulimwaga hadharani. Tuna watoto tunawagombeza na hata kuwachapa, lakini hakuna anayenuna hata kwa nusu saa baada ya tukio. Ikizidi mama au baba atamuombea msamaha mtoto na kuongeze tu usirudie tena hili, ukirudia sikuombei msamaha na hata mimi nitakuchapa zaidi ya hivi. Yamekwisha na maisha yanaendelea.

Mzee jichunguze vizuri unaweza kugundua mengi. Kama huna ubavu mezea, kula jiwe ili maisha yaendelee. kama huwezi zungumza naye ujue sababu ya kununa siku 3, ikishindikana washirikishe jamaa zenu wa karibu, ili maisha yaendelee.
 
Hapana ndugu,
Mie nje simegi kabisa. Hata kama umefatilia thread zangu hapa nalaani kabisa hiyo mambo, iweje leo yeye afanye hivyo. . . .
mkuu pole sana lakini kwa ninavyokujudge, inaonekana ulikuwaq na wasiwasi na huyo kid kwa muda mrefu tu na mkeo alishahisi hivyo, labda ulikuwa unamkaguakagua sana mtoto mara vidole, mdomo, mikono na vitu vingi tu na inelekea mama alikuwa anakuona na kusubiri kauli yako na nadhani kinachokuuma zaidi ni pale wadau wanapokwambia ujafanana na mtoto wako kabisa,
kitu kingine cha kujiuliza utasemaje labda sio mwanangu, wanao kwani wanabehave vipi na wakati huna mtoto,
mkuu nadhani unajipa presha kubwa tu, nenda kapime DNA, hiyo ndio itakuweka huru
 

Ndugu..alireact vile kwa sababu ulimtolea negligent statement.... hukujua itam affect vipi.
Siku zote ujizuie kutoa matamshi kama yale.Mwanamke yeyote atakasirika kusikia mumewe anasema.."utadhani huyu mtoto siyo wangu"!
 
Ndugu..alireact vile kwa sababu ulimtolea negligent statement.... hukujua itam affect vipi.
Siku zote ujizuie kutoa matamshi kama yale.Mwanamke yeyote atakasirika kusikia mumewe anasema.."utadhani huyu mtoto siyo wangu"!

Waswahili siku zote wanasema ukweli unauma kama si kweli kwanini upate shida za kupoza amani yako na ya mwenzio? Hapa suala si kauli wala nini ila mzee inaonesha aligusa pabaya..
 
Napenda kutofautiana na wachangiaji wote, isipokuwa BABUKIJANA na MVINA.

Huyo mke kakasirika kwasababu yuko guilty na sasa yuko tayari kutimiza alilokuwa anashindwa kulitimiza (kuvunja ndoa) kwa kujifanya kutumia hasira au kukufanya uwe mtoto mwingine ndani ya ndoa na hivyo kumpa taji la utawala.

Ukimpenda mtu, utamsamehe na wala haitachukuwa mwezi kumsamehe. Kama anakupenda kweli ilitakiwa kwanza achukulie kama utani, na kama akiona kwamba ulikuwa hautanii basi angekaa na kukutoa wasiwasi. Hajafanya hivyo na badala yake anakasirika ili kukuchosha na kukufanya wewe uchukuwe uamuzi wa kumwacha. Waingereza wanasema the GUILTY SPEAKS LOUDER.

Ushauri wangu; wewe wala husisumbuke na DNA badala yake jiulize kama kweli ndoa iko. Wanawake asilimia kubwa wakifanya madudu nje ya ndoa wanatoa visingizio vya kawaida ndani ya ndoa na mara nyingi visingizio ni kukasirika kusiko isha, kuzua issues kiibao zisizo na msingi, na emotions kibao zisizo eleweka. Hivyo basi yawezekana 100% huyo mtoto ni wako lakini mke anajambo ambalo anahisi unakaribia kulijuwa, na hivyo lazima akudhibiti kwa kukulazimisha utubu kwa kosa ambalo hujalifanya.

Take my words.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…