Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Ukweli ni kwamba Polepole ameanza kunikumbusha enzi za Nyerere katika misimamo yake na kuonyesha anasimamia sheria na taratbu na miiko na maadili (integrity) katika uongozi.
Sasa anazidi kujionyesha kuwa tofauti sana na genge la wahuni walioishika serikali na nchi kwa ujumla, na ni wazi wanamchukia sana. Tanzania imekamatwa sana na genge hili linalotia watu waliokuwa wakuu wa nchi, wafanya biashara na viongozi mbalimbali wa dola hususa vyombo vya usalama.
Tanzania imefikia mahali ambapo unaweza kuona wazi kabisa kwamba tunaongozwa na kikundi cha namna ya Mafia ya Marekani au Urusi Tunaongozwa na watu wachafu wasio na aibu katika kufanya uovu, wamjejaa ufisadi, ukatili na hata hawaogopi kuua! Hawa ndio watu wanaweza kutoa majibu kama kupokea fedha chafu kwa ajili ya CCM hakuna ubaya kwa sababu wao ni wachafu kuliko hata hao wanaowapa fedha!
Tunaongozwa na genge la wahalifu lisilojali miiko au maadili yeyote ya uongozi, na kinachosikitisha ni kwamba kuna watanzania wengi wajinga sana wanalidhangilia hili genge, aidha kwa kutokujua au kwa sababu wanafaidika kibinafsi na genge hili la waovu, ambalo wengine wao wala sio wanachama wa CCM bali wanaitumia CCM.
Mtanzania yeyote anaepingana na yake Polepole anaeleza aidha ni mjinga sana au nae ana damu ya uovu kama hili genge la Mafia lililoshikilia nchi kwa sana. Polepole anapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania alie mwadilifu na anaeitakia nchi yetu mambo mema.
Kama hauko na Polepole, uko na genge la wahuni, mafia wa Tanzania, na huo ndio ukweli.