kaka we umeliwa kuanzia sasa chokochoko zote kwa mkeo uache kama bado unapenda muishi pamoja,yaani huyo kweli master yake kaitumia vizuri,kitendo cha wewe kukubaliana nae kuuza nyumba ukae kwake pole sana bro inabidi uwe mpole hata kama kakauchezea faulo maana mi yashanikuta kama yako nae alikua binti wa hukohuko arusha,nakumbuka mwishomwisho wa mapenzi mama alinifukuza kama mbwa nyumbani na nguo zilitupwa nje uwanjani na majirani wanaona,nnachoshukuru mtoto sina shaka nae kabsaaa maana nilipiga kopi ya nguvu,sema baaada ya kuzaa mama alikuja na revolution ndio tukaachana,sasa ushauri wangu huyo kashakuzidi ujanja,ukianza kuingiza mambo ya kupima d.n.a na nini umekwisha mama atajua tuu,mtoto tayari mkubwa huyo hata ufanyeje atamwambia,na gia zao ndo hizo kwanza lazima unyimwe unyumba ili uzidi kukasirika na yeye akuwashie moto na ikiwezekana kukutimua kabisa,inawezekana upole wake ni imani tu alikua anakuwekea sababu hujawahi leta ukorofi sasa ukilianzisha hilo kashapata sababu,yaani nakuonea huruma kitanzi kinakunyemelea,mi nilipata uchizi kabisa mpaka nikaombewa na kufanyiwa counselling ya nguvu ndo nikapiga moyo konde na mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.